Tuesday, October 3

Meya wa jiji Kampala apelekwa kusikojulikana



Meya wa jiji la Kampala, Erias Lukwago .
Meya wa jiji la Kampala, Erias Lukwago . 
Kampala, Uganda. Harakati za kupinga kuondolewa ukomo wa umri wa rais zimeendelea kuwa chungu kwa wapinzani baada ya viongozi kadhaa wa Forum for Democratic Change (FDC) akiwemo meya wa jiji Erias Lukwago kukamatwa.
Kiongozi mwingine aliyekamatwa kuhusiana na sakata hilo ni Katibu Mkuu wa Uhamasishaji wa FDC Ingrid Turinawe huku na nyumba za wabunge wawili ikiwemo ya Bobi Wine kulipuliwa na watu wasiojulikana.
 Meya Lukwago amekamatwa na polisi nyumbani kwake Wakaliga, tarafa ya Rubaga na amepelekwa kusikojulikana. Polisi walizingira nyumba ya Lukwago na wakamzuia kuondoka.
Wakati akizungumza na waandishi mapema Jumanne Lukwago aliilaumu serikali kwa kuigeuza nyumba yake kuwa kambi ya jeshi na kwa kukiuka haki zake wakati akitetea katiba.
"Haya yote yanaonyesha kwamba Rais Yoweri Museveni anaogopa nguvu ya umma. Kamwe hatutamruhusu kuchezea katiba kwa sababu ni jukumu letu kama raia. Ni lazima tupambane na tabia hii ya kuponyoka makosa," alisema Lukwago.
Taarifa zinasema wiki iliyopita mabomu mawili ya kurushwa kwa mkono yalitupwa kwenye nyumba za Mbunge wa Rubaga Kaskazini Moses Kasibante saa moja tu baada ya kurejeshwa nyumbani na polisi waliokuwa wanamshikilia kituo cha Kibuli baada ya kukamatwa bungeni.
 “Tumepokea taarifa kwamba mabomu yalirushwa kwenye nyumba za wabunge wawili Allan Ssewanya (Makindye Magharibi) na Robert Kyagulanyi (Kyaddondo Magharibi). Timu zetu zimeanza kuchunguza matukio hayo,” amesema msemaji wa polisi Asan Kasingye.
Bomu katika makazi ya Ssewanyana lilirushwa saa 7.20 usiku. “Watu wasiojulikana wamerusha bomu la mkono kwenye nyumba yangu,” alithibitisha Ssewanya kupitia Facebook.
Katika eneo la Magere, wilaya ya Wakiso, Kyagulanyi ambaye ni maarufu kwa jina la Bobi Wine amesema nyumba yake ilirushiwa mabomu matatu ambayo yalilipuka na kuvunja madirisha ya chumba cha kulala mtoto wake.

Kuku mweusi aliyefungwa kitambaa cheupe azusha taharuki


Geita. Ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni, ndivyo unavyoweza kusema baada ya watu wasiofahamika kumfunga kuku kitambaa cheupe mithili ya sanda na kumweka nyumbani kwa Emanuel Kabodi, mkazi wa Mtaa wa 14 Kambarage mjini Geita.
Tukio hilo lililovuta watu wengi limetokea leo Jumanne saa 11:00 alfajiri.
Mama wa familia hiyo, Scholastica Nicodemus alipoamka kuanza shughuli za siku alishangaa kumkuta kuku huyo nje ya nyumba yake huku geti likiwa limefungwa.
Akizungumza nyumbani kwake, Nicodemus amesema ni kawaida yake kuamka alfajiri kwa ajili ya shughuli za nyumbani ili baadaye aweze kwenda kwenye biashara zake sokoni.
“Nilivyotoka nje nilikuta kitu kimefungwa na kitambaa cheupe, nilirudi ndani nikamwita mume wangu aje aone. Alitoka kwa hofu nikamwambia asiogope kwa kuwa ameokoka,” amesema.
Nicodemus amesema alimuita mchungaji ambaye baada ya kufungua kitambaa walikuta kuku mweusi akiwa amepitishwa kwenye moto akiwa amefungwa kitambaa cheupe.
Amesema tukio hilo wanalihusisha na ajali iliyotokea juzi Jumapili na mume wake kunusurika kifo baada ya gari lake kuacha njia na kupinduka.
“Kuna mambo ya ajabu, juzi alipata ajali ambayo hata haieleweki. Si mara ya kwanza huwa anakuta chura ndani ya gari kwenye mazingira yasiyoeleweka ila sisi tunamuamini Mungu wala hatuogopi,” amesema Nicodemus.
Askofu wa Kanisa la Pentekoste (TMRC), Stefano Sagada amesema tukio hilo la kuku linaonyesha jinsi watu walivyo na imani haba.
Amewataka wananchi waache kuamini ushirikina na badala yake wamtegemee Mungu.
“Mungu yupo na yeye ndiye zaidi ya kila jambo. Watawatisha kwa vitu vya aina nyingi lakini mkimtazama Mungu yote yatawezekana na adui zenu hawatafanikiwa,” amesema Askofu Sagada.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa 14 Kambarage, Justa Fungameza amesema yamekuwepo matukio ya ajabu mtaani hapo yanayohusishwa na ushirikina.
Amesema kwa mwaka huu, tukio hilo ni la tatu baada ya mawili yakihusisha mtoto anayedaiwa kufufuka na mwingine  mchanga aliyezikwa kufukuliwa na mwili kukutwa kwenye boksi pembeni mwa kaburi.
Mjumbe mwingine, Stefano Mayovu amesema kinachosababisha mambo hayo ni chuki binafsi, wivu na wananchi kutoamini Mungu na badala yake kuamini ushirikina.

