Monday, November 13

WAZIRI MPINA ATOLEA UFAFANUZI UCHOMAJI WA VIFARANGA


Mawakili wa Lulu wajipanga kukata rufaa


Dar es Salaam. Muda mfupi baada ya  Mahakama Kuu kumuhukumu msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Elizabeth Michael kifungo cha miaka miwili jela, msanii huyo  alianza mapambano upya kuhakikisha anarejea tena uraiani kwa njia ya dhamana na rufaa.
Jaji Sam Rumanyika alimhukumu  adhabu hiyo msanii huyo baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Steven Kanumba bila kukusudia.
Kanumba ambaye  pia alikuwa mwigizaji maarufu wa filamu ndani na nje ya nchi alifariki dunia April 7, 2012, kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo wake lijulikanalo kwa kitaalamu kama Brain Concussion, lililosababisha mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi.
Alipatwa na tatizo hilo wakati wa ugomvi ulioibuka baina yao usiku huo nyumbani kwake Sinza Vatcan, kutokana na wivu wa kimapenzi, baada ya kumtuhumu mpenzi wake huyo kuongea na simu na mwanaume mwingine.
Japo msanii huyo alikana shtaka la kumuua mpenzi wake huyo bila kukusudia akidai kuwa hahusiki kwa vyovyote na kifo hicho, bali mpenzi wake alijigonga ukutani ghafla wakati akimpiga kwa ubapa wa panga, lakini Jaji Rumanyika alimtia hatiani.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye Lulu kupitia kwa mawakili wake alianza mchakato wa kujinasua kutoka katika adhabu hiyo, baada ya kuwasilisha mahakamani hapo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani.
Mmoja wa mawakili wa msanii huyo, Peter Kibatala ameieleza Mwananchi leo Jumatatu kuwa hawakuridhika na hukumu hiyo na kwamba tayari waliwasilisha mahakamani hapo taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kumtia hatiani na kumhukumu adhabu hiyo.
“Tayari tumeshawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa mahakamani (Mahakama Kuu) hivyo kilichobakia ni process (taratibu nyingine tu za kimahakama,” amesema Wakili Kibatala.
Kibatala amesema kuwa mbali na kukata rufaa pia watawasilisha maombi ya dhamana ili wakati anasubiria usikilizwaji na uamuzi wa rufaa yake akiwa nje.

Mnyika asema bomoabomoa iliyofanyika barabara ya Morogoro ni haramu



Dodoma. Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika amesema bomoabomoa iliyofanyika katika barabara ya Morogoro ni haramu kwa sababu sheria ya barabara iliyotumika ilitungwa mwaka 1932 na ilishafutwa.
Akiuliza swali bungeni leo Jumatatu Mnyika amesema Rais John Magufuli akiwa katika ziara Mwanza alitoa kauli ya kibaguzi na kwamba kama si ya kibaguzi basi Serikali itoe kauli ya kuwalipa fidia wakazi hao waliobomolewa nyumba zao.
"Kwa sababu Serikali ilisingizia sheria mimi kama mbunge nilichukua hatua nilileta marekebisho bungeni ili barabara yote iwe mita 60 lakini Serikali ikafanya njama na Katibu wa Bunge aliyeondoka(Thomas Kashililah) kuzuia huo muswada ni lini hasa ikaachana na hizi njama ikakubaliana na Rais na muswada ukaletwa hapa bungeni ili barabara hii iwe na upana wa mita 60? Amehoji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukizi na Mawasiliano, Elias Kuandikwa amesema sheria mbalimbali za barabara zilipokuwa zikitungwa zilikuwa zikizingatia maendeleo na kwamba Sheria ya Barabara ya Mwaka 1932 ilianisha ukubwa wa barabara katika maeneo yote inapojengwa.
Alimtaka mbunge huyo kuwasiliana na mamlaka za halmashauri za serikali za mitaa ambazo ndio wasimamizi kuona kama kuna mahitaji ya baadhi ya maeneo kufanyiwa marekebisho kwenye sheria hiyo.
"Hakuna njama yoyote na suala la fidia litakwenda kwa mujibu wa sheria," amesema.
Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema Kanuni za Bunge sehemu ya nne inaonyesha jinsi shughuli za Bunge zinavyopangwa na sehemu ya tano inaonyesha namna majadiliano yatakavyofanywa ndani ya Bunge.
"Si kweli kwamba Serikali ilipanga njama na Bunge kuzuia muswada wowote uliokuwa uletwe ndani ya Bunge, suala liloelezwa na Mnyika katika swali la nyongeza si kweli ni suala lililojitokeza katika muswada wake," amesema.
Mhagama amesema Serikali haina utaratibu wowote wa kula njama na Bunge.
Katika swali la msingi Mnyika alitaka kujua ni lini Serikali itawasilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya barabara ili eneo la hifadhi ya barabara iwiane na barabara nyingine.
Akijibu swali hilo Kuandikwa amesema Serikali haina mpango wa kufanya marekebisho sheria ili kufanya barabara ya Morogoro kuwiana na barabara kuu nyingine kwa kuwa eneo la hifadhi la barabara hiyo lilotengwa linahitahika kwa ajili ya upanuzi wa barabara ili kuwiana na mahitaji ya sasa na ya miaka ijayo.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amesema Mkoa wa Dodoma hauna sababu zozote za kukumbwa na tatizo la upungufu wa Chakula wala Njaa kwa wananchi wake kwa kuwa unazo fursa za kutosha za kuzalisha mazao ya chakula yanayotosheleza mahitaji ya Mkoa. 

