Wednesday, July 12

Kumbe mashabiki walijipanga kwa selfie na Rooney


Baadhi ya mashabiki waliofika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walikuwa wakiwaza kupiga picha za selfie na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney.

Mashabiki waliofika JNIA walikuwa wakiuliza kama Rooney yumo kwenye msafara na waliposikia atakuwepo wakaanza kujipanga kwa ajili ya picha.
“Mimi nataka Rooney akitoka nimuombe nipige naye picha yaani hiki ndicho kilichonileta hapa,” alisema shabiki moja akiwa na simu yake ya smart.
Shabiki mwingine alilazimika kumfuata mwandishi wa habari wa Mwananchi na kumuuliza kama kuna uwezekano wa kupiga picha na wachezaji wa Everton, lakini hakukuwa na nafasi hiyo.
Baada ya wachezaji kuwasili, hata waandishi wa habari hawakuwa na nafasi ya kuzungumza na wachezaji zaidi ya kuwekewa mpaka wa kufanya kazi na zaidi ilikuwa kwa wapigapicha waliokuwa wakiwavuta kwa lenzi kwani hawakupewa hata nafasi ya kuwasogelea.
Wakati basi lililokuwa na wachezaji lilipokuwa linatoka, simu zaidi ya 100 zilikuwa juu kurekodi ujio wa wachezaji hao wakitoka uwanjani. Mashabiki lukuki walikuwa nje la lango japo kushuhudia tu ujio huo.

No comments:

Post a Comment