Magufuli awaonya wakurugenzi wanne kwa ulevi



Rais  John  Magufuli

Rais  John  Magufuli 
Dar es Salaam. Rais John Magufuli, ametoa onyo kwa wakurugenzi wanne wa halmashauri nchini walioanza kujihusisha na matumizi ya kilevi, akiwataka waache mara moja na ikiwezekana waokoke.
Rais Magufuli ambaye hakuwataja wakurugenzi hao, amesema wapo na tayari taarifa zao ameshazipata hivyo waache tabia hizo na badala yake wajikite kuwatumikia wananchi.
Tabia ya ulevi imeonekana kuwa ni dosari kubwa kwa wateule wake, baada ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwangwa mwaka jana kutokana na ulevi.
Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Kitwanga baada ya kuingia bungeni kujibu swali linalohusu wizara hiyo akiwa amelewa.
“Nimesikia kuna wakurugenzi watatu, wanne waache mara moja na ikiwezekana waokoke kabisa,” ameonya Rais Magufuli wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) unaofanyika Dar es Salaam leo na kesho Jumatano.
Katika mkutano huo uliowakutanisha mameya kutoka mikoa yote nchini, mwenyekiti wa jumuiya hiyo Gulamhafeez Mukadam aliwasilisha changamoto kadhaa ikiwamo hali ngumu ya madiwani hivyo waongezewe posho kutoka Sh350, 000 hadi Sh800,000, ombi ambalo lilikataliwa na Rais Magufuli.
Hata hivyo, Rais Magufuli ameeleza umuhimu wa Alat katika utekelezaji wa Ilani na mikakati yake kwa Watanzania, kubaliana na kuahidi kushughulikia changamoto za uhaba wa watumishi katika halmashauri na ucheleweshwaji na uhaba wa ruzuku za miradi ya maendeleo.
Akijibu mapendekezo hayo, amesema Serikali licha ya kutoajiri mwaka jana, tayari imeshatangaza ajira mpya 52,000 zitakazojaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi hewa zaidi ya 20,000 pamoja na walioondolewa kwa vyeti feki 12,000.
Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli alitumia zaidi ya saa mbili kueleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miezi 23 ya uongozi wake, kueleza miradi mipya ya Serikali, dhamira yake katika kudhibiti mitandao ya ufisadi huku akiwataka Watanzania kuvumilia katika mabadiliko aliyoanzisha.