Aidha amesema mkoa huo una fursa za kuzalisha mazao ya biashara yatakayoweza kuwainua kiuchumi wa mwananchi na Mkoa kwa ujumla. 

Dk. Mahenge ameyasema hayo mwishoni mwa wiki akiwa katika ziara Wilayani Kongwa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Wilaya za Mkoa wa Dodoma. 

Kufuatia hali hiyo, Mkuu huyo amewataka Viongozi na wataalamu kuwasimamia wananchi kupanda mazao yanayotumia maji kidogo na kustawi kwa ufanisi Mkoani Dodoma kama Mtama, Uwele, Muhogo, Alizeti na Sasa zao la Korosho lililothibitika kustawi vizuri kwenye Ardhi ya Dodoma. 

Aidha amewataka viongozi na Wataalamu wa kilimo wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanawaelimisha na kuwasimamia wananchi kutekeleza mkakati wa kilimo wa Mkoa unaolenga kuzalisha chakula cha kutosheleza mahitaji ya Mkoa, kwa kuachana na kilimo cha mazoea badala yake unasisitiza kilimo cha maarifa, na cha kisasa. 

Amewatoa hofu wananchi kuwa zao la mtama mbali na kutumika kama chakula lakini lina soko la uhakika kwa ajili ya viwanda vya kutengeneza vinywaji hivyo hata kama mwananchi hataki kula mtama anaweza kuuza na akanunua chakula anachokitaka mwenyewe lengo likiwa kuwa na uhakika wa chakula. 

Amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi kwa kuanzisha kampeni ya kuondoa njaa wilayani Kongwa (ONJAKO) na kuzitaka Wilaya nyingine kuiga mfano huo. 

Awali, akielezea Kampeni ya ONJAKO Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwenye wilaya hiyo kila kaya, pamoja na mazao mengine ni lazima kulima heka mbili (2) za mtama kwa ajili ya chakula na endapo kaya yoyote itakayokaidi muhusika atalazimika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini (50) na endapo atashindwa basi adhabu ya kifungo cha miezi mitatu (3) itamkabili, Lengo likiwa kuhakikisha kila kaya inazalisha chakula cha kutosheleza mahitaji yake. 

Kadhalika, Dk.Mahenge amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Rehema Madenge kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Dodoma kuhakikisha kila Wilaya ina ainisha mahitaji ya vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya elimu ili vifaa hivyo vinunuliwe kwa mfumo wa pamoja moja kwa moja kutoka Viwandani baada ya kupata idhini ya Wizara ya Kisekta lengo likiwa kupunguza gharama za vifaa.
 
Amepiga marufuku tabia za viongozi na Wakuu wa Idara kwenye Wilaya kukaa tu ofisini na kuwataka waweke ratiba ya mara kwa mara ya kutembelea shule kufanya ukaguzi ili kubaini changamoto halisi zinazo kabili hali ya utoaji elimu na kuzitafutia majibu ya kudumu, pia ametaka Wilaya ziwape walimu ushirikiano unaohitajika ili waweze kutekeleza jukumu la kuwafundisha watoto kwa ufanisi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua mradi wa maji ya chemichemi kwenye kijiji cha Kongwa Maji
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua mashine ya kusukumia maji kwenye mradi wa maji ya chemichemi kijijini Kongwa Maji
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Suguta Wilayani Kongwa.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akiwasalimia Watoto wenye Ulemavu wa Viungo na matatizo ya akili wanaotibiwa kwenye kituo cha Watoto cha Mlali Kongwa.

