Monday, December 4

Mahakama haijaarifiwa kuapishwa Odinga


Nairobi, Kenya. Mahakama imesema haijapata mawasiliano rasmi kutoka kwa Muungano wa Nasa kuhusu hatua ya kumuapisha kiongozi wake Raila Odinga.
Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi amesema Mahakama haina taarifa kuhusu sherehe iliyopangwa kufanyika Desemba 12,2017.
“Hatujaarifiwa chochote kuhusu hafla ya kumuapisha Raila Odinga inayopangwa na muungano wa upinzani,” amesema.
Muungano wa Nasa umeanza matayarisho ya hafla ya kumuapisha kiongozi huyo kwa kuunda kamati ya kusimamia shughuli hiyo.
Kuteuliwa kwa kamati hiyo ya watu saba kumefanyika siku chache baada ya Odinga kutangaza Jumanne iliyopita kuwa ataapishwa kupitia mabunge ya kaunti, hatua ambayo Serikali imesema ni kinyume cha sheria.
Gazeti moja la Kenya limesema muungano huo umetuma kadi za mwaliko wa hafla hiyo iliyopangiwa kufanyika Desemba 12,2017 Taifa hilo litakaposherehekea siku ya uhuru.
Kadi za kidigitali za mwaliko zenye jina la Odinga hazionyeshi mahali hafla hiyo itafanyika.
“Umekaribishwa. Njoo ushuhudie rais wa wananchi Raila Amollo Odinga akiapishwa tarehe 12 Desemba saa sita mchana. Taarifa kuhusu itakapoandaliwa hafla hii itatolewa baadaye,” ndivyo inavyosomeka kadi hiyo ambayo inasisitiza kuwa inaruhusu mtu mmoja pekee kwa kila kadi.
Kamati hiyo ambayo itakuwa ya kitaifa ya kuendesha mabunge ya wananchi, itaongozwa na msomi wa uchumi maarufu, David Ndii.

