Tuesday, September 12

SANAA MASHULENI

SHINDANO LA SANAA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA MIKOA YA UKANDA WA PWANI BARA NA VISIWANI: WITO WA KUWASILISHA KAZI ZA UBUNIFU WA SANAA

Chama cha Wanayansi wa Elimu Bahari ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (WIOMSA) kwa ushirikiano kati ya WIOMSA, Taasisi ya Sayansi Bahari (IMS) na Idara ya Sayansi Akua na Teknolojia ya Uvuvi (DASF) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na ya Ukanda wa Pwani wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (Mkataba wa Nairobi), kinaandaa Kongamano la 10 la Kisayansi. 

Kongamano hilo litafanyika kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi tarehe 4 Novemba katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ulioko Dar es Salaam, Tanzania.

Katika Kongamano hili la 10 kutakuwa na mashindano ya kazi za sanaa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za mikoa ya ukanda wa pwani wa Bahari ya Hindi. Kwa upande wa Tanzania Bara itahusisha mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara na kwa Zanzibar itahusisha shule zilizopo Unguja na Pemba. Dhamira ya mashindano hayo ni: “Umuhimu wa Mazingira ya Pwani na Bahari kwa Tanzania”. 

Bahari ni muhimu sana kwa jamii zetu na kwa ustawi wa maisha yako. Kwa hiyo tumia mawazo yako, ubunifu wako na maarifa uliyo nayo katika kuwasaidia wengine waelewe mawazo yako kuhusiana na umuhimu wa mazingira ya ukanda wa pwani na ya bahari kupitia kazi yako ya sanaa. Chora, paka rangi, tumia program za kompyuta za uchoraji au eleza mawazo yako hayo kwa kutunga wimbo.
Wanafunzi watumie ubunifu wao wenyewe kueleza maoni yao juu ya dhamira husika. Uwasilishaji wa ubunifu huo unaweza kufanyika kwa njia zifuatazo: michoro (zikiwemo katuni/vibonzo) au utunzi wa nyimbo.

Kazi zote za sanaa ziwasilishwe kabla ya tarehe 30 Septemba 2017 kwa njia ya mtandao ambao ni http://symposium.wiomsa.org/art-competition/

Kwa maelezo zaidi juu ya vigezo na masharti ya kushiriki na mfumo wa uwasilishaji wa sanaa, pakua tangazo kamili la shindano hili kwa kubofya link hii chini:

No comments:

Post a Comment