Msaada huo umekabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Akipokea msaada huo wenye thamani ya Sh20 milioni, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dk Ali Salim amesema utasaidia katika wodi za wazazi, saratani na watu wenye matatizo ya afya ya akili.
“Tuna upungufu wa vitanda 100 kwenye wodi hizo lakini msaada huu utasaidia kupunguza changamoto zilizopo,” amesema Dk Salim.
Benki hiyo iliyoanzishwa mwaka 1997 ilipata faida kabla ya kodi ya Sh83.3 bilioni hivyo kujiweka kwenye nafasi ya nne kwa ukubwa wa mtaji nchini.
Katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, Arafat Haji amesema wametenga Sh200 milioni kwa ajili kusaidia sekta ya afya nchini.
Amesema mikoa 13 yenye upungufu wa vitanda itasaidiwa kupitia mradi huo kwa kuwa malengo yaliyopo ni kutoa magodoro na vitanda 500 katika hospitali za umma. “Hospitali na kliniki nyingi zina upungufu wa dawa, vifaatiba na vitanda. Tumeona tuanze na vitanda ili kurahisisha huduma ya uzazi kwa wajawazito,” amesema Haji.
Baadhi ya mikoa inayotarajiwa kunufaika ni Mbeya, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga na Mtwara. Pia visiwa vya Pemba na Unguja.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuna uwiano wa vitanda saba kwa kila watu 10,000 kwenye hospitali zilizopo nchini.
No comments:
Post a Comment