RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Mh. Anthony Mtaka, kwa kutambua mchango mkubwa wa wadau mbalimbali katika maendeleo ya mchezo wa riadha hapa nchini, ameandaa kusanyiko (kikao cha pamoja), na waandaaji mbalimbali wa mbio ndefu hapa nchini.
Waandaaji wa matukio mbalimbali ya mchezo wa raidha hapa nchini, kwa namna moja ama nyingine wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya mchezo wa riadha hapa nchini na jamii kwa ujumla, hivyo kwa kutambia hilo, RT imeona kuna umuhimu mkubwa Kamati yake ya Utendaji ikakutana na waandaaji hao katika uboreshaji
Itakumbukwa kwamba, hivi sasa kumekuwa na uibukaji mkubwa wa watu mbalimbali kuandaa matukio hayo ya riadha bila kufuata taratibu na kanuni zilizopo kisheria na kikanuni hivyo kupoteza lengo tajwa la mchango wa kimaendeleo katika mchezo na jamii kwa ujumla.
Hivyo RT inaamini kupitia kusanyiko hilo litakalofanyika Septemba 16 mwaka huu kwenye ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi litaibuka na maazimio chanya ya kuweka taratibu na miongozo sahihi kwa pande zote, ikiwamo taratibu za uandaaji wa matukio ya riadha, viwango vya matukio hayo, pia mpishano wa tukio moja na jingine bila kuingiliana (Kalenda).
Hivyo tunapenda kutoa wito kwa waandaaji wote, ambao tayari tunaamini wameishapata wito ‘official’ watajitokeza bila kukosa. RT inapenda kuwashukuru Kampuni ya MultChoice Tanzania ‘DStv’ kufanikisha tukio hili kwa manufaa ya maendeleo ya mchezo wa Riadha Tanzania.
Itakumbukwa, DStv kwa muda sasa, wamekuwa washirika wazuri katika kuchangia maendeleo ya mchezo wa raidha Tanzania, ikiwamo kufadhili kambi za timu zetu za Taifa na hata kwa wanariadha mmoja mmoja, akiwamo Mshindi wa Medali ya Shaba katika mashindano ya Dunia, Alphonce Felix Simbu .
MBIO MBALI MBALI ZINAZOENDESHWA
HAPA NCHINI
JINA LA MBIO INAKOENDESHWA
1. KILIMANJARO INTERNATIONAL MARATHON - KILIMANJARO
2. KILFM HALF MARATHON - KILIMANJARO
3. HEART HALF MARATHON - DAR ES SALAAM
4. NGORONGORO HALF MARATHON - MANYARA
5. KARATU 10KM - MANYARA
6. BABATI HALF MARATHON - MANYARA
7. TULIA HALF MARATHON - MBEYA
8. SEREBUKA HALF MARATHON - SONGEA
9. TANGA HALF MARATHON - TANGA
10. MT. MERU MARATHON - ARUSHA
11. DAR ROTARY INT. MARATHON - DAR ES SALAAM
12. BAGAMOYO HALF MARATHON - PWANI
13. 10KM - ARUSHA
14. KIA HALF MARATHON - KILIMANJARO
15. SERENGETI MARATHON - SIMIYU
16. ROCK CITY MARATHON - MWANZA
17. IGOMBE HALF MARATHON - TABORA
18. MEI DAY HALF MARATHON - DAR ES SALAAM
19. IKUNGI HALF MARATHON - SINGIDA
20. NAMTUMBO HOSPITAL FUND RAISING - SONGEA
21. ARUSHA TOURISM HALF MARATHON - ARUSHA
IMETOLEWA NA WILHEM GIDABUDAY
KATIBU MKUU RT
SEPTEMBA 12, 2017
No comments:
Post a Comment