"Mifumo ya afya nchini Nambia inajitegemea," alisema rais wa Marekani Donald Trump wakati wa kikao na viongozi wa Afrika mjini New York, siku ya Jumatano.
Lakini cha kushangaza ni kuwa hakuna nchi yenye jina "Nambia"
Huenda Rais Trump alikuwa akimaanisha Namibia? Zambia au Gambia?
Watumiaji wa mitandao ya kijamii hawakuchelewa kutoa maoni.
Mtu mmoja alisambaza picha ya mwaharakati wa ubaguzi raia wa Marekani Rachel Dolezal, ambaye anajitambua kuwa mtu mweusi licha ya yeye kuzaliwa akiwa mzungu na ambaye alizuru Afrika Kusini hivi majuzi.
No comments:
Post a Comment