Rais wa kenya Uhuru Kenyatta ameutaja uamuzi wa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais kuwa ''mapinduzi ya mahakama''.
Viongozi hao wawili walikuwa wakijibu uamuzi kamili wa mahakama ambapo majaji wa mahakama ya juu walitoa sababu zao kwa nini walifutilia mbali matokeo hayo ya urais.
Idadi kubwa ya majaji hao walisema kuwa matokeo hayo hayakuwa na 'uwazi wala kuhakikiwa'.
Viongozi hao wawili hatahivyo waliangazia uamuzi wa majaji wawili waliopinga uamuzi hao ambao walisema kuwa kesi iliowasilishwa katika mahakama hiyo haikuwa na uzito wowote.
Rais Kenyatta alisema kuwa hakuna uchaguzi usikumbwa na makosa madogo madogo.
"Haya ni mapinduzi ....nitayaita yanavyostahili...,alisema alipokuwa akikutana na viongozi wa chama tawala cha Jubilee waliochaguliwa kutoka Kaskazini mwa Kenya katika ikulu ya rais, jijini Nairobi.
''Hii ni sauti ya watu wachache , ambao wao wenyewe waliamua wanaweza kuchagua kiongozi kwa niaba ya Wakenya wengi. Kama huu sio udikteta basi sijui ni nini'' , alisema.
- Uhuru Kenyatta: Tuheshimu matokeo
- Rais Uhuru Kenyatta aionya mahakama
- Kenyatta atangazwa mshindi wa urais Kenya
- Uhuru Kenyatta: Idara ya mahakama ina 'tatizo'
Amesema kuwa mafanikio yote ya katiba mpya ilioidhinishwa 2010 yamepotezwa na uamuzi huo ambao umewawacha watu wachachee kuongoza dhidi ya walio wengi.
''Uamuzi huo umeonyesha kwamba sauti ya wengi haijalishi tena.Kile muhimu ni sauti ya wachache, ambao wanajipatia mamlaka wasiokuwa nayo'', alisema.
Amesema kuwa katiba ilikuwa imeweka maadili ya kidemokrasi , ugatuzi na kuwapatia raia haki na uhuru na kupunguza mamlaka ya urais ili raia waamue wanavyotaka.
Amemwambia jaji Maraga kwamba uamuzi huo hauendi sambamba na katiba mpya.
No comments:
Post a Comment