Tuesday, September 19

Musukuma, wenzake wasomewa mashtaka manne

Mbunge Msukuma na madiwani walioshiriki kufunga
Mbunge Msukuma na madiwani walioshiriki kufunga barabara zinazoingia kwenye mgodi Wa GGM September 14 wakiwa kwenye gari ya polisi 
Geita. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma na wenzake wanane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita wakishtakiwa kwa makosa manne, likiwemo la kula njama ya kutenda kosa kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo iliyovuta wananchi wengi waliojitokeza nje ya jengo la Mahakama, makosa matatu yanawahusu washtakiwa wanane na moja la kwanza linawahusu wote tisa.
Mbali ya Musukuma ambaye ni mshtakiwa wa nane; wengine ni Steven Werema ambaye ni mshtakiwa wa kwanza na ni mwananchi wa kawaida.
Wengine ni madiwani, Costantine Morandi, Winfrida Malunde, Ngudungu Joseph, Martin Kwilasa, Adija Said, Michael Kapaya na Maimuna Mengisi (anashtakiwa kwa kosa la kula njama pekee).
Mbele ya Hakimu Mkazi, Ushindi Swalo Wakili wa Serikali, Emil Kiria amedai washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka manne. Wakili mwingine wa upande wa mashtaka ni Hezron Mwasimba.
Mbali na kosa la kula njama, wanadaiwa pia kufanya kusanyiko lisilo halali, kufunga barabarana kusababisha wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) kushindwa kuingia kazini na kufanya uharibifu wa mali.
Wanadaiwa Septemba 13 saa nne asubuhi katika ukumbi wa Gedeko ulioko katika Halmashauri ya Mji wa Geita walitenda kosa la kula njama ya kutenda kosa kinyume cha kifungu cha 386 (1)(e) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16  kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
Katika kosa la pili wanadaiwa Septemba 14 saa 12:00 asubuhi katika Mtaa wa Mtakuja walifanya kusanyiko lisilo halali kinyume cha kifungu cha 74(1) na cha 75 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
Washtakiwa katika kosa la tatu wanadaiwa kufanya kizuizi kwenye barabara ya umma kinyume cha kifungu cha 239 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 .
Wanadaiwa Septemba 14 saa 12:00 asubuhi katika Mtaa wa Mtakuja wilayani Geita walitenda kosa kwa kufunga barabara inayoingia GGM na kusababisha wafanyakazi wa mgodi kushindwa kufika kazini siku hiyo.
Mbele ya Hakimu Swalo, washtakiwa katika kosa la nne wanadaiwa kufanya uharibifu wa mali kinyume cha kifungu cha sheria namba 326(6A)(a) na (6B) (e) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16  kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
Wanadaiwa saa 12:00 katika Kijiji cha Nungwe kwa nia ovu waliharibu bomba linalosambaza maji katika bwawa la Nyankanga na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh12 milioni.
Upande wa mashtaka umedai hali hiyo ilisababisha shida ya maji katika mgodi wa GGM na kwa wananchi wa mji wa Geita.
Washtakiwa wanaotetewa na mawakili Deo Mngengeli  na Neema Christian walikana kutenda makosa hayo na wako nje kwa dhamana.
Hakimu aliwataka kuwa na mdhamini mmoja kila mmoja atakayesaini bondi ya Sh5 milioni. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 10 itakapotajwa.

Musilimu: Rais anasema KA-TA mimi nasema KA-MA-TA

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Kamanda
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Kamanda Fortunatus Musilimu 
Dar es Salaam. Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Kamanda Fortunatus Musilimu ametangaza kiama kwa madereva wasiotaka kutii Sheria za barabarani.
Amesema hayo leo wakati wa Shindano la Uchoraji wa Picha za Kampeni ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa Mkoa wa Dar es Salaam lilofanyika katika Shule ya Msingi Diamond na kuratibiwa na Kampuni ya Puma Energy pamoja na Amend.
Amesema katika kutekeleza hilo, hatojali Cheo, Sura au Jinsia ya mtu yoyote ambaye atakiuka Sheria zilizowekwa.
"Nitapambana na madereva wasiofuata sheria kwa nguvu zangu zote,"amesema na kuongeza:
" Rais Magufuli anatumia maneno mawili tu kwa watu wasiotaka kulipia ankara za umeme,anasema "KA-TA", sasa mimi natumia maneno matatu tu "KA-MA-TA, ",amesema
Amesema Kikosi chake kimejipanga katika kuimarisha usalama kwa wanafunzi wote wakati wanapozitumia barabara wakati wa kwenda Shule na kurudi majumbani.
Ameipongeza Kampuni ya Puma kwa kuendesha Kampeni ya usalama barabarani kupitia uchoraji na kwamba inawajengea uwezo wanafunzi kwa kupata elimu na kujua namna ya kujikinga na ajali.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy hapa nchini,Phillipe Corsaletti amesema wameendelea kutoa elimu kwa wanafunzi ikiwa ni mkakati wa kupunguza vifo vitokanavyo na ajali kwa manufaa ya Kizazi kijacho.
Amesema hadi sasa elimu hiyo imezifikia shule zaidi ya 47 na kuwafikia wanafunzi zaidi ya 60,000 huku wakilenga kutanua wigo kuzifikia Shule zote nchini.
"Watoto wa shule ni hazina kwa Taifa, na suala la usalama wao linabaki kuwa moja ya agenda kwa kampuni yetu, "amesema
Naye, Mkurugenzi msaidizi wa Kampuni ya Amend,Tom Bishop amesema kila mwaka watu zaidi ya 1.2 Milioni hupoteza maisha huku zaidi ya 50Milioni wakijeruhiwa duniani.
Amesema hali inaonyesha Tanzania ajali zimekuwa zikipungua kutokana na jitihada za uelimishaji zinazofanywa na wadau mbalimbali.
Katika Shindano hilo lililoshirikisha Wanafunzi kutoka Shule zaidi ya 12,Mwanafunzi kutoka Shule ya msingi ya Amani,Nasri Meena (darasa la tano) ameibuka mshindi baada ya kuchora picha kwa ustadi mkubwa.
Mshindi amekabidhiwa hundi ya Sh 2 milioni na kikombe, begi na madaftari kutoka Kampuni ya Puma Energy.

