Shughuli ya kupiga picha Bwana na Bibi harusi iligeuka ghafla wakati bwana harusi aliporuka na kuingia mtoni kumuokoa mvuana mdogo aliyekuwa anazama.
Clayton na Brittany Cook walikuwa wanapiga pozi kwa picha zao walizokuwa wanapigwa baada ya harusi katika daraja la bustani huko Cambridge, Ontario, wakati bwanaharusi alipomuona mtoto huyo akitaa taa ndani ya mto.
Pasi kufikiria hata suti aliyovaa, Bwana Cookaliruka mtoni na kumvuta mtoto huyo hadi ufukweni.
Mpiga picha alilinasa tukio zima kwa kamera.
Zimesambazwa kila mahali.
"Kwa dakika kadhaa watoto hawa walikuwa wanatufuata, na nilikuwa nawatupia jicho kwasababu walikuwa wamesimama karibu na mto," Clayton ameiambia BBC.
"Alafu wakati Brittany alipoanza kupigwapicha peke yake, nikaona watoto wawili walikuwa wamesimama kwenye mbao ya daraja.
" Nikamuona mtoto ndaniya maji akitapa tapa kuinua kichwa chake juu ya maji, hapo ndipo niliruka ndani ya maji.
" Nilimvuta nje na akawa sawa."
Mkewe Clayton anasema awali alifikiria kuwa aliruka mtoni ki mzaha.
"Tunataka kuamini kwamba mtu yoyote mwingine angeamua kuchukua hatua kama hiyo," alisema.
"Punde tu nilipowqeza kugeuka, tayari alikuwa ameshamvuta nje ya mto," Mpiga picha Darren Hatt ameiambia BBC.
"Kwahiyo niliendelea tu kupiga picha tukio zima."
Baada ya kuokolewa, mtoto huyo alionekana na uoga kiasi lakini alikuwa sawa kwa jumla, na akaondoka na nduguye mkubwa.
Bi Cook amesema kujitolea kwa mumewe na uwezo wake wa kufikiria haraka ndio baadhi ya mambo yaliomfanya akubali kuolewa naye.
No comments:
Post a Comment