Tuesday, August 22

Misa Tanzania wapata Kaimu Mkurugenzi


Katika hatua za kuboresha utendaji wa Taasisi ya Misa Tanzania , Bodi imemteua  Gasirigwa Sengiyumva kuwa Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Mpito Baraza la Uongozi Salome Kitomari inasema kwamba uteuzi huo umefanyika Agosti nane .

Gasirigwa anachukua nafasi ya  Andrew Marawiti ambaye ataendelea na
majukumu yake kama Ofisa wa Fedha na Utawala.
Katika taarifa hiyo Kitomari anasema  ‘’Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa katika kikao kilichokaa Ijumaa ya  tarehe 12 Mwezi huu na kuendelezwa tarehe 18. Bodi ya Mpito ya Taasisi yetu imefanya mabadiliko ya kiutawala katika Sekretarieti yetu’’
Gasirigwa ni msomi wa shahada ya Mawasiliano ya Umma na ana uzoefu wa miaka 12 kazini.
Kabla ya uteuzi, alikuwa ni Ofisa Habari na Utafiti kwa takriban miaka
sita sasa.

No comments:

Post a Comment