Changamoto za mashirika zaanikwa

Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani, Kamanda

Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani, Kamanda Fortinatus Musilimu akimtangaza,Mwanafunzi kutoka Shule ya Amani, Nasri Meena(aliyeshika kikombe) kama mshindi wa Shindano la kuchora Picha juu ya usalama barabarani. 
Dar es Salaam. Msajili wa hazina, Dk Oswald Mashindano, ameeleza hali ya Mashirika ya Umma na kutaja changamoto zinazosababisha yasifikie utendaji kwa ufanisi unaotakiwa.
Changamoto hizo ni pamoja na kuwapo na watumishi wasio na taaluma ya kutosha, mitaji na weledi mdogo kwa wajumbe wa bodi za mashirika hayo.
Akizunguma na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki Katika Kampeni ya Usalama barabarani kwa wanafunzi, Dk Mashindano amesema bado kuna deni kubwa kuhakikisha mashirika yanakuwa na utendaji mzuri.
"Hali ya mashirika ya umma ni nzuri lakini tuna deni kubwa bado kuhakikisha yanafanya kazi kwa asilimia mia moja , "amesema.
"Tuna changamoto kwenye baadhi ya uongozi wa mashirika ikiwamo wajumbe wa bodi ambao siyo wale wenye weledi wa kutosha," amesema.
Amesema katika kutatua changamoto hizo, Mikakati mbalimbali imeanza kuchukuliwa ikiwamo kuishauri Serikali kuanza kupitia upya bodi za Mashirika zenye hisa chache.
"Tunaangalia zaidi taaluma, na tunafanya mapitio ya bodi zote za mashirika na kuangalia uhai wa wajumbe wake, "amesema
Aidha,  amesema lengo jingine ni kuboresha guidelines (maelekezo) ya utendaji kazi wa bodi