Namna idadi ya wanaosusa ving’amuzi ilivyoongezeka kwa kasi nchini


Asilimia 29.4 ya waliokuwa wamenunua ving’amuzi mwaka jana walikuwa
hawavitumii ikilinganishwa na asilimia sifuri mwaka 2014
Takribani theluthi moja ya watumiaji wa ving’amuzi nchini hawavitumii
tena vifaa hivyo kutazama luninga, kiwango ambacho ni kikubwa kuwahi kurekodiwa ndani ya miaka mitano iliyo-pita. Wachambuzi wa masuala ya habari na mawasiliano wanaeleza kuwa mwenendo huo uliopaa kwa kasi ndani ya miaka mita-tu iliyopita unahatarisha upatikanaji wa taarifa kwa wananchi kupitia luninga. Uchambuzi wa takwimu za robo ya pili
ya mwaka 2017 za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa idadi ya ving’amuzi
vinavyonunuliwa inaongezeka kila mwaka, lakini ukuaji huo unaathiriwa na kasi ya kupaa kwa ving’amuzi visivyotumika kwa muda mrefu. Takwimu hizo zinabainisha kuwa hadi kufikia Desemba mwaka 2016 Tanzania ili-kuwa na ving’amuzi milioni 1.7 hata hivyo watumiaji 500,000 walikuwa hawavitumii
kwa wakati huo sawa na asilimia 29.4 ya ving’amuzi vyote vilivyokuwa vimenu-nuliwa. Idadi ya watu wenye ving’amuzi lakini hawavitumii ilianza kupanda miaka miwili iliyopita kutoka asilimia sifuri mwaka 2014 hadi asilimia 29.4 mwaka jana huku baadhi ya wananchi wakieleza kuwa ukata umesababisha kutotumia vifaa hivyo vya dijitali. Ikumbukwe kuwa mwaka 2014
ving’amuzi vyote vilivyokuwepo nchini vilikuwa vinafanya kazi.
Baadhi ya wananchi walimweleza mwandishi wetu kuwa licha ya ukata baa-dhi ya kampuni za huduma za ving’amuzizinabadilibadili mifumo ya kulipia kila
mwisho wa mwezi kiasi cha kuleta ugumu kufanikisha malipo kwa wakati.
Pia uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa baadhi ya watu walikuwa wamenunua zaidi ya king’amuzi kimoja kutimiza mahitaji yao ya luninga, lakini kutokana na ukata wamelazimika kubakiza kimoja huku nacho wakilipia kwa msimu.
Mkazi wa Tabata, Athumani Bendera anasema malipo ya kila mwezi yanamtesa kutokana na ugumu wa upatikanaji wa fedha kwa sasa ndiyo maana hatumii ving’amuzi mara kwa mara.
“Nina ving’amuzi vya Azam na StarTimes lakini hali ni ile ile kwani bila kufanya malipo ya mwezi sahau kupata chaneli za ndani ambazo nyingi hutuhabarisha habari za kitaifa na taarifa mbalimbali, sasa kwanini iwe hivi?” alihoji Bendera.
Ukosefu wa fedha za kulipia ving’amuzi kwa baadhi umefanya wategemee huduma za luninga kwenye vibanda ama sehemu za huduma kama baa na kwenye migahawa.
Zaharia Mohamed alisema kipindi anachoshindwa kulipia ankara ya king’amuzi hupata habari kupitia vijiwe tena zile ambazo zimekuwa gumzo mbali na hapo hushindwa kupata taarifa rasmi.
“Malipo ya mwezi si chini ya Sh10, 000 kwa kingamuzi kimoja na pia unaweza kulipia kifurushi cha wiki mbili kwa Sh6,000 jambo ambalo huwezi kukidhi mahitaji hivyo hushindwa kupata taarifa hasa ukilinganisha na hali ya maisha kwa sasa,”anasema Zaharia.
Wakala wa ving’amuzi na muuzaji wa vifaa vya luninga, Dotto Ally anasema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wateja hasa wa ving’amuzi vya StarTimes wakidai antena ndio kikwazo kikubwa.
“Wateja walio wengi wanalalamikia antena kuwa na gharama kubwa licha ya king’amuzi chenyewe hali inayowafanya kutumia njia mbadala na kukosa ubora wa picha wakati wa kuangalia taarifa kupitia luninga,” anasema Ally.
Mbali na kuuza ving’amuzi kulingana na msimu, Ally anabainisha kwa sasa bei za ving’amuzi na gharama za mwezi zimeshuka tofauti na zamani huku mfumo wa malipo kwa channeli za ndani ikiwa ni kilio kikubwa.
“Bei ya kifurushi cha Dstv Compact zamani ilikuwa Sh219,000 kwa sasa imeshuka hadi Sh 120,000. Mbali na kushuka kwa bei za ving’amuzi bado wateja wengi wanashindwa malipo kwa mwezi na kusababisha wasivitumie,” anasema Ally.
Omari Ahmed, fundi wa antena na madishi anayefanya kazi katika ofisi za StarTimes Buguruni anasema wateja wengi hawafuati ushauri wa kiufundi ndiyo maana hujikuta wakinunua ving’amuzi vingi ambavyo bado baadhi hupata picha dhaifu.
“Wengi wana zaidi ya king’amuzi kimoja na ukiuliza wanasema walinunua ili kupata picha bora na chaneli nyingi zaidi lakini matokeo yake hawajapata,” anasema.
Kauli za wachumi
Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema uchumi pekee hauwezi kuwa sababu ya kuongezeka idadi ya watu wanaoshindwa kutumia ving’amuzi.
Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Humphrey Moshi anasema hali ya uchumi kwa sasa haisababishi watu kushindwa kununua ving’amuzi kwani wanaendana na mabadiliko ya teknolojia.
Profesa Moshi anasema simu za kisasa zimechukua nafasi kubwa kuliko hata matumizi ya luninga kwa sasa hasa ikizingatiwa bei za simu za inteneti imekuwa rahisi kuliko zamani.
“Mabadiliko ya teknolojia kwa simu ambazo zinakupa kila kitu zimechagiza kushuka na kupoteza umaarufu wa ving’amuzi. Siku hizi kila kitu unapata katika simu kitu ambacho starehe zote unapata humo hivyo wahusika wanatakiwa kuwa wabunifu katika hili ili kuwa washindani,”anasema Profesa Moshi.
Hata hivyo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT), Pili Mtambalike anasema mfumo wa ulipiaji wa kila mwezi ndio chanzo kikubwa kwa wananchi kukosa taarifa hivyo kuna haja kwa mamlaka husika kukaa upya kuchunguza tatizo.
Mtambalike anasema uchumi wa nchi haumpatii tu wa kawaida fursa ya kupata habari kwani wanaishi chini ya Dola moja za Marekani ni ngumu mtu kulipia king’amuzi kwa ajili ya kupata taarifa.
“Watu hawawezi kuhangaikia kutafuta fedha za chakula halafu bado wanalipia kupata taarifa iwapo muda wa malipo umefikia kikomo ni suala la kukaa kwa wataalamu wa mamlaka husika ili kujadili mfumo mpya ambao tumekubali kuingia kwa miaka ya nyuma,” anasema Mtambalike.
Anasema kulingana na takwimu hizo ni wazi kuwa watu wengi hawapati taarifa kwani hata yeye anamiliki ving’amuzi vitatu ambavyo kwa mahitaji mbalimbali ilimlazimu kuvinunua.
Ofisa habari wa Kampuni ya StarTimes Media, Juma Suluhu anasema kampuni yao imetoa aina mbili ya ving’amuzi wateja wao ambavyo wanaweza kuangalia chaneli zote bila ya malipo.
Anasema baada ya kulipia malipo ya awali king’amuzi kingine wanalipia fedha kidogo kwa ajili ya matengenezo.
“Tuna ving’amuzi viwili kimoja ni bure kabisa, kingine unalipia kidogo ili kuweza kupata channeli nyingi zaidi,”anasema Suluhu.
Suluhu anasema katika kipindi cha kuhamia katika mfumo wa kidigitali walitengeneza ving’amuzi kwa bei ya chini ambavyo viligharimu dola 50 hadi 55 za Marekani mbali na bei halisi ya Dola za Marekani 60 kwa seti moja ya kingamuzi.
“Bei hizo zinajumuisha na kufungiwa king’amuzi na vifaa vyote ikiwemo rimoti, huku mtumiaji akipata chaneli 30 zikiwemo za nje na kulipia gharama ya mwezi kwa matengenezo ya dola 3 za kimarekani,” anasema.
Anasema katika mpango wa upya, zaidi ya vijiji 10,000 vitapata televisheni za dijitali ikiwa ni muendelezo kwa watu kuweza kupata taarifa kwa njia ya kidigitali na tayari vijiji 800 Tanzania wamepatiwa televisheni hizo.
TCRA hawakuweza kujibu maswali yetu kwa wakati kuelezea kiundani hali hiyo licha ya kuwatumia maswali zaidi ya mwezi mmoja na kufuatilia mara kwa mara kwa simu na kutembelea ofisini kwao.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani kabla ya kujiuzulu aliliambia Mwananchi kuwa TCRA ilitoa leseni kwa kampuni tatu (multiplex operators) zilizotakiwa kurusha matangazo ya idhaa tano za kitaifa bila ya malipo ya mwezi.
Ngonyani alisema leseni zilizotolewa kwa ajili kurusha matangazo zilihususha kampuni zinazouza ving’amuzi vya Digitek, Ting, Continental na Startimes.
“Wanaotumia satellite kurusha matangazo kama Azam, Dstv, na Zuku wao kwa kila mwisho wa mwezi ni lazima ulipie ili kupata chaneli zote zikiwemo za ndani,”alisema Ngonyani.
Alisema kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu watu milioni 1.5 wametumia ving’amuzi vyao kupata taarifa hawa ni wale ambao wanatumia Ting, Startimes, Continental na Digitek.
Ngonyani alibainisha kuwa takwimu hizo ni sehemu ya watu 2.65 milioni wa Tanzania Bara ambao wanatumia ving’amuzi mbalimbali kujipatia taarifa huku akiwataka wananchi kutambua aina mbili za ving’amuzi ambavyo wanatumia.
“Mimi ni mmoja wa watu 1.5 milioni wanaotumia ving’amuzi vinavyotakiwa kutoa chaneli tano za ndani bure na tangu nimenunua sijapata tatizo hilo la chaneli za ndani kutokuonekana,” anasema.