Rais Magufuli ataka wakuu wa mikoa waige kwa Makonda


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amezungumzia elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kwamba suala hilo lilianzishwa wakati kiongozi huyo alipojaribu kuwakamata wahusika wa dawa za kulevya.
Hata hivyo, alisisitiza kwamba elimu yake (Makonda) siyo kitu kwake na kwamba hata angekuwa hajui kusoma yeye ni bora kwake kwa sababu anafanya kazi nzuri ambayo hata baadhi ya waliosoma hawaifanyi.
Rais Magufuli aliyasema hayo leo Jumanne wakati akifungua mkutano mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kauli hiyo ya Rais imekuja ikiwa ni muda mrefu tangu watu mbalimbali walipoanza kuhoji elimu ya Makonda huku akituhumiwa kuwa amefoji vyeti vyake vya elimu. Hata hivyo, Rais Magufuli amesisitiza kwamba mkuu huyo wa mkoa anafanya kazi nzuri na wakuu wengine wa mikoa waige mfano wake.
Rais Magufuli amesema mtu yeyote ambaye atawakamata wauzaji dawa za kulevya ni bora zaidi kwake kwa sababu ataokoa watoto wengi wa Watanzania ambao wanaathirika na dawa hizo huku watoto wa wauzaji wakiwa na maisha mazuri.
“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipojaribu kuzungumza kidogo, vita ikawa kubwa kwake, hajasoma hajafanya nini… Mimi hata kama hajui ‘a’ ili mradi anashika madawa ya kulevya huyo ni msomi mzuri.”
“Kwani wenyeviti mliopo hapa wote mmesoma? Kwani halmashauri haziendi vizuri? Kwani hamkupata matokeo mazuri kwenye ripoti ya CAG? Hata wasomi wengine wazuri wametuangusha, kinachohitajika ni uzalendo na kuipenda Tanzania,” amesema Magufuli.
Amesisitiza kwamba wahusika wa dawa za kulevya wakikamatwa nje ya nchi wahukumiwe kwa sheria za huko huko hata kama ni kunyongwa basi wanyonge. Amesema madhara ya dawa za kulevya ni makubwa.
Amesema mtu akishaingia kwenye vita ya dawa za kulevya hawezi kupendwa na wauzaji wa dawa hizo na kuwa yeye hataki wampende bali anataka kuokoa vijana wengi wanaoathirika na dawa hizo.
Rais Magufuli alimpongeza mkuu wa mkoa kwa kazi anayofanya na kuwataka wakuu wengine wa mikoa nchini kuiga kutoka kwake kwa kubuni miradi na kuomba fedha kwa kampuni mbalimbali kwa ajili ya miradi hiyo.
“Waziri mkuu, waambie wakuu wa mikoa wengine waige mfano wa Makonda, anafanya kazi kubwa ya kuomba fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Nimeambiwa kwenye kampeni yake ya nyumba za walimu tayari amekusanya Sh186 milioni,” amesema Rais Magufuli akimwambia Waziri Mkuu Majaliwa.

Aliyekuwa rais wa Iraq aaga dunia

Aliyekuwa Rais wa Iraqi na kiongozi mkuu wa Wakurdi, Jalal Talabani, amefariki.
Image captionAliyekuwa Rais wa Iraqi na kiongozi mkuu wa Wakurdi, Jalal Talabani, amefariki.
Aliyekuwa Rais wa Iraqi na kiongozi mkuu wa Wakurdi, Jalal Talabani, amefariki.
Talabani ameaga dunia huko Ujerumani, akiwa na umri wa miaka 83.
Aliingia kwa mara ya kwanza katika siasa za Wakurdi akiwa kijana mdogo na akapanda ngazi hadi kufikia ngazi ya juu kwenye uongozi wa kundi la Wakurdi pamoja na kiongozi nchini Iraq kupitia hatua ya ugawanaji mamlaka, baada ya kupinduliwa kwa hayati Rais Saddam Hussein.
Kama Rais, Bwana Talabani aliamua kutumika kama muunganishi mkuu, kwa Wairaqi wote, na pia kujaribu kurejesha uhusiano mzuri na mataifa jirani.
Aliunga mkono juhudi za Marekani kuivamia Iraq.

Trump: Muuaji wa Las Vegas ana matatizo ya kiakili


Baadhi ya waliohudhuria tamasha hilo wakitoroka kufuatia shambulio la bwana PaddockHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBaadhi ya waliohudhuria tamasha hilo wakitoroka kufuatia shambulio la bwana Paddock

Rais Donald Trump wa Marekani amemtaja muuaji wa watu 59 huku 527 wakijeruhiwa mjini Las Vegas kuwa mgonjwa aliye na akili punguani.
Akizungumza katika ikulu ya Whitehouse , amesema kuwa ataziangazia upya sheria za umiliki wa bunduki katika siku za usoni lakini hakuelezea zaidi.
Maafisa wa polisi wanajaribu kubaini kwa nini Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa katika tamasha akiwa katika ghorofa ya 32 karibu na hoteli ya Mandalay Bay.
Polisi walipata bunduki 23 katika chumba chake pamoja na vilipuzi.
Kufikia sasa hakuna sababu mwafaka iliotolewa na wachunguzi hawajapata ishara zozote za shambulio hilo kuhusishwa na ugaidi wa kimataifa.
Baadhi ya wachunguzi wamesema kuwa Paddock alikuwa na historia ya matatizo ya kiakili, lakini hilo halijathibitishwa.
Paddock hajakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu na hakuwa akijulikana na maafisa wa polisi.