VIJANA 120 KUTOKA NCHI MBALIMBALI BARANI AFRIKA KUHUDHURIA KONGAMANO LA VIJANA NA UONGOZI JIJINI DAR

JUMLA ya vijana 120 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, wanatarajiwa kuhudhuria kongamano la vijana viongozi, litakalofanyika kuanzia Novemba 15 hadi 17 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo lililoandaliwa na kuratibiwa na Shirika la Open Society Initiative For Eastern Africa(OSIEA) kwa kushirikiana na Shirika la Mulika Tanzania, litawakutanisha vijana hao na kuweza kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana wa bara la Afrika huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Waleavu, Antony Mavunde.
 
Akizungumza na waandiishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Ofisa Program Msaidizi wa OSIEA, Adam Antony, alisema kogamano hilo ni mara ya pili kufanyika baada ya lile la mara ya kwanza kufanyika mwaka jana na kushirikisha nchi za Afrika Mashariki pekee.

Antony alisema katika mkutano huo,vijana hao watakaohudhuria ni pamaoja na wale ambao tayari wameshaanzisha biashara  na miradi mbalimbali huku wengi wakiwa kutoka nchini Tanzania.

“Pia tunategemea kuwa na vijana ambao walishawahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali zao  ambao wataweza kutoa shuhuda  mbalimbali za namna walivyoweza kufanikiwa katika kazi zao kama moja ya kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa vijana ambao ni viongozi kwa sasa,”alisema Ofisa huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mulika Tanzania, Hussein Melele, alisema mada zitakazozungumziwa katika kongamano hilo ni pamoja na nafasi ya vijana kufikia Afrika tuitakayo(Agenda 2063), vijana kushirikishwa katika ngazi za maamuzi kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.

Jingine ni kujadili masuala ya rasilimali zinazopatikana Afrika na namna zinavyoweza kuwasaidia vijana katika kujiletea maendeleo kwa mmojammoja na jamii kwa ujumla.

Matarajio baada ya kufanyika kwa kongamano hilo, Melele alisema ni kutokana na kongamano hilo kuwakutanisha vijana viongozi na wadau wa maendeleo , mashirika ya kitaifa, mabalozi na wanataaluma ni wazi kwamba baadaye  wataweza kuwaonesha njia ya namna gani wataweza kufanya nao kazi pamoja.

“Aidha kongamano hili litakuwa ni daraja kwa vijana hawa kuweza kutatua changamoto katika sekta mbalimbali hususani zinazowahusu vijana wenyewe ikiwemo za afya, ajira, uongozi, elimu, biashara na mengineyo,”alibainisha Mkurugenzi huyo.

IDARA YA MAAFA YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MAAFA

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe. William Ngeleja akitoa maelezo ya awali kuhusu utendaji kazi wa kamati hiyo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 bungeni Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uratibu wa Maafa na namna Serikali inavyojenga uwezo wa Idara hiyo ili kuongeza tija wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa .
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu Maafa Novemba 12, 2017 bungeni Dodoma.
 Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu  (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Idara yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe hao iliyoandaliwa na Ofisi hiyo mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe.  Aida Kenani akichangia hoja wakati wa wakati  wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa bungeni mjini Dodoma.
 Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa mhe. Abdallah Mtolea (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati na Watendaji wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi hiyo kwa lengo la kutoa uelewa wa masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Mmoja wa wawezeshaji kutoka Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ili kutoa uelewa wa masuala  ya Menejimenti ya maafa nchini Novemba 12, 2017. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)


Ofisi ya Waziri Mkuu imeendesha warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo inayohusu Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa masuala ya Menejimenti ya maafa nchini.
Akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Novemba 12, 2017 Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.William Ngeleja alieleza kuwa warsha hiyo itawajengea uwezo wajumbe wa Kamati hususani katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Warsha hii ni muhimu kwa wajumbe wa kamati kwani itaongeza uelewa kuhusu sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 pamoja na dhana nzima ya Menejimenti ya Maafa"

Akifanua mhe.Ngeleja amesema warsha hiyo itasaidia kuongeza tija katika utendaji wa kamati hasa katika kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya maafa.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwaeleza wajumbe kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini ili kujenga uwezo wa Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali pindi maafa yanapotokea hivyo warsha hii inatija kwa wajumbe wote.

"Warsha hii itasaidia kuongeza uelewa kwa wajumbe kuhusu namna bora ya kupambana na majanga yanapoytokea nchini na madhara yake, vyanzo na sababu za kutokea, hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia, kupunguza  madhara, kujiandaaa , kukabili na kurejesha hali katika ubora zaidi" Alisisitiza Mhe. Mhagama.