TBA yasema nyufa majengo ya hosteli walizitarajia


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga amesema nyufa kwenye jengo moja la Block A katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) hazina madhara na walizitarajia.
Amesema nyufa katika jengo hilo la hosteli ambalo ni kati ya sita yaliyopo Block A zimetokea eneo walilotarajia ambalo kitaalamu linajulikana (expansion joint) hivyo hazina madhara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 4,2017 Mwakalinga amesema kwa kawaida udongo unaobeba jengo hutitia baada ya muda fulani, hivyo wakati wa ujenzi huacha nafasi kuliwezesha jengo kupumua bila kusababisha nyufa.
Mwakalinga amesema kuna makosa yalifanyika ya kuziba nafasi zilizoachwa (expansion joint) kwa kutumia saruji badala ya mbao au plastiki maalumu hivyo kuonyesha nyufa kwenye jengo hilo.
Amesema nyufa zimetokea sehemu mwafaka ambazo walitarajia na kwamba kila jengo lina expansion joint tatu kwa ajili ya usalama wa jengo.
Mwakalinga amesema majengo hayo ya hosteli za wanafunzi bado yako chini ya uangalizi wa TBA, kwa hiyo wataanza ukarabati na hakuna haja ya kuhamisha wanafunzi kwa sababu jengo liko imara.
Amesema kwa taaluma ya ujenzi wa majengo, dosari hiyo ni ya kawaida kutokea na kwamba, wakala umeanza kuchukua hatua kuzisahihisha kwa kuhakikisha uwazi uliopo unakuwa huru bila kujazwa kitu kigumu.
Mwakalinga amesema ujenzi umegharimu Sh10 bilioni walizopewa na Serikali na kwamba fedha hizo zilitosha kwa sababu walizingatia hadidu za rejea walizopewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya ujenzi.
Amesema wamejenga vyumba 960 vyenye uwezo wa kubeba wanafunzi 3,840 na kwamba, gharama ya vyumba hivyo ni sawa na Sh10.4 milioni kwa kila kimoja.

Mwakalinga amesema Sh10.8 bilioni zimetumika kujenga shule ya Ihungo mkoani Kagera iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi ambayo itakuwa na nyumba 30 za walimu.
"Walijitokeza watu kujenga kwa Sh60 bilioni lakini sisi tumejenga kwa Sh10 bilioni tu. Kwa hiyo, inawezekana na sisi ndiyo tuliojenga, msiwasikilize wengine ambao hawana ujuzi wowote katika ujenzi," amesema.
Akizungumzia muda wa ujenzi, amesema hosteli hizo zilijengwa kwa miezi minane ambayo kitaalamu inatosha kwa ujenzi imara.
Amesema msingi wa mabweni hayo una uwezo wa kubeba ghorofa nyingine mbili zaidi na utaalamu ulizingatiwa katika ujenzi.