Mshukiwa wa mauaji ya las Vegas Stephen PaddockHaki miliki ya pichaFAMILIA YA PADDOCK
Image captionMshukiwa wa mauaji ya las Vegas Stephen Paddock

Akizungumza na wanahabari wakati alipokuwa akijiandaa kupanda ndege ya rais, bwana Trump alisema kuwa Paddock ni mgonjwa wa kiakili .
''Ana matatizo chungu nzima, na tunamchunguza kwa kina'' .
Alipoulizwa, bwana Trump alikataa kuliita shambulio hilo ugaidi wa nchini.
Kuhusu swala la udhibiti wa bunduki, rais alisema: Tutakuwa tukizungumzia kuhusu sheria za bunduki siku sijazo.
Rais Trump ambaye mipango yake kuhusu udhibiti wa bunduki umebadilika katika miaka ya hivi karibuni hakutoa maelezo zaidi.

Mwandishi akamatwa kwa ''habari ya nguo za ndani'' za Bi Mugabe

Bi Grace Mugabe adaiwa kuwagawanyia wafuasi wa Zanu PF ngu za ndaniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBi Grace Mugabe adaiwa kuwagawanyia wafuasi wa Zanu PF ngu za ndani
Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wanamzuilia mwandishi mmoja wa habari kuhusu taarifa yake iliodai kwamba mbunge mmoja wa chama tawala cha Zanu-PF aliwapatia wafuasi wa chama hicho nguo za ndani kwa niaba ya mke wa rais bi Grace Mugabe kulingana na mawakili wa ripota huyo.
Habari hiyo ilichapishwa katika jarida la Newsday, linalomilikiwa kibinafsi.
Polisi mashariki mwa mji wa Mutare walimkamata Kenneth Myangani siku ya Jumatatu jioni , mawakili wa haki za kibinaadamu walisema katika taarifa.
Mwandishi huyo kutoka Mutare huenda akakabiliwa na mashtaka ya ''uhalifu wa kumuharibia mtu jina'' baada ya kukamatwa kwa kuandika na kuchapish habari kuhusu ufadhili wa nguo za ndani zilizotumika na bi Grace Mugabe.
Kulingana na gazeti hilo, nguo hizo zilisambazwa na mbunge wa eneo hilo Esau Mupfumi ambaye alisema kuwa zilitolewa na bi Mugabe.
Wakili wa mwandishi huyo alisema kuwa haijulikani iwapo mlalamishi alikuwa mbunge huyo ama mke wa rais.
Hali mbaya ya kiuchumi nchini Zimbabwe inawalazimu watu wengi kununua nguo zilizotumika kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Kinasema kuwa vitu hivyo ni kama vile nguo za ndani kutoka mataifa ya magharibi ambazo huingizwa nchini Mozambique kwa bei rahisi.
Mke wa rais bi Grace Mugabe alivutia vyombo vya habari mnamo mwezi Agosti wakati aliposhutumiwa kwa kumshambulia mwanamitindo katika hoteli moja ya Johannesburg ambapo watoto wake walikuwa wakiishi. Amekana kufanya makosa yoyote.

KUMBUKUMBU YA KUZALIWA ADELINE MAWALLA MKINDI 03/10/1947


Dearest Mother,
Today was supposed to be your birthday, but you are no longer with us.
Even if you are no longer with us, we still celebrate you for what you were.
We still remember your devotion in helping others
Your advices when anybody goes astray
Your intelligence in knowing what is supposed to be done
You discipline in life in general as you were a teacher
Missing you my dearest mother …
Today is truly filled with memories of happiness and tears  
Wonderful birthday in heaven mom!
Although we will always miss you,
The endless joy you brought to our lives still brings warmth to our hearts.
On this birthday of yours, we wish you to be happy wherever you are right now.
I your son Idris, your daughter Zainab and son in law George,
Your grandchildren Ilu, Ruby, Idris jnr. and Fidel
Pamella and her family
Your sisters Maria, Ericka, 
Brothers Simon, Ilet and their families
Relatives, neighbors and friends will surely remember you forever.
May your soul continue to rest in peace, Amen.

