Rais Donald Trump wa Marekani amezilaumu tena pande zote kwa ghasia zilizotekea katika maandamano ya Charlottesville, siku ya jumamosi ambapo mwanaharakati anayepinga ubaguzi wa kijamii aliuawa.
Katika mkutano na waandishi wa habari , Rais Trump amesema waandamanaji wa mrengo wa kushoto waliwashambulia kwa makusudi wale waliokuwa wakipinga kuondolewa kwa sanamu.
Kauli hiyo imelaaniwa vikali zaidi na maafisa wa ngazi ya juu wa chama cha Republican.
Watu wengine kadhaa pia walijeruhiwa katika katika tukio hilo
Rais wa Marekani alitoa tamko hilo pia siku ya Jumatatu akiyalaumu makundi yenye kujenga chuki likiwemo la Ku Klux Klan na lile la neo-Nazis.
No comments:
Post a Comment