Serikali yashauriwa kuboresha sheria ya uvuvi


Mtwara. Serikali imeshauriwa kuboresha sheria ya uvuvi ili kuwabana wote wanaojishughulisha na uvuvi haramu wa kutumia milipuko.
Imeelezwa kutokana na sheria kutotoa adhabu kali kwa watuhumiwa wanapofikishwa mahakamani hulipa faini na kuendelea na shughuli zao, hivyo kupunguza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya Taifa.
Hayo yameelezwa leo Jumatatu Desemba 4,2017 mkoani Mtwara wakati wa kikao cha utambulisho wa mradi wa kukabiliana na uvuvi wa milipuko ulioandaliwa na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira na Maendeleo ya Jamii (WWF).
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kwa kushirikiana na wadau wamedhibiti uvuvi haramu wa kutumia milipuko lakini baadhi ya watu wachache wamekuwa wakiendelea na hata wanapofikishwa mahakamani wanaishia kulipa faini.
Mmanda amesema uvuvi haramu umeleta matatizo mengi ambayo hayakuwepo, ikiwa ni pamoja na kuharibu mazingira ya bahari, soko la samaki nje ya nchi na umasikini kwa jamii.
"Kuna watu wanajishughulisha na uvuvi haramu, mwingine hata akifikishwa mahakamani anakuja tayari ana faini mfukoni analipa anarudi kuendelea na uvuvi ili arudishe fedha aliyolipia faini," amesema Mmanda.
Mtendaji wa mradi wa WWF, Thomas Chale amesema uvuvi wa kutumia milipuko umepungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
Amesema huo mkoani Mtwara kwa sasa uvuvi wa kutumia milipuko unafanyika mara moja kwa wiki na wakati mwingine haufanyiki kabisa lakini kwa maeneo ya Kigamboni na Masaki jijini Dar es Salaam bado unafanyika.
"Maeneo ya Kilwa kwa siku walikuwa wanasikia milipuko 20 lakini sasa unaweza usisikie kabisa au mmoja kwa wiki,” amesema.
Mkutano huo umewashirikisha wadau kutoka Kilwa, Lindi na Mtwara.

Wanafunzi UDSM wazungumzia nyufa majengo mapya ya hosteli

Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameingia hofu baada ya mabweni wanayoishi kuwa na nyufa.
Mabweni hayo yanayotumiwa na wavulana katika jengo la Block A yana nyufa sehemu mbalimbali kuanzia chini hadi ghorofa ya tatu.
Akizungumza na MCL Digital mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso), Simon Masenga amesema nyufa hizo zilianza kuonekana wiki mbili zilizopita.
Amesema walitoa taarifa kwa meneja wa hosteli lakini majibu waliyopewa ni kuwa majengo hayo yako chini ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Mbunge mwingine wa serikali ya wanafunzi, Kumbusho Dawson amesema leo Jumatatu Desemba 4,2017 kuwa majengo hayo yana upungufu, ukiwemo wa maji kutuama kwenye bafu na kutokuwa na makabati.
"Tumelalamika kwa meneja wa mabweni kuhusu upungufu katika majengo haya na majibu tunayopewa ni kuwa bado yako chini ya TBA," amesema Dawson.
Majengo hayo yaliyojengwa na TBA kwa miezi minane yakielezwa kugharimu Sh10 bilioni yalizinduliwa Aprili 15,2017.
Ujenzi ulifanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kumaliza tatizo la malazi kwa wanafunzi wa UDSM.
Picha zinazoonyesha nyufa kwenye majengo hayo zilianza kusambaa mitandaoni jana Jumapili Desemba 3,2017.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga akizungumza na MCL Digital jana Jumapili alisema naye aliziona picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.
“Nimeziona na muda huu najiandaa kwenda huko kuangalia kama taarifa hizo ni za kweli,” alisema Mwakalinga alipozungumza na MCL Digital saa mbili usiku na kuahidi kutoa taarifa baada ya kukagua majengo hayo.
Kwa mujibu wa wanafunzi waliozungumza na MCL Digital, maofisa wa TBA walifika kwenye hosteli hizo maarufu kwa jina la Hosteli za Magufuli jana usiku na kufanya ukaguzi.
Baadhi yao inaelezwa walilala katika eneo hilo kwa ajili ya uchunguzi na hata walipofuatwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi hawakuwa tayari kuzungumza lolote.

Wakuu wa polisi wajadili ushirikiano


Dar es Salaam. Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Rwanda, Emanuel Casana kutathmini makubaliano yaliyofikiwa  mwaka 2012 kuhusu ushirikiano na kufanya operesheni za pamoja.
Akizungumza leo Jumatatu Desemba 4,2017 IGP Sirro amesema walisaini makubaliano ya kufanya operesheni kwa pamoja kukomesha uhalifu na kubadilishana wataalamu.
Amesema kuna wataalamu kutoka Rwanda watatoa mafunzo ya kushughulikia makosa ya kimtandao.
“Wenzetu wa Rwanda ni wazuri kwenye masuala ya kudhibiti uhalifu wa kimtandao, hivyo watatoa mafunzo kwa wataalamu wetu,” amesema IGP Sirro.
Amesema wamepata mafanikio kwa kushirikiana na Rwanda kwa kukamata dawa za kulevya zikiwemo bangi mkoani Kagera na wameimarisha usalama katika ukanda wa kati.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Rwanda, Casana amesema tangu wameingia mkataba huo wamekuwa wakibadilishana wataalamu kwa ajili ya kupeana mafunzo.

