Mtuhumiwa huyo ambaye ni mlemavu wa miguu na mkazi wa Kata ya Mandewa, Manispaa ya Singida alimchoma kisu kwa hasira Selemani.
Mke wa mtuhumiwa huyo, pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi juu ya mauaji hayo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Isaya Mbughi alisema tukio hilo lilitokea juzi maeneo ya Mandewa, Tarafa ya Unyakumi.
Mbughi alisema mtuhumiwa huyo alitumia mbinu ya kumvizia Selemani wakati akijamiina na na mkewe, ndipo amshambulia.
“Kuna kila dalili mtuhumiwa alipewa taarifa na majirani zake kwamba mbaya wake ameingia nyumbani kwake. Alipofika aliwakuta wakifanya tendo la ndoa juu ya kitanda chake. Haraka alifunga mlango na kuanza kumshambulia kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za kifuani,” alisema.
Alifafanua alikimbizwa Hospitali ya Mkoa, lakini alifariki dunia njiani kutokana na kuvuja damu nyingi.
Mbughi aliwataka wanandoa kubaki njia moja na watambue kuwa michepuko ni hatari na inaua.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Mandewa, Mosi Nkii alisema wakati akipita nyumbani kwa mtuhumiwa alisikia sauti ya mwanamke ikiomba asaidiwe kuamua ugomvi kati ya mume wake na mwanaume mmoja.
“Nilipoingia nyumbani hadi chumbani anakolala, nilikuta amemwangusha chini Selemani, huku amemkamba miguu. Kifuani upande wa kulia kulikuwa na jereha kubwa lililokuwa likitoka damu nyingi. Pia kushoto kulikuwa na majeraha mawili nayo yalikuwa yanatoka damu,” alisema.
No comments:
Post a Comment