Polisi aua watu wawili akijihami

Morogoro. Watu wawili wamekufa kwa kupigwa risasi na askari polisi baada ya kuibuka mzozo kuhusu ng’ombe waliokamatwa katika Kijiji cha Nyalutanga wilayani Morogoro.
Pia, imeelezwa mtu mmoja amejeruhiwa kwa risasi kwenye makalio na ng’ombe 35 wameuawa na zaidi ya 40 kujeruhiwa katika mzozo huo.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa amethibitisha vifo vya watu hao wawili, akisema hana taarifa kuhusu aliyejeruhiwa.
Dk Kebwe amesema mzozo huo umeshapatiwa ufumbuzi na waliokufa katika tukio hilo wamezikwa leo Jumanne, huku uchunguzi ukiendelea kuhusu wananchi waliojichukulia sheria mkononi na kumshambulia kwa mawe askari aliyefika kutuliza mzozo huo.
Mkuu wa mkoa amesema ameunda kamati kuchunguza tukio hilo ambalo lilisababisha askari kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi waliokuwa wamemzonga na kwa bahati mbaya risasi ziliwapata watu wawili.
Amesema watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria. Pia, amewaonya wafugaji wanaoacha mifugo ikizurura ovyo.  
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyalutanga kilichopo Kata ya Kisaki, Said Masongele amesema mzozo huo ulitokea jana saa saba mchana katika eneo la ofisi za serikali ya kijiji.
Masongele amewataja waliofariki dunia kuwa ni Ramadhan Kiwenge na Kibwana Msipwile.
Amesema mkazi mwingine Ismail Msagule amejeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye makalio na amelazwa katika zahanati hiyo.
Mwenyekiti huyo amesema hilo lilitokea baada ya mifugo kuingia shambani kwenye bonde la Kikwato na kukamatwa na mgambo na walinzi wa jadi (Sungusungu).
Amesema awali, viongozi wa kijiji wakiwa kwenye kikao walipata taarifa kwamba kuna mifugo imevamia mashamba, hivyo walitumwa mgambo kwenda kuikamata.
Muda mfupi baadaye amesema alipokea simu ikieleza Mohamed Kassim alijeruhiwa kichwani na mfugaji wakati wa kukamata mifugo.
Mgambo wa kijiji hicho, Kibwana Mbegu aliyeshiriki kukamata mifugo amesema watu hao watatu walifyatuliwa risasi wakati askari akijihami baada ya wananchi kujaribu kupora silaha.
“Tulikamata mifugo isiyopungua 80 katika mashamba ya Kikwato ikila mazao, wakati tukifanya hivyo mwenzetu alijeruhiwa kwa kupigwa fimbo kichwani na mfugaji.  Tuliwazidi nguvu wafugaji na kuswaga  mifugo hadi ofisi za kijiji kwa hatua za kisheria,” amesema Mbegu.
Mbegu amesema baada ya dakika chache, wafugaji walifika ofisi za kijiji wakiwa na silaha za jadi, wakati huo wananchi wakiwa wanakusanyika huku kukiwa na askari polisi mwenye silaha kulinda amani eneo hilo.
Amesema baada ya wafugaji kufika eneo hilo, walianza kuchukua mifugo kwa nguvu jambo lililosababisha askari kufyatua risasi hewani kuwatawanya.
Mbegu amesema baadhi ya wananchi walimfuata askari kwa lengo la kumnyang’anya silaha, huku wengine wakirusha mawe.
Amesema askari alifyatua risasi ili kuwazuia ambazo ziliwapata watu wawili na baadaye alikimbia eneo hilo.
Mgambo huyo amesema kundi la wananchi lilimkimbiza ndipo alipofyatua risasi nyingine iliyomjeruhi mwananchi mwingine kwenye makalio.
Amesema askari huyo alijificha ndani ya nyumba kijijini hapo na alipiga simu kituo cha polisi Kisaki Gomero kuomba msaada kwa wenzake waliomuokoa katika eneo hilo ambalo lilikuwa limezingirwa na wananchi.

Tahadhari ongezeko biashara ya tumbaku nchini

Dar es Salaam. Chama cha Kudhibiti Tumbaku Tanzania (TTCF) kimesema kinasikitishwa na ongezeko la kilimo na biashara ya tumbaku nchini Tanzania.
Mkuruguenzi Mtendaji wa chama hicho Lutgard Kagaruki amesema leo Septemba 19 kwamba kuongezeaka kwa kilimo cha zao hilo kunahatarisha afya za watanzania.
Kagaruki amesema baadhi ya kampuni za tumbaku zimefungua ofisi Tanzania wakati katika nchi nyingine kampuni za aina hiyo zimeshtakiwa kuuza bidhaa za tumbaku ambazo wanajua fika kwamba ni hatari kwa afya.
 “Hizi ni bidhaa ambazo kwa makusudi zinachochewa  zilete utegemezi kwa haraka zaidi,’’ amesema.
“Kampuni nyingine zimeshitakiwa kwa kuwahonga viongozi ndani ya Africa Mashariki hususan Kenya, wasipitishe sheria madhubuti ya kudhibiti matumizi ya tumbaku. Inasikitisha  kuona kampuni kama hizi, zimepokelewa kwa mikono miwili hapa Tanzania,’’ ameongeza Kagaruki
Tanzania iko nyuma ya nchi nyingine za Afrika Mashariki, Afrika na dunia kiujumla katika utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti  Tumbaku (World Health Organisation Framework Convention on Tobacco Control – WHO FCTC).
Mpaka sasa nchi 180, ambazo ni zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wote duniani zimeridhia  Mkataba huu. Tanzania iliridhia Mkataba huu Aprili 2007, hivyo ina wajibu wa kuutekeleza kikamilifu.
“Nchi ambazo zimetekeleza huu Mkataba kikamilifu, magonjwa yanayosababishwa na tumbaku yamepungua  ,’’ amesema.
Magonjwa hayo ni pamoja na saratani, magonjwa ya moyo, kisukari na magonjwa sugu ya kifua – yote yakiwa ni magonjwa yasiyoambukiza. 
Kagaruki amesema  Tanzania ni nchi pekee ndani ya Afrika Mashariki ambayo haina sheria madhubuti ya kudhibiti matumizi ya tumbaku.
“Isitoshe Zanzibar wanayo Sheria na Kanuni madhubuti za kudhibiti Tumbaku zinazoendana na matakwa ya Mkataba,’’ amesema.
 “Tunawaomba viongozi wetu waone na kukubali kuwa tumbaku ni janga la kitaifa na halina faida kwa mkulima wala kwa Taifa, bali faida ni kwa kampuni za tumbaku tu.” amesema
“Hivyo wajiunge na wenzao ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Dunia kwa ujumla, kuongoza mapambano dhidi ya tumbaku, huku wakiwasaidia wakulima kujikita kwenye mazao mbadala na kuwapatia masoko bora na ya uhakika kwa mazao hayo,’’ anasema  Kagaruki.
“Inasikitisha sana kuona hata wale wakulima waliobadilika na kulima mazao mbadala, mazao yao kwa sasa hivi yanakosa masoko, huku hamasa zikiendelea kwa nguvu kutaka kuwarudisha kwenye kilimo cha tumbaku,’’ amesema.
“Tuna shaka kama kweli hizi siyo njama za kampuni ya tumbaku. Ukweli ni kwamba, ongezeko la kilimo na biashara ya tumbaku nchini, litasababisha ongezeko la matumizi ya tumbaku na hivyo ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza,’’ ameongeza.

