Tuesday, September 12

Mtoto wa msichana wa miaka 13 afariki dunia India

Watu wataka haki itekelezwe kwa watoto wabaonajisiwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu wataka haki itekelezwe kwa watoto wabaonajisiwa
Mtoto wa msichana wa miaka 13 raia wa India ambaye alinajisiwa na kushika mimba lakini baadaye akaruhusiwa kuitoa mimba hiyo, amefariki siku mbili baada ya kutolewa kwenye mji wa uzazi wa msichana huyo.
Mtoto huyo, aliyetolewa kwa njia ya upasuaji, amekuwa katika chumba cha kuwatunza watoto wachanga walio katika hali mahututi huko Mumbai na alifariki siku ya Jumapili.
Msichana huyo ambaye alikuwa mimba ya wiki 32, alijifungua mtoto mwanamume kupitia njia ya upasuaji siku ya Ijumaa, hospitali hiyo imesema.
Mwanamume anayefanya kazi na babake, amekatwa kwa kutekeleza ubakaji huo.
India kwa kawaida inaruhusu utoaji wa mimba baada ya wiki 20 na iwapo tu maisha ya mama yamo hatarini.
Kesi hiyo iligonga vichwa vya habari baada ya mimba yake kugundulika mwezi Agosti 9 pale wazazi wake walipompeleka kwa daktari kupokea matibabu kutokana na ongezeko la uzani kupita kiasi.
Wakili ambaye makao yake ni mjini Delhi alifika mbele ya mahakama kuu kumuwakilisha, akitaka msichana huyo aruhusiwe kumtoa mtoto huyo.
Katika uamuzi wa mahakama ambao hautasahaulika, korti hiyo ilimpatia ruhusa siku ya Jumatano kupata usaidizi wa madaktari kutoa mimba hiyo.
Madaktari hao walikuwa wamesema asubiri kwa wiki mbili zaidi ili kupatia kijusi muda kukua zaidi lakini majaji waliamrisha utoaji wa mimba hiyo ufanyike kwa haraka ili kumsaidia msichana huyo kuepukana na mshtuko.
Kikosi cha madaktari watano, wakiongozwa na daktari wa watoto Dkt Ashok Anand , walifanya upasuaji huo katika hospitali ya JJ huko Mumbai.
Kwa kuwa mimba yake ilikuwa katika kiwango cha juu, utoaji wa mimba hiyo ulisababisha kuzaliwa kwa mtoto huyo wa kiume, Dkt Anand aliambia BBC siku ya Jumatatu.
''Msichana huyo anaendelea kupata afueni na atatolewa hospitalini katika siku zijazo.''
Daktari huyo alisema mtoto huyo mvulana alizaliwa na uzani mdogo wa kilo 1.8(41b).
Haijabainika kilichosababisha kifo cha mtoto huyo, lakini ripoti kutoka gazeti la Times of India limewanukuu madaktari waliosema mtoto huyo alikuwa na matatizo ya mapafu na shida kubwa ya uvutaji wa pumzi.
Watoto wa India wanaonajisiwa wanaomba haki yao.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWatoto wa India wanaonajisiwa wanaomba haki yao.
Katika ripoti nyengine, gazeti hilo limesema ''familia ya msichana huyo ilionyesha mabadiliko ya kutaka kumlea mtoto huyo.''
Wafanyikazi wa hospitali hiyo waliambia BBC, msichana huyo mwenye umri wa miaka 13 alikuwa amearifiwa kuhusiana na kifo cha mtoto wake na kwa hivi sasa ameonekana kupata afueni.
Mwanahabari wa BBC, Geeta Pandey huko Delhi amesema hiyo ni kesi ya tatu kwa miezi michache iliyopita inayohusiana na ubakaji miongoni mwa watoto wa India ambao walipata uja uzito na kufika mbele ya mahakama kupata ruhusa ya kutoa mimba .
Mwezi uliopita mtoto wa miaka 10 aliyekuwa ambebakwa alijifungua mtoto msichana kaskazini mwa mji wa Chandigarh. Alikuwa na uja uzito wa wiki 32 lakini alinyimwa ruhusa ya kutoa mimba hiyo baada ya kundi la madaktari kusema utoaji wa mimba utakuwa na ''harati kubwa sana.''
Mwezi Mei, kesi sawia na hiyo iliripotiwa kutoka jimbo lililoko kaskazini mwa Haryana ambapo msichana wa miaka 10, anadaiwa kubakwa na babake wa kambo, aliruhusiwa kutoa mimba hiyo na alikuwa na uza uzito wa wiki 20, daktari alisema.
Hatuwezi kutaja majina ya wasichana hao kwa sababu za kisheria.
Kesi hizi zilianza kuangaziwa kuchelewa , kwa sababu watoto wenyewe hawakutambua hali zao wenyewe na wazazi pia hawakutambua dalili za kawaida za mimba kwani hawakuamini kwamba watoto wao wangeweza kupata mimba katika umri mdogo, mwandishi wa BBC mjini Delhi amesema.

No comments:

Post a Comment