Vurugu zimesababisha walinzi wa chama hicho (Green Guard) kuzuiwa kufanya kazi yao na badala yake mgambo wa Jiji la Mwanza kusimamia uchaguzi huo. Akizungumza nje ya ukumbi leo Jumatano, Katibu wa wajumbe hao, Samora Msiba amesema baada ya kuhoji sababu ya wao kuzuiwa kuingia ukumbini walielezwa kiongozi wao wa kata hana mawasiliano au mahusiano mazuri na Serikali.
“Tunaomba viongozi wa ngazi za juu waliangalie suala hili kwa kuwa hata sisi tuna haki ya kupiga kura na si kusukumwa na kususiwa ovyo kwa kuhusishwa na kesi zisizotuhusu,” amesema Msiba
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mahina, ambaye pia ni Katibu wa Green Guard wilayani Nyamagana, Kagambo Paul amesema amekerwa na kitendo cha kuporwa jukumu lake la kusimamia uchaguzi na kupewa jeshi la akiba la mgambo ambalo halihusiani na chochote kwenye uchaguzi huo.
Uchaguzi kwa mara ya kwanza ulifanyika Septemba 23 ambao mshindi hakupatikana kutokana na kura kutofikia nusu ya zilizopigwa.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala amesema uchaguzi umerudiwa kwa sababu hakuna mgombea aliyepata nusu ya kura zilizopigwa.
Wagombea hao waliopitishwa na Halmashauri Kuu ya Mkoa ni Hassan Mambosasa aliyepata kura 37 kati ya 336 zilizopigwa, mwingine ni Philipo Magori aliyepata kura 137 na Yusuph Rudumo aliyepata kura 148.
Wanaorudia uchaguzi ni Philipo Magori na Yusuph Rudumo. Matokeo bado hayajatangazwa.
No comments:
Post a Comment