Majaji kueleza kinaganaga kufutwa matokeo Kenya

Nairobi, Kenya. Mahakama ya Juu kesho inatarajiwa kutoa maelezo kamili kuhusu hukumu ya kihistoria ya kesi ambayo ilisababisha kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Agosti 8.
Wanasheria wa vyama mbalimbali vya siasa walitaarifiwa jana kuhusu kutolewa kwa hukumu nzima kazi itakayoanza saa 4.00 asubuhi. Kutokana na uamuzi wa majaji wengi, mahakama hiyo iliamua kufuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta ikitaja dosari kadhaa na kukosekana uhalali wakati wa kutuma matokeo.
Jaji Mkuu David Maraga, Makamu wake Philomena Mwilu, majaji Smokin Wanjala na Isaac Lenaola walifuta uchaguzi huo Septemba 1 mwaka huu na kuamuru Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuandaa uchaguzi mwingine ndani ya siku 60 kama inavyosema Katiba.
Lakini majaji wawili JB Ojwang na Njoki Ndungu walitupilia mbali kesi hiyo iliyofunguliwa na kiongozi wa muungano wa Nasa, Raila Odinga. Pia na wao watatoa maoni yao kesho.
Tayari IEBC imetangaza Oktoba 17 kuwa siku ya uchaguzi wa marudio lakini sintofahamu imejitokeza kuhusu tarehe hiyo.
Joto limeanza kupanda mitaani kwani leo asubuhi mamia ya wafuasi wa Jubilee waliandamana nje ya Mahakama ya Juu wakiishutumu kwa “kuiba ushindi wao.”
Wakinyanyua mabango na vipeperushi, waandamanaji hao wengi wao vijana walilalamikia majaji waliotoa hukumu hiyo kwamba haikuwa halali.

Kubenea mikononi mwa polisi

Dar es Salaam. Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea yupo mikononi mwa polisi akisubiri mchakato wa kusafirishwa kupelekwa mjini Dodoma kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Jumanne, Kubenea amesema yupo katika kituo cha polisi cha Oysterbay  wilayani Kinondoni na akisubiri utaratibu wa safari ya kwenda Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kama Spika wa Bunge Job Ndugai alivyoagiza.
Kubenea amesema awali kabla ya kushikiliwa alikwenda kujisalimisha polisi katika kituo hicho kisha aliambatana na askari hadi Katika Hospitali ya Aga Khan ambako alitakiwa kwenda kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha MRI.
“Baada ya kipimo kukamilika daktari alishauriwa nipumzike, lakini askari wakaamuru niondoke na kurudi Oysterbay. Hapa ninapozungumza na wewe nipo kituo nikisubiri kusafirishwa kwenda Dodoma,”amesema Kubenea na kuongeza kuwa;
“Hata hivyo, daktari ameshauri nisisafiri kwa njia ya barabara kutokana na matatizo ya mgogo niliyokuwa nayo hivyo nasubiri utaratibu hapa,” amesema mbunge huyo.
Akizungumzia kushirikiliwa kwa Kubenea, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo lilikuwa na hati ya kukamatwa kupelekwa Dodoma kwa mbunge huyo ndiyo maana yupo mikononi mwao.
“Atapelekwa lini, atatoka saa ngapi au atasafirishwa kwa njia gani hilo mimi sijui ila atapelekwa Dodoma chini ulinzi wa polisi. Ukishakuwa na hati ya kukamatwa lazima utakaa mahabusu tu,”amesema Kamanda Mambosasa.
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amesema;“Kwanza sijui kama yupo polisi ndiyo kwanza nakisikia kwako,” alieleza.
Alipotafutwa mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika kujua kama wajumbe wajumbe kamati yake, bado wapo Dodoma baada ya kikao cha Bunge kuhairishwa wiki iliyopita alijibu;
“Shughuli za kamati yangu hazifanyika katika magazeti, sisi tunafanya kimyakimya kisha  tunamkabidhi Spika wa Bunge,” alijibu Mkuchika kisha kukata simu.