Lissu aomba aombewe apone

Dar es Salaam. Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ametumia maadhimisho ya wiki ya msaada wa sheria kuwaomba wananchi kumwombea apone na kurudi nchini aendelee kutoa mchango wake katika taaluma ya sheria.
Lissu tangu Septemba 7 amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa katika makazi yake Area D mjini Dodoma.
Akizungumza leo Jumatatu Desemba 4,2017 katika ufunguzi wa wiki ya msaada wa sheria, mwakilishi wa TLS, John Seka amesema Lissu anawasalimia wananchi.
“Rais wa TLS, Tundu Lissu anawasalimia sana, anaendelea kupata nafuu ila anawaomba Watanzania waendelee kumwombea ili apone haraka,” amesema Seka.
Amesema Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) ana hamu ya kurudi nyumbani aendelee kutoa mchango wake wa kisheria kwa wananchi.
Kuanzia leo hadi Desemba 8,2017 wananchi wanapata fursa ya kupata msaada wa kisheria katika migogoro inayowakabili.
Seka ametoa wito kwa wananchi kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na mikoani kupata huduma ya msaada wa kisheria.
Amesema baada ya wiki hiyo kumalizika, wananchi watatakiwa kufika ofisi za TLS kupata msaada wa kisheria kwa kuwa hilo ni moja ya majukumu ya chama hicho.

Marekani yaonywa juu ya mpango wa kuhamishia ubalozi wake Jerusalem

 Jumuiya ya nchi za kiarabu, Palestina  na Jordan zimeionya Marekani dhidi ya uamuzi wake wa kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem. 

Israel | Palästina Jerusalem - Felsendom (picture alliance/dpa/R.Holschneider)
Jumuiya hiyo ya nchi za kiarabu imesema hatua hiyo inaweza ikakwamisha mazungumzo yoyote ya siku zijazo na pia inaweza ikasababisha kuibuka tena vurugu katika kanda ya Mashariki ya Kati. 
Onyo hilo linakuja mnamo wakati rais wa Marekani Donald Trump akifikiria kufanya uamuzi wa kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka mjini Tel Aviv hadi Jerusalem, hatua ambayo itakuwa inaashiria kuutambua rasmi mji huo wa kale kama mji mkuu wa Israel. Mji huo unagombaniwa kati ya Israel na Palestina.  Uamzi huo wa Marekani kuhusiana na hatua hiyo unaweza ukatolewa leo Jumatatu.
Naabil Shaath ambaye ni mshauri mwandamizi wa rais wa Mamlaka ya ndani ya Palestina  Mahmoud Abbas alinukuliwa akisema hapo jana kuwa " Tumeionya Marekani kuwa kama serikali ya nchi hiyo itathubutu kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel  na kuhamishia ubalozi wa Marekani katika mji huo basi hii itakua ni hatua itakayofikisha mwisho fursa ya mazungumzo ya amani"
Kwa upande mwingine, katibu mkuu wa jumuiya ya nchi za kiarabu  Ahmed Aboul Gheit amesisitiza juu ya onyo hilo na kusema hatua hiyo ya Marekani haitasaidia kuleta amani au uthabiti bali itachochea vurugu na pia kunufaisha upande mmoja ambao ni serikali ya Israel.
Waziri wa mambo ya nje wa Jordan Ayman Safadi ambaye amesema ameibua swala hilo katika mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson.
Safadi  aliandika katika ukurasa wa twitter kuwa uamuzi kama huo utaibua hasira miongoni mwa jamii ya waislamu katika mataifa ya kiarabu, kuchochea mivutano na kuvuruga juhudi za amani. 

Trump bado kutoa uamuzi
USA Präsident Donald Trump (Reuters/J. L. Duggan)
Rais wa Marekani Donald Trump
Hapo jana Jumapili  mshauri wa rais Donald Trump kuhusu Mashariki ya Kati  Jared Kushner ambaye amepewa jukumu  la kuongoza juhudi za Marekani katika mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina amesema rais Trump bado  hajafanya uamuzi kuhusiana na hatua hiyo.
Rais Trump anaripotiwa kufikiria kutoa uamuzi kuhusiana na suala hilo  mapema iwezekanavyo kabla ya Jumatano wiki hii.
Marekani kwa muda mrefu imekua ikisema kuwa suala linalohusiana na hadhi ya mji wa Jerusalem ambao pande zote za Israel na Palestina  zinadai kuwa ni mji mkuu wake ni lazima liamuliwe kama sehemu ya mchakato wa amani.
Kwa mujibu wa shirika la habari la mamlaka ya ndani ya Palestina Wafa , rais Mahmoud Abbas  amewaonya viongozi wa Jumuiya ya kimataifa kuwa uamuzi huo utapelekea ukanda huo kuingia katika machafuko ambayo suluhu yake itakua vigumu kupatikana.
Israel imekua ikiichukulia Jerusalem kua ni mji wake mkuu na kwa muda mrefu imekua ikiitaka Marekani kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv na kuupeleka katika mji huo huku serikali ya Mamlaka ya Palestina nayo pia ikisema Jerusalem Mashariki utakua mji mkuu wa taifa la baadaye la Palestina.

Yemen:Hofu yatanda kutokana na mashambulizi ya anga

Ni wazi kwamba ushirikiano hamna tena kati ya kundi la waasi wa Houthi na vikosi vinavyomtii Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdallah Saleh na hali hiyo inaashiria mabadiliko katika mgogoro wa Yemen.