Sambamba na hilo Mhe. Mhagama alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini kwa kuanzisha Idara ya uratibu wa maafa inayotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Pamoja na hatua hizo Serikali ina sera ya Taifa ya Usimamizi wa maafa ya mwaka 2004 ambayo inaeleza hatua na majukumu ya wadau mbalimbali katika shughuli za Manejimenti ya maafa na kutoa muongozo wa utekelezaji wake.

Aidha mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Mhe.Elibariki Kingu alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendesha warsha hiyo na kushauri serikali kuwekeza zaidi katika kupambana na majanga yanayoweza kujitokeza hapo nchini.

AWALI
Mada zilizowasilishwa katika warsha hiyo zilijikita katika Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa hapa nchini ikiwa ni moja ya jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuwajengea uwezo wadau na wananchi kwa ujumla ili kuweza kuyakabili maafa pindi yanapotokea. Warsha ilikuwa ya siku moja iliyojumuisha wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu masuala ya Menejimenti ya Maafa iliyofanyika Bungeni Dodoma.

WAZIRI MWAKYEMBE:WATANZANIA JITOKEZI KUMSHANGILIA BONDIA WETU IBRAHIM CLASS

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kumshangilia bondia Ibrahim Class katika pambano lake la kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia kutoka Afrika ya Kusini  Koos  Sibiya.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito huo jana  jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake bondia  kwa pambano litakalofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017.

“Bondia huyo anauwezo mkubwa na amekwisha kushinda mara mbili kwa Afrika na kwa mkanda huu wa kugombea ubingwa wa dunia nimeona ni vyema akapigania hapa nchini ili watanzania waweze kuona uwezo wake na pamoja na kumongezea ari ya kupambana kwa ajili ya watanzania walikuja kumuunga mkono,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea  kuzungumza katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alisema  atasimamia mchezo wa ngumi na kuhakikisha unarudisha heshima yake kama ilivyokuwa zamani kwa kuhakikisha anadhibiti wapiganaji wanaokwenda kwenye mapambano na kununuliwa huku wakililetea sifa mbaya taifa ya kutumika kupandisha watu madaraja.

Kwa upande wa Bondia Ibrahim Class wa nchini aliwahakikishia watanzania kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha anauchukua ubingwa huo na mkanda huo kubaki nchini huku akiwataka watanzania kuja kujionea wenyewe namna atakavyopambana na kuonyesha uwezo wake.

“ Nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa  waje kujionea wenyewe jinsi gani nitakavyo mpiga huyo mwafrika kusini na kuchukua mkanda nimejiandaa vizuri na mazoezi ninayofanya niyakiwango cha juu,”alisema bondia Class.
Pamoja na hayo nae Rais wa TPBC Bw.Chaurembo Palasea aliongeza kuwa mchezo wa ngumi umekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ulingo kwa ajili ya kufanyia mazoezi kwani hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa sekta ya mchezo wa ngumi. 

Halikadhalika Waziri Mwakyembe  amesema kuwa serikali itaanzisha bodi itakayosimamia sekta ya ngumi kwa lengo la kuondoa kukosekana kwa dira ya usimamizi wa sekta ya ngumi nchini.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia) akitoa wito kwa watanazania  kujitokeza kwa wingi uwanja wa uhuru tarehe 25/11/2017 kushangilia pambano la bondia Ibrahim Class (kushoto)  wanchini akitetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini leo jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo  kambini  Joe Gym  Kawe. yake ya mazoezi .
 Bondia Ibrahim Class (kulia) akifanya mazoezi na Mwalimu Msaidizi Bw.Kelvin Magembe (kushoto) kuonyesha uwezo wake mbele ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia)alipomtembelea kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano litakalofanyika kati yake na Bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017 Uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.

 Bondia Ibrahim Class (kulia) akimkabidhi  zawadi ya tisheti yenye jina lake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) alipomtembelea bondia huyo  kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano la tarehe 25/11/2017 katika uwanja wa uhuru na bodia wa Afrika ya Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati leo jijini Dar es Salaam.

MHANDISI MTIGUMWE AITAKA BODI YA KAHAWA KUONGEZA UZALISHAJI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua kiwanda kidogo cha uzalishaji wa kahawa katika Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili Ofisi hizo kwa ziara ya kikazi.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameitaka Bodi ya Kahawa ambayo ni Taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kusimamia sekta ya Kahawa nchini kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa Kahawa nchini kwani  Kahawa ni miongoni mwa mazao ya kipaumbele.