ADELINE MAWALLA MKINDI
03/10/1947 – 14/05/2016

Mama mpendwa,
Leo ilitakiwa kuwa siku yako ya kuzaliwa, lakini hauko tena na sisi.
Hata kama huko tena pamoja nasi, bado tunakusherehekea kwa ulivyokuwa.
Bado tunakumbuka kujitoa kwako kwa kuwasaidia wengine
Ushauri wako wakati mtu yeyote anapotea
Ujuzi wako kwa kujua kile kinachopaswa kufanyika
Nidhamu katika maisha kwa ujumla kwa kuwa wewe ulikuwa ni mwalimu
Nakukumbuka mama yangu mpendwa ...
Siku ya leo imejawa na kumbukumbu za furaha na machozi
Heri ys siku ya kuzaliwa huko mbinguni mama!
Ingawa tutakukosa kila wakati,
Furaha isiyo na mwisho ambayo umeleta katika maisha yetu bado huleta joto kwa mioyo yetu.
Katika siku hii ya kuzaliwa kwako, tunataka ufurahi popote ulipo sasa.
Mimi mwanao wa kiume Idris, Mwanao wa kike Zainab na mkwe George,
Wajukuu zako Ilu, Ruby, Idris jnr. na Fidel
Pamella pamoja na familia yake
Dada zako Maria, Ericka, 
Kaka zako Saimon, Ilet na familia zao
Jamaa, majirani na marafiki hakika tutakukumbuka daima milele.
Na roho yako iendelee kupumzika kwa amani, Amina.

ADELINE MAWALLA MKINDI
03/10/1947 - 14/05/2016

MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA WAZEE DUNIANI OKTOBA 01, 2017 YALIYOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA NYERERE SQUARE MJINI DODOMA.

MAKAMU WA RAIS AWASILI NGORONGORO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mabinti wa Kimasai waliojitokeza wakati wa mapokezi kwenye lango la kuingia kwenye hifadhi ya Ngorongoro ambapo anategemewa kuzindua Makumbusho Mpya ya Olduvai kesho tarehe 3, Oktoba 2017. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya Hifadhi ya Ngorongoro kutoka kwa Msaidizi Mkuu wa Lango Bw. Mansuet Valentine mara baada ya kuwasili kwenye hifadhi ya Ngorongoro ,Makamu wa Rais anategemewa kuzindua Makumbusho Mpya ya Olduvai kesho tarehe 3, Oktoba 2017. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MKUU WA MKOA WA MWANZA AKUTANA NA WAGENI KUTOKA MAREKANI


Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani ikiongozwa na Mwinjilisti Rojas Matias, walipomtembelea ofisini kwake jana. 

Watumishi hao walikuwa na mkutano mkubwa wa injili tangu Septemba 27 hadi Oktoba Mosi, 2017 katika uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza ulioandaliwa na kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola.

Mhe.Mongella aliwahakikishia ushirikiano mwema pindi watakapokuwa tayari kuwekeza katika shughuli mbalimbali ikiwemo za kielimu katika mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani
Wageni kutoka Marekani pamoja na mwenyeji wao Mchungaji Kulola, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani. Katikati ni Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani na kushoto ni Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Baada ya mazungumzo, watumishi hao walifanya maombi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Baada ya mazungumzo, watumishi hao walifanya maombi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati), Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani (kushoto) pamoja na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kulia)
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiwa pamoja na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kulia).
Katibu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Levi Matia (kushoto), akiwakaribisha wageni kutoka Marekani walipotembelea ofisini hapo jana.
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani ikiwa kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani ikiondoka katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza na mwenyeji wao Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (wa kwanza kushoto).
Salamu na wenyeji katika mitaa ya Jiji la Mwanza
Timu ya More International Ministry kutoka Marekani pamoja na wenyeji wao fukwe za Ziwa Victoria ili kujionea mawe ya "Bismarck Rock" katika eneo la Kamanga
Walifurahia uzuri wa eneo hili na hakika hii ni nenmbo ya Jiji la Mwanza
Walifurahia ukaaji wa mawe haya
Pia ilikuwa furaha kugusa maji ya Ziwa Victoria mubashara
Eneo hili lina mijusi wakubwa hivyo walifurahia kuitazama mubashara
Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) kutoka kanisa la kimataifa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, katika fukwe za Kishimba Beach.

PSPF YAFUNGUA OFISI MPYA PEMBA NA UKEREWE, NI SEHEMU YA WIKI YA UTUMISHI DUNIANI





NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.

MFUKO wa Pensheni wa PSPF,  umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza leo Oktoba 2, 2017.

“Mtakumbuka kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka,  huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”

Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”
Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,
hapa makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.
Aliwataja washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu, (MCB).

Alisema, PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.

Miongoni mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na maafisa wa PSPF.

“Kwa kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa uchapakazi wa namna hii.” Alisema Dkt. Msengi.