Jemen Sanaa Kämpfe (Reuters/M. al-Sayaghi)
Usiku wa kuamkia leo wakaazi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa walijawa na hofu kutokana na mashambulizi ya anga yaliyoendelea usiku kucha katika mapigano kati ya waasi na wafuasi wa rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.
Hata hivyo msemaji wa muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia jenerali Ahmed Assiri hajatoa tamko rasmi kuhusiana na mashambulio hayo. Chanzo kimoja kutoka uwanja wa ndege wa Sanaa kimefahamisha kuwa mashambulizi hayo yalilenga hususan maeneo ya waasi na kwamba uwanja huo wa ndege uko salama.Hadi sasa watu watu wapatao 60 wamuwawa katika mapigano hayo.
Rais wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi (Getty Images/AFP/E. Hamid)
Mbele: Rais wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi
Yemen imegawanyika kwa kati ya majeshi na serikali ya rais Abedrabbo Mansour Hadi katika eneo la kusini. Mansour Hadi anaungwa mkono na Saudi Arabia na anatambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa, na kwa upande wa kaskazini kuna waasi wa Houthi na vikosi vinavyomuunga mkono rais wa zamani Ali Abdallah Saleh mwenye ushawishi mkubwa.
Kutokea mwaka 2014 mji mkuu Sanaa umekuwa unatawaliwa kwa makubaliano baina ya rais huyo wa zamani Saleh na waasi wa Houthi walioifurusha serikali ya Mansour Hadi na kisha kuanzisha serikali yao na kwa kipindi cha miaka miwili kwa pamoja na vikosi vya Ali Abdallah Saleh wamekuwa wanapambana na muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia.
Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh (picture-alliance/AP Photo/H. Mohammed)
Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh
Lakini baada ya rais huyo wa zamani kutangaza kwamba sasa yuko tayari kufungua ukurasa mpya akiwa na maana kuwa anataka kufanya mazungumzo na utawala wa Saudi Arabia. Hatua hiyo ya Saleh ndiyo imesababisha mgawanyiko huo na kuongeza chuki kati yake na waasi wa Houthi.  Mgogoro huo umesababisha hofu ya kuzuka mapinago mapya katika nchi hiyo inayokabiliwa na machafuko. Watu wapatao 8,750 wameuwawa tangu majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia yalipoanza operesheni yake nchini Yemen.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Reuters/L. Jackson)
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres
Mgogoro huo umezidi kuitumbukiza Yemen katika hali mbaya ya ukosefu wea chakula na mahitaji ya msingi kwa binadamu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezihimiza pande zote kuacha mapigano ili kutoa njia ya kuifikisha misaada.


