Meya wa mji mkuu wa Uganda Kampala amekamatwa leo asubuhi na bado yuko katika mahabusu ya polisi.
Polisi inasema kuwa ilikuwa na taarifa kwamba Erias Lukwago angeongoza maandamano ya kupinga kikomo cha umri anayepaswa kugombea urais.
Wanasema kuwa wamebaini fulana zilizochapishwa maneno ya "kupinga kikomo cha umri wa rais" katika ofisi zake za City Hall.
Yuko mahabusu na hawezi kujibu shutuma hizi.
Kukamatwa kwa Meya Lukwago kunakuja wakati Mbunge Raphael Magyezi kutoka chama tawala cha NRM akitarajiwa kuwasilisha hoja yake bungeni akitaka apewe kipindi cha mapumziko kwa ajili ya kuandaa muswada wa kuondoa kikomo cha umri wa rais.
Kwa sasa kikomo cha umri wa rais nchini Uganda ni miaka 75.
Rais Yoweri Museveni anasema kuwa ana umri wa miaka 73. Hii ina maana kuwa, kwa sheria ilivyo sasa ,hataweza kugombea katika uchaguzi ujao.
Kuna hali ya wasi wasi kote mjini Kampala, ambako polisi wamesambazwa mjini humo.
Polisi wa kikosi cha kupambana na ugaidi wamezingira jengo la bunge huku askari polisi wengine wakifanya doria mjini.
Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Kampala Patience Atuhaire anasema kuwa hata wabunge wanaoingia bungeni wanasakwa na maafisa wa usalama kabla ya kuingia.
No comments:
Post a Comment