Thursday, September 21

36 washikiliwa vurugu za Jangwani



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni 
Dar es salaam. Watu 36 wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kuhusika kufanya vurugu eneo la bonde la Jangwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema leo Alhamisi kuwa bomoabomoa inaendelea eneo hilo na ulinzi umeimarishwa.
"Tumewakamata watu 36, bado tunaendelea kuwasaka waliofanya fujo akiwemo kiongozi wa mtaa wa Jangwani anayetuhumiwa kuhamasisha vurugu hizo," amesema.
Kamanda Hamduni amesema kiongozi huyo (jina tunalihifadhi kwa sasa) jana Jumatano aliwahamasisha wananchi kuwapiga mawe maofisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala waliokuwa wakisimamia bomoabomoa kupisha mradi utakaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa).
Amemtaka kiongozi huyo kujisalimisha polisi.

No comments:

Post a Comment