MBUNGE WA CUF KUJIUZULU

SIKU moja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF) kutangaza kujiuzulu ubunge na nafasi zote za uongozi ndani ya chama hicho, sababu za uamuzi wake zimebainika.
Taarifa kutoka ndani ya CUF kupitia watu wake wa karibu zilidai  mbunge huyo amekuwa akikabiliwa na madeni mengi kiasi cha kuwa kwenye hatari ya kufilisiwa baadhi ya mali zake.
Chanzo cha kuaminika kiliambia MTANZANIA kuwa licha ya hali hiyo, kwa mwezi mmoja, hakumshirikisha   kiongozi yeyote kwenye matatizo yake.
Gazeti hili lilimtafuta Mtulia na kuzungumza naye lakini akasema  wote wanaomzushia mitaani kwa uamuzi wake, wanasumbuliwa na povu.
Alisema ameamua mwenyewe kwa hiari yake na si suala linalohusu madeni yake ila amevutiwa  na uchapakazi wa Rais Dk. John Magufuli.
Alipoulizwa kama atawania tena jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, alisema   anasubiri kupangiwa na wakubwa wake lakini kwa sasa hawezi kujipangia.
Na hata alipoulizwa ni kwa nini kila kiongozi au mwanachama akitoka upinzani anasema ni kwa sababu anamuunga mkono Rais Dk. Magufuli, alisema ni lazima iwe hivyo.
Alisema  kwa sababu  ndiye kiongozi wa nchi na chama tawala ambaye pia ni mtekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa Watanzania.
“Hivi unafikiri inakua kwa ajili ya nani?  Ni Magufuli kutokana na utendaji wake na ndiyo msimamizi mtekelezaji wa shughuli zote ndani ya chama changu nilichokiona kinafaa.
“Hakuna mwingine ni yeye na huwezi kukwepa kumpa sifa hizo,” alisema Mtulia.
CUF MAALIM WAMBARIKI
Chama cha Wananchi (CUF), upande unaounga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kimesema kimeridhia kujiuzulu kwa Mtulia huku kikimtakia safari njema katika siasa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  jana na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa CUF, Mbarala Maharagande, chama hicho kilitarajia hayo mapema na wala hakikushtushwa kutokana na taarifa za intelijensia kilizopata.
“Tuliyatarajia hayo mapema na wala hatukustushwa na uamuzi wake kutokana na taarifa za intelijensia za ukaribu wake na viongozi wa CCM akishirikiana na Profesa Ibrahim Lipumba.
“Tuna uhakika kuwa wafuasi wengi wa Lipumba watafuata mkondo huo na yeye amefungua njia,”alisema.
Maharagande alisema   uamuzi aliochukua Mtulia ni haki yake kwa mujibu wa katiba ya CUF ibara ya 117(1) na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 11 Ibara ya 149(1), (d).
Hata hivyo, alisema CUF hakikubaliani na sababu za kujiuzulu kwake kwa sababu upo mwenendo usiofaa wa kuua mfumo wa demokrasia nchini, ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
“Kila mtanzania mwenye akili na fahamu timamu kwa kiwango kidogo tu bila ya kujali itikadi ya vyama, anashuhudia ukweli huu wa ugumu wa hali ya maisha.
“Tunatoa pole kwa wanachama na wananchi wa Kinondoni ambao walipambana kwa hali na mali kuhakikisha   mabadiliko ya  siasa nchini yanapatikana kwa kusimamia ushindi wa CUF na Mtulia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,” alisema.
Aliwahakikishia Watanzania kuwa CUF kitaendelea kusimamia imara kupinga vitendo vya ovyo na kinaamini   ukombozi haujawahi kupiganiwa na watu wenye fikra dhaifu na maono duni.
“Mwisho tunamtakia Mtulia safari njema ya siasa huko alikokwenda.
“Ni haki na uhuru wake ambao unapaswa kuheshimiwa na kila mmoja wetu.
“Tunapingana naye kwa nguvu zote kwa sababu alizozieleza katika kufikia uamuzi alioufanya,”alisema Maharagande.
CUF LIPUMBA KUZUNGUMZA LEO
Kwa upande wa CUF inayoongozwa na Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, umesema utatoa tamko lake leo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma, Abdul Kambaya allisema wamepanga kutoa tamko leo.
“Sisi tumepanga kutoa tamko leo kwa waandishi wote na si mmoja mmoja hivyo ngoja hadi hapo kesho (leo) nitakapozungumza na waandishi wa habari,’’ alisema Kambaya.
BUNGE HALIJAPATA TAARIFA
Akizungumza na MTANZANIA kwa   simu, Katibu wa Bunge, Dk. Steven Kagaigai alisema  ofisi ya Bunge haijapokea taarifa rasmi.
“Bado hatujapata taarifa rasmi, tunazisikia hizo za kwenye mitandao tu,” alisema Dk. Kagaigai.
CHADEMA YANENA
Chadema ambacho kiliungana na CUF katika Uchaguzi Mkuu uliopita na kuwa sehemu ya ushindi wa Mtulia, kimesema mbunge huyo alikuwa timu ya Profesa Lipumba hivyo hana madhara yoyote kwa Ukawa.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, aliliambia MTANZANIA kuwa Mtulia baada ya kushinda ubunge aliusaliti Ukawa ambao ulimwezesha kushinda.
“Kuhusu hatima ya Ukawa, ni kuwa huyu alikuwa timu Lipumba na hivyo hana madhara yoyote kwa Ukawa  kwa sababu baada ya kushinda uchaguzi aliamua kuusaliti Ukawa ambao ulimwezesha kushinda.
“Hivyo hajapunguza lolote kwa vile  hakuwa muumini wa Ukawa. Tunajua kuna jitihada kubwa za kuwarubuni baadhi ya wabunge, madiwani na viongozi wa Ukawa  waweze kujiengua au kujiuzulu kwa hoja kuwa wanaunga mkono serikali.
“Kama wanataka kufanya hivyo wanatakiwa kuchapa kazi na si kuacha kazi waliyoomba kwa wananchi … huwezi kuacha kazi ukasema unaenda kuunga mkono dhana ya hapa kazi tu wakati huna kazi,” alisema Mrema.
WASOMI WATOFAUTIANA
Akizungumzia hatua hiyo ya Mtulia, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO), Profesa GaudenceMpangala, alisema kujitoa kwake  na wengine wanaofanya hivyo, ni wazi  siasa ya Tanzania ina matatizo makubwa.
Alisema haiwezekani mbunge akajitoa kabla ya kumaliza muda wake huku akisahau maelfu ya wananchi waliomchagua.
Mpangala alisema katika nyakati hizi ambazo demokrasia imeminywa huku katiba mpya ikikataliwa, alitegemea upinzani ungejiimarisha kwa kupigania hayo lakini si kukimbilia kulekule.
“Huu ni ubinafsi. Wakati huu nilitegemea upinzani wangejiimarisha kwa sababu ni wazi kwamba demokrasia imeminywa, Katiba mpya imekataliwa. “Ilikuwa ni wakati wao kusimama pamoja kupigania hayo badala ya kufanya hivyo ndiyo unakimbilia kulekule… ndiyo maana nimesema kuna utata mkubwa. Binafsi nachanganyikiwa kabisa kwa haya yanayoendelea.
“Ninavyoona siasa ya Tanzania ina matatizo. Haiwezekani mtu unajitoa katikati, bora ungesubiri muda wako uishe vinginevyo hiyo haieleweki.
“Wananchi walikuchagua na imani yako kwa chama chako sasa wewe unaamua kama mtu binafsi unasahau wale maelfu waliokuchagua katika misingi ya chama chako, unavyojiuzulu binafsi wala hushauriani na wananchi waliokuchagua, hili ni tatizo kubwa.
“Wanasiasa wa sasa wengi ni wasomi, sielewi elimu wanayopata, nahisi ina utata haina misingi ya demokrasia na wanaofanya hivyo wanaangalia masilahi yao ukizingatia serikali ya sasa inabana upinzani hivyo wanaona ukiwa kule utanufaika.
“Yule wa Singida Kaskazini (Lazaro Nyalandu) sababu alizotoa zilikuwa nzito na alikuwa na hoja, lakini wengine hawana hoja eti yale waliyokuwa wakiyapigania sasa yanatekelezwa kwani ukiwa upinzani huwezi kufanya hivyo?”aliuliza Profesa Mpangala.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema sababu zilizotolewa na Mtulia zisipuuzwe.
“Mbunge alipigania ubunge wake hivyo anaona upinzani umeshanyang’anywa donge mdomoni. Kitendo cha kujiondoa na CUF unaijua iko vipande vipande, hivyo wanawanyima wananchi haki hivyo ameona bora ajiondoe.
“Kuacha ubunge si jambo la kawaida ni nyeti unapoteza mamilioni yako ni uamuzi mgumu na mkubwa lakini lazima tuuheshimu,”alisema Dk. Bana.