Taasisi zakabidhiwa historia ya Tanganyika

Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Kavazi LA

Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Kavazi LA Mwalimu Nyerere Profesa Saida Yahya akipokea nyaraka zenye kumbukumbu ya Tanganyika kutoka kwa Urmila Jhaveri. 
Dar es Salaam. Taasisi tatu leo zimekabidhiwa nyaraka zinazoelezea historia ya Tanganyika sasa Tanzania.
Nyaraka hizo zilizokabidhiwa zinaonyesha  kumbukumbu za matukio yaliyotokea zaidi ya miaka 50 iliyopita zikielezea mapambano ya uhuru yalivyokuwa.
Taasisi zilizopokea nyaraka hizo ni Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Kavazi la Mwalimu Nyerere na National Archives.
Nyaraka  hizo zilikabidhiwa na Urmila Jhaveri mke wa marehemu  Jhaveri  Laxmichand, kiongozi wa kisiasa wa muda mrefu aliyekuwa na jukumu kubwa katika mapambano ya uhuru wa nchi, akishirikiana na Hayati Mwalimu Nyerere.
"Nyaraka hizi na picha zinaendelea kwa undani maendeleo ya kisiasa yalivyokuwa wakati ule na jinsi mume wangu alivyokuwa anachangamana na jamii nyingine," alisema  Urmila.
Naye aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini India Gertrude Mongela wanakati anapokea nyaraka hizo kwa niaba ya mfuko wa Mwalimu Nyerere amesema  anaamini zitakifundisha kizazi kilichopo na kijacho harakati za ukombozi wa nchi hii zilikuwa.
"Ninakubali mchango mkubwa wa mume wake kwa kuzingatia na kuona umuhimu wa kutunza barua, picha na nyaraka mbalimbali zinazohusu Tanganyika-Tanzania," amesema.
“Zinaeleza kuhusu Tanganyika na baadaye Tanzania zina picha na zikiwa katika mfumo wa video, inaonyesha ni kwa jinsi gani familia ya Jhaveri imethamini jambo hili, ”amesema Mongela.
Kwa upande wake, Mboneko Munyanga, aliyezungumza kwa niaba ya  familia ya Mwalimu Nyerere amesema "Tunaamini nyaraka hizi sio tu mchango muhimu kwa taasisi hizi tatu, lakini pia ni muhimu kwa ya historia ya nchi yetu."

Ameongeza "kizazi cha sasa kinakosa kumbukumbu muhimu za nchi hii, kupitia nyaraka hizi kuna jambo jipya watajifunza, "
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Kavazi la Mwalimu Nyerere, Profesa  Saida Yahya amesema licha ya kutunza nyaraka hizo pia wameonyesha uzalendo na umoja.
Alifafanua Tanzania ni nchi isiyokuwa na matabaka na umoja huo ndiyo umezaa matunda ya kupata nyaraka muhimu kama hizo.
Amesema ni vema kizazi cha sasa kikaiga mfano huo kwa kuandika matukio muhimu na kuyatunza kwa ajili ya kizazi kijacho.
Balozi wa Mashariki ya Kati na Kusini mwa Afrika, Matthew Beeki-Uwiafo alimsifia  Urmila kwa kusimamia hati za kihistoria ambazo zilionekana kuwa muhimu katika rekodi ya historia ya nchi, hata baada ya mumewe kufariki mwaka 2004.
Hayati Jhaveri Laxmichand alikuwa kiongozi wa kisiasa hapa nchini na alikuwa miongoni mwa wanaharakati waliokuwa bega kwa bega na wapigania uhuru.
Amefariki nchini India mwaka 2004 baada ya kuugua na kwenda kutafuta matibabu. Mkewe Urmila alilazimika kurudi nchini kwa ajili ya kukabidhi nyaraka mbalimbali

