Mamlaka nchini Sri Lanka zimemkamata mwanamume ambaye alijaribu kusafirisha dhahabu na vito vya karibu kilo moja, alivyokwa ameficha sehemu ya nyuma ya siri.
Maafisa wa forodha walipata gramu 904 za dhahabu yenye thamani ya dola 29,370 ndani sehemu ya nyuma ya siri.
Mwanamume huyo raia wa Sri Lanka mwenye umri wa miaka 45, alikuwa safarini kwenda nchini India, lakini akasimamishwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Colombo.
Kumekuwa na visa kama hivyo miaka ya hivi karibuni.
Watu hununua dhahabu maeneo kama Dubai na Singapore ambapo bei ni ya chini na kisha kuisafirisha hadi India ambapo bei yake ni ya juu.
Maafisa wa forodha waliiambia BBC kuwa walimshuku mwanamume huyo kwa sababu alikuwa akiotembea kwa njia isiyo ya kawaida.
Vifaa vya kutambua chuma kisha vinatambua mkoba uliokuwa umefungwa mfuko wa plastiki na kufichwa sehemu ya nyuma ya siri.
Wiki iliyopita mwanamke mmoja raia wa Sri Lanka alipatwa na maafisa wa forodha akiwa ameficha gramu 314.5 za dhahabu sehemu ya nyuma ya siri.
No comments:
Post a Comment