PROFESA NDALICHAKO NA HATIMA YA TAIFA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema ikiwa taifa litashindwa kusonga mbele kwa maendeleo litachangiwa na watu kukosa hofu ya Mungu.
Kauli hiyo aliiyoa   Dar es Salaam jana katika ibada maalumu ya kuwaombea wanafunzi wa vyuo vikuu iliyoandaliwa na Kanisa la Tanzania Assemblies of God linalojulikana kama City Christian Centre lililopo Upanga.
Alisema ni jambo la busara na lenye kumpendeza Mungu kwa TAG kuandaa ibada hiyo kwa vile  vijana wengi siku hizi wamekuwa wakijiingiza katika makundi yasiyofaa yakiwamo ya kutumia dawa za kulevya.

Waziri alisema vijana ndiyo taifa la leo na kama wengi wao wanahitaji kuingia katika siasa baadaye basi ni vema wakawa na hofu ya Mungu ili baada ya siasa kuwaneemesha waweze kuitumikia jamii.

“Nimeona Mchungaji alipouliza wangapi baada ya kumaliza vyuo vyao wanataka siasa wengi mlinyoosha mikono.
“Hapa ni vizuri mkajua kwenye siasa si kwa ajili ya kujitumikia ninyi wenyewe bali kuwatumikia Watanzania walio wengi na wenye mahitaji,’’ alisema Profesa Ndalichako.
Alisema kanisa lina wajibu wa kuwafundisha vijana uadilifu na endapo wakiwa na hofu ya Mungu basi mambo maovu yataepukika.
Alisema ni lazima kijana huyo atakuwa na uwezo wa kupambana na watu wenye utovu wa nidhamu, watumiaji wa dawa za kulevya kama ambavyo serikali inafanya kwa sasa  sambamba na kupambana na ufisaidi.
Askofu Mkuu wa Kanisa hilo,  Dk. Ranwell Mwenisongole,  alisema ibada ya aina hiyo itakuwa inafanyika mwaka hadi mwaka lengo likiwa ni kuongeza maadili na mioyo ya upendo kwa wanafunzi na vijana.
Baadhi ya wanafunzi waliliohudhuria ibada hiyo wanatoka Chuo cha Afya Muhimbili (MUHAS), Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU),  Chuo cha Usafirishaji (NIT) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

Wahudumu wa ndege waliona kombora la Korea Kaskazini likipaa

This photo taken on 29 November 2017 and released on November 30, 2017 by North Korea's official Korean Central News Agency (KCNA) shows launching of the Hwasong-15 missile which is capable of reaching all parts of the US.Haki miliki ya pichaAFP/KCNA
Image captionWahudumu wa ndege waliona kombora la Korea Kaskazini likipaa
Wahudumu kwenye ndege ya shirika la Cathay Pacific iliyokuwa katika anga ya Japan waliripoti kuona Kombora la Korea Kaskazini lililokuwa likifanyiwa majaribio wiki iliyopita.
Shirika hilo lilithibitisha kwa BBC kuwa wahudumu wa ndege waliona kitu ambacho kilikisiwa kuwa kombora hilo likiingia kwenye anga ya dunia.
Tarehe 29 mwezi Novemba Korea Kaskazini ililifanyia jaribio kombora la masafa marefu ambalo ilisema kuwa linaweza kufika popote pale nchini Marekani.
Cathay Pacific aircraftHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWahudumu wa ndege waliona kombora la Korea Kaskazini likipaa
Jaribio hilo lilizua msukosuko zaidi na Korea Kaskazini na pia Marekani, ambao Jumatatu walianzisha mazoezi yao makubwa zaidi ya angani kuwai kufanya, ambayo yametajwa na Korea Kaskazini kuwa uchokozi.
Kombora hilo lililotajwa na Korea Kaskazini kuwa lenye nguvu zaidi lilianguka katika maji ya Japan lakini likapaa mbali zaidi kuliko kombora lolote kuwai kufanyiwa majaribio.
Kinyume na nchi zingine Korea Kaskazini mara nyingi haitangazi ikifanyia majaribio makombora yake na na wala haitoi tahadhari na njia mbayo hupitia mara nyingi hajulikani.
A US Air Force F-22 Raptor stealth jet flies over the air base at Gwangju as joint military exercises with South Korea get under wayHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMazoezi hayo yanashirikisha ndege 230 zikiwemo ndege hii aiana ya F-22 Raptor stealth jets na maelfu ya wanajeshi
Pyongyang haina uwezo wa kupata data ya safari za angani ili ipate kuelewa kabla ya kufanya jaribio lolote la kombora.
Mazoezi hayo ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini yatadumu kwa muda wa miaka mitano.
Yanashirikisha ndege 230 zikiwemo ndege aiana ya F-22 Raptor stealth jets na maelfu ya wanajeshi.