Mhandisi Mtigumwe ametoa Rai hiyo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa Mara baada ya kutembelea Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa Railway, Kata ya Mawenzi Katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa Mwaka 2011 wadau waliandaa na kupitisha mkakati wa miaka 10 wa maendeleo ya Kahawa ambayo lengo kuu ilikuwa ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia Tani 80,000 Mwaka 2017 na Tani 100,000 Mwaka 2021 lengo ambalo halijafikia na bado uzalishaji ni mdogo hivyo kuongeza uzalishaji linapaswa kuwa jambo la haraka iwezekanavyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua namna Kahawa inavyohifadhiwa tayari kwa kuingia sokoni.

Katibu Mkuu Alimuelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa Kahawa na uhamasishaji Masoko Kufanya Utafiti ili kubaini nini chanzo cha uzalishaji mdogo wa Kahawa iwapo wananchi kutotunza vizuri kahawa yao, Hali ya hewa na udongo au mbegu sio nzuri zinazotumika.

Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inajipanga kwa kampeni kubwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kufahamu umuhimu wa kulima kwa wingi mazao ya Chakula na Biashara ikiwemo zao la Kahawa.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo, Alisema miongoni mwa sababu ambazo huchangia uzalishaji mdogo katika mazao mbalimbali nchini huwa ni pamoja na Wananchi kuchanganya mazao wakati wa kupanda jambo ambalo sio rafiki sana katika Kilimo, sambamba na Kutoacha nafasi kati ya mche na mche.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza na wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazo.

Mhandisi Mtigumwe aliitaka Bodi ya Kahawa Kufanya Utafiti wa maeneo ambayo Kahawa inastawi kwa wingi ili kuongeza sehemu za kuzalisha Kahawa kufikia uzalishaji wa kiwango kikubwa tofauti na ilivyo hivi sasa.

Hata hivyo amesema kuwa atazishughulikia haraka iwezekanavyo Changamoto za Uzalishaji, Changamoto za Ubora, Changamoto za Masoko sambamba na Changamoto za Sekta.

Majukumu ya Bodi ya Kahawa ni pamoja na usimamizi wa sheria namba 23 ya marekebisho yake ya Mwaka 2009 na kanuni za Kahawa 2013 sambamba na kuratibu Majukumu shirikishi (Shared Functions) Baina ya serikali na wadau.
Muonjaji katika Maabara ya Kahawa Bi Regina Mushi Daud akiendelea na majukumu yake katika maabara ya Kahawa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko Kutoka Bodi ya Kahawa akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe namna wanunuzi wanavyokabiliana katika ununuzi wa Kahawa
Picha ya pamoja wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.

Tetemeko nchini Iran na Iraq lawaua zaidi ya watu 348

A damaged storefront is seen after an earthquake in Halabja, IraqHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTetemeko nchini Iran na Iraq lawaua zaidi ya watu 200
Tetemeko la ukubwa wa 7.3 katika vipimo vya richa limekumba eneo la kaskazini mwa Iran na Iraq na kuua watu kadha.
Takriban watu 348 waliuawa katika mkoa ulio magharibi mwa Iran wa Kermanshah, kwa mujibu wa maafisa.
Tetemeko hilo lilizua hofu hadi kusababisha watu kukimbia kutoka manyumbani mwao kwenda barabarani.
Misikiti kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad, imekuwa ikifanya maombi kwa kutumia vipasa sauti.
Wengi wa waathiriwa walikuwa ni kwenye mji wa Sarpol-e Zahab, kilomita 15 kutoka mpakani.
Kulingana na kituo cha Marekani USGS tetekemo hilo lilitokea umbali wa kilomita 33.9 chini ya ardhi la lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait
Three Baghdad residents in the streets after a powerful earthquake struck
Image captionTetemeko nchini Iran na Iraq lawaua zaidi ya watu 200
Uharibifu umeripotiwa kuetka katika vijiji vinane kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Iran Morteza Salim.
Baadhi ya vijiji vimekumbwa na matatizo ya nguvu za umeme na mawasiliano yamevurugwa
Makundi ya uokoaji yanatatizwa na maporomoa ya ardhi.
Tetemo hilo lilitokea kilimita 30 kusini magharibi mwa mji wa Halabja karibu na mpaka wa Iran.
Lilitokea umbali wa kilomita 33.9 na lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait.
A map showing an earthquake in the Iran-Iraq border region
Image captionTetemeko nchini Iran na Iraq lawaua zaidi ya watu 200

PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA LEO NOVEMBA 13,2017