Sunday, September 17

MAJAJI NCHINI WAAGIZWA KUMALIZA MLUNDIKANO WA MASHAURI IFIKAPO DESEMBA 15, 2017

Majaji nchini wameagizwa kumaliza kesi zote za muda mrefu Mahakamani ifikapo Disemba 15, mwaka huu ili kuendana na azma ya Mahakama ya kutoa haki  kwa wote na kwa wakati.
Akizungumza katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali alisema kuwa Kanda zote za Mahakama Kuu nchini tayari zimeshaainisha idadi ya kesi zote za kuanzia miaka miwili kuendelea (kesi za mlundikano) ambazo zitafanyiwa kazi.
“Nawaagiza Majaji wote nchini kuendelea na zoezi la kusikiliza kesi hususani kesi za muda mrefu Mahakamani, na zoezi hili lianze kufanyika Oktoba 16,mwaka huu na kazi hii nataka ikamilike kufikia Desemba 15,mwaka huu,” alisisitiza.
Mhe.Jaji Kiongozi amezitaja Kanda za Mahakama Kuu ambazo zinaonekana kuelemewa na mzigo wa mashauri kuandaa orodha ya mashauri ‘causelist’wanayohitaji kusaidiwa.
Mahakama hizo ni Mahakama Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza, Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, Mahakama Kuu-Kanda ya Mbeya, Mahakama Kuu-Kanda ya Shinyanga, Mahakama Kuu-Divisheni ya Ardhi na Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi.
Aidha Mhe. Wambali ameagiza zoezi hilo lifanyike ndani ya wiki moja kuanzia Jumatatu, Septemba 18 ili kuwezesha kujua uhitaji wa msaada wa Majaji wengine kutoka Kanda nyingine watakaoenda kusaidia kusikiliza na kumaliza mashauri hayo katika maeneo tajwa.
Aidha Mhe. Jaji Kiongozi amewataka Majaji Wafawidhi kuitisha vikao na Wadau wa Mahakama ili waweze kujua juu ya kuwepo kwa Programu maalum ya kusikiliza na kumaliza kesi zote za muda mrefu Mahakamani.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma amewataka Majaji na Watumishi wa Mahakama kwa ujumla kufanya kazi kwa kuzingatia nguzo tatu za Mpango Mkakati wa Mahakama ili kutekeleza majukumu kimkakati na hatimaye kupata matokeo chanya.
“Majaji Wafawidhi ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Mpango Mkakati hususani katika nguzo namba mbili ambayo ni Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati, kupitia Majaji na Mahakimu waliopo chini yao” alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Akiongelea juu ya jukumu kuu la utoaji haki nchini, Mhe. Jaji Mkuu amesisitiza juu ya kuwa na kumbukumbu sahihi ya takwimu za mashauri zilizopo katika Mahakama husika hali ambayo itawezesha kujua ni msaada utakaohitaji, bajeti na kadhalika.
Kwa upande mwingine Mhe. Jaji Mkuu amesisitiza juu ya matumizi ya TEHAMA katika uendeshaji wa kesi ili kuendeana na kasi ya Teknolojia hali ambayo itawezesha huduma ya haki kuwafikia wananchi kwa wakati.
Mambo mengine aliyoyasisitiza Mhe. Jaji Mkuu alipokuwa akifunga Mkutano wa Majaji Wafawidhi ni pamoja na ufanyaji kazi kwa ushirikiano kwa Watumishi wote wa Mahakama na kubadili mtazamo hasi ‘change of attitude’ na kuzingatia maadili katika utendaji kazi.
Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, uliofanyika kwa siku mbili (2), Septemba 15&16 ni mwendelezo wa Vikao mbalimbali ambavyo vimekuwa vikifanyika mara kwa mara vyote vikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa azma ya Mahakama ya Tanzania ya kutoa haki kwa wakati inaonekana kutekelezeka.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa neno alipokuwa akifunga Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa-AICC jijini Arusha, Septemba, 15 na 16, 2017. 
 Sehemu ya Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu nchini wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) 
Waheshimiwa Majaji Wafawidhi pamoja na Wasajili wakiwa katika Mkutano huo uliokamilika Septemba 16, 2017
 Waheshimiwa Majaji Wafawidhi pamoja na Wasajili wakiwa katika Mkutano huo uliokamilika Septemba 16, 2017
 Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania,Mhe. Hussein Kattanga akitoa neno, akisisitiza juu ya ufanyaji kazi kwa malengo.
 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akiongea katika Mkutano wa Majaji Wafawidhi
 Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama,Mhe.Zahra Maruma akitoa mara ya utekelezaji wa kazi mbalimbali za Mradi mbele ya Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania mara baada ya kuhitimisha kikao cha siku mbili cha kujadili juu ya mikakati ya kuondosha mashauri ya muda mrefu Mahakamani. aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, wa kwanza kushotoni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa pia ni Jaji namba moja wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa pili kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi,Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi na wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga.Picha na Habari na Mary Gwera wa Mahakama

BLOGGER TUPOKIGWE ABNERY KUZINDUA KITABU CHA RIWAYA "MAPENZI KABURINI" JIJINI ARUSHA

Tupokigwe Abnery Mwampondele amezaliwa,Seronera - Serengeti mkoani Mara.Alisomea shahada ya Isimu ya lugha ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kwa sasa ni mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule ya Sekondari ya Wasichana Precious blood iliyopo mkoani Arusha-Tanzania. N’je na kazi ya uwalimu Tupokigwe Abnery ni mtunzi wa vitabu vya hadithi, mbunifu wa mavazi ya kiasili, mjasiriamali na mwandishi wa gazeti tando (blogger) inayoitwa Sinyati Blog.

Tupokigwe Abnery alikuwa na kawaida ya kupenda kujibembeleza au kujifariji akiwa anatembea kwa kutengeneza hadithi katika fikra zake ili kuweza kulala au kufika anakoelekea bila kuchoka,ndipo siku moja baada ya kushiriki shindano la uandishi wa Riwaya fupi kwa wanafunzi wa shule ya msingi,sekondari na vyuo vikuu Tanzania kwa ajili ya Tuzo ya mama Salma Kikwete iliyoandaliwa na TASAKI(Tamasha la Sauti ya Kiswahili) aliibuka mshindi wa pili wa riwaya fupi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania.

Hivyo hiki kitabu ni muendelezo wa Riwaya aliyopatia Tuzo.Soma kitabu hiki uweze kujionea ubunifu wa hali ya juu wa fani pamoja na mshikamano wa maudhui uliyopo ndani ya kitabu hiki. 

Mapenzi Kaburini ni kitabu chenye mtazamo yakinifu,ni kitabu ambacho maudhui yake yamezitazama nchi za Afrika Mashariki na changamoto zilizopo katika nchi kwa upande wa viongozi pamoja na wananchi.Kimebeba maudhui yanayowalenga wananchi wote bila kujali utabaka.Kwa upande wa fani kimetumia majina ya halisi na kubuni hasa kwa upande wa maeneo ya miji mfano kuna miji kama Kinyonga,kupe,chatu ambayo ni majina yaliyopo katika nchi ya Simba.Nchi hii ya Simba ni nchi inayosimamia nchi zilizopo Afrika Mashariki.

Mbali na hilo pia visa na matukio vimepewa majina ya hifadhi za Taifa zilizopo katika nchi ya Tanzania.Mfano hifadhi ya Ruaha,Sanane,Manyara na kitulo kama ukisoma kitabu hiki utagundua kuwa sifa ya hifadhi inaendana na visa na matukio yaliyopo katika sehemu hiyo iliyoandikwa kwa jina la hifadhi.Mfano hifadhi ya Kitulo inasifika kwa kuwa na maua,kama tujuavyo maua huashiria sifa nyingi moja wapo hapo ni upendo,watu wengi hutumia maua katika kuwapa wapenzi wao,mfano kuomba msamaha,kumfariji mtu,hata kuonesha upendo kwa mtu unayempenda.

Utakaposoma kitabu hiki utaburudika na kufundishwa baadhi ya mambo kama Kukuza imani yako kwa Mungu,uaminifu katika ndoa,uzalendo katika nchi yako na Madhara ya kujihusisha katika mahusiano na mtu usiye mjua.
Nitakupatia kionjo kidogo katika sura ya kwanza ili kuweza kuona mwanzo tu wa hadithi hii ambayo hutapenda kuacha kuifuatilia:

Sura ya kwanza 

Hifadhi ya Sanane 
Ilikuwa siku ya Jumatatu katika ghorofa la tajiri mmoja, mmiliki wa hoteli maarufu katika nchi ya Simba. Tajiri huyo alifahamika sana kwa kuwa alikuwa akijitolea sana kwa wananchi wasiojiweza, katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.Watu husemamfadhili punda kuliko mwanadamu vilevile tenda wema kisha nenda zako baraka utazipata kwa Mungu,usisubiri hisani za wanadamu.

Pamoja na misaada aliyoitoa kwa watu mbalimbali lakini wananchi wa Simba hawakujali misaada yake, walimteta kila kona kuwa anatumia nguvu za giza na amekwisha toa kafara ndugu, jamaa na hata watoto wake ili kujipatia utajiri mkubwa alionao. Siku hiyo ya Jumatatu katika pagala la tajiri huyo aliyefamika kwa jina la Pesa nyingi.

katika moja ya chumba cha ghorofa hilo kulikuwa na mwanamke mrembo na mzuri sana wa sura, mrefu mithili ya twiga, mwenye umbo zuri la kiafrika, chini alikuwa amevaa suruali ya chupa huku akiwa amevaa blauzi tatu juu zenye rangi tofauti na nywele timutimu zikiwa zime nakishiwa na vitu vya jaani kama vichana,visude, rasta chakavu na kufungwa kitambaa cha kitenge aina ya makenzi ,uso wake ulikuwa kama paka mwenye madoa kutokana na kujipamba kwa majivu na masizi ya mkaa wa jaani. Pembeni ya ua hilo alikuwepo mnyama mwenye maringo 

mbugani kuliko wote, sio mwingine bali ni kijana mtanashati aliyekwenda hewaani, rangi ya ngozi yake nyeusi ya kung’aa. Tabasamu la mwanaume huyo lililokuwa likimfariji mtoto mzuri, lili mvutia sana Savannah. Ghafla ilisikika sauti ya mwanamke huyo ikiita kwa sauti ya chini iliyojaaa simanzi na mateso ya muda mrefu,ilisema “John naumia mume wangu, hali yangu kila kukicha afadhali ya jana”. 

John alijibu “usijali Savannah nipo hapa mke wangu kwa ajili yako utapona tu tutakwenda hospitali,subiri nikuandalie chakula ule, kisha nikupeleke hospitali malikia wangu”. Basi baada ya John kumfariji Savannah aliamka na kuelekea jikoni pembeni ya sehemu aliyokuwa amelala mpenzi wake. 

Watu hawa walipendana sana ni vile tu hali yao haikuwa nzuri kifedha waliishi kwa kuhangaika, kuomba msaada na wakati mwingine walifukuzwa na walimwengu pale walipokuwa wakiomba msaada, watu waliwapita kama mbwa waliokosa matunzo. 

Wapenzi hao Walizoea maisha ya kuokota vyakula jalalani na kukimbilia magari ya taka sambamba na kusubiria mabaki ya chakula katika migahawa mbalimbali. Wakati huo John alikuwa akitimiza ahadi aliyo mhahidi malikia wake alimuandalia chakula walicho kiokota katika soko kuu la mji huo wa Chatu. John alimuinua Savannah pale alipokuwa amelala kwenye kanga chakavu akiwa amejifunika magunia yalionekana ni ya mpunga. John alimlisha Savannah chakula kile ambacho hawakujua kilipikwa lini na kutupwa na nani na lini. Savannah alisikika akisema “asante mume wangu hata 

mwanangu anafurahi sasa naona napata nafuu, nahisi ni njaa ilikuwa inaniuma”. Mwanangu nisamehe mama kakushindisha njaa, nakupenda sana najua wewe utakuwa mrembo zaidi yangu mwanangu hata baba yako anakupenda”. John alikuwa anapenda sana utani alicheka na kusema “atakuwa mrembo kama wewe kweli mke wangu lakini rangi ya ngozi yake itakuwa kama yangu, yako iko kama ya nguruwe hahahaaaa!” Savannah alikuwa mweupe kama Nguruwe, ingawa alivyokuwa anaonekana ni kama mtu mwenye ngozi ya rangi ya maji ya kunde kutokana na ugumu wa maisha. 

Wawili hao walifurahi pamoja na kusahau shida walizokuwa nazo.Walipomaliza kula wapenzi hao waliamua kutoka nje baada ya kukaa ndani ya paghala hilo kwa muda wa wiki moja, Dikidiki hao walikuwa na kaida ya kufanya hivyo wanapotafuta riziki na kujilimbikizia ndani ya paghala lao kisha wana kaa kwa muda huo bila kutoka. Usilolijua ni kama usiku wa kiza, basi Savannah na John walipotoka wakiwa n’je ya mgahawa mmoja uliokuwa unapendwa sana na wananchi wa mji huo wa Chatu zilisikika sauti za wanawake wakisema: 

“haya jamani sasa ni ule wakati wa Pesa nyingi kuingiza hela sasa wenzi wametoka fungate”. Waliamini kuwa Pesa nyingi alikuwa anawatumia Dikidiki hao kama misukule inayotoka na kurudi ndani na wanapotoka basi mzee Pesa nyingi huingiza hela nyingi sana. Kwakuwa wenzi hao walikuwa hawaelewi kinachoongelewa waliendelea kuomba msaada kwa wateja waliokuwepo hapo mgahawani. Wanapokosa waliamua kucheza baadhi ya nyimbo zilizokuwa 

zikipigwa katika mgahawa huo, wakicheza hupewa chakula na fedha ambazo hutoka katika mifuko ya wateja. John alikuwa anapenda sana kucheza,wakiwa wamekaa chini walisikia wimbo wa mwanamuziki maarufu Tanzania Diamond unaosema Je, Utanipendaga? John alimuinua Savannah aliyeonekana kachoka na mimba yake. Savannah aliamka na kucheza na mpenzi wake ,walicheza kwa miondoko ya kihindi, machozi yalisafisha uso wa Savannah huku yakiosha kifua cha John kilichokuwa kimejaa kama mlima na mikono iliyokuwa na miinuko ya kupanda na kushuka ilizunguka juu ya kifua cha Savannah na kumfanya ahisi kazungukwa na jeshi kubwa la malaika wa ulinzi.

Baada ya kumaliza kucheza savannah alikuwa amechoka sana, kitendo cha kucheza kilimsababishia kuchokoza maumivu na kupelekea kupata uchungu katika kizazi chake. Baada ya kuona hivyo John aliinama na kuchukua zawadi walizozipata kutoka kwa hadhira iliyokuwa ikiwatazama huku baadhi ya hadhira wakibubujikwa na machozi walimpelekea hela na chakula John katika kapu lake la kukusanyia riziki. Watu waliokuwa wakiwatazama Savannah na John hawakujali maumivu ya mwanamke yule na kuona kawaida. 

Wapo waliosikika wakisema hawa vichaa wana akili, wengine walisema hawa si vichaa, vichaa gani wana akili ya kutafuta hela hivi, wamekusanya umati mkubwa hivi na kuwafanya watu kutoa kile walichonacho. Mama mmoja mwenye busara anayeuza katika mgahawa huo aliyefahamika kwa jina la mama ndaga akasema“Jamani mimi nawafahamu hawa vichaa kwanza hawakuwa wakitembea hivi pamoja kama Dikidiki, huyo kaka unayemuona alikuwa..........pata mwendelezo kwa kujipatia kitabu hiki.

NKAMIA APINGWA KUSUDIO LA KUONGEZA UKOMO WA BUNGE

NA AZIZA MASOUD – DAR ES SALAAM
KITENDO cha Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), kuwasilisha kusudio la kutaka kuwasilisha muswada binafsi wa mabadiliko ya Katiba bungeni ili kuongeza ukomo wa Bunge, kimepingwa vikali na baadhi ya wasomi na wanasiasa, huku baadhi yao wakidai huenda akawa anatafuta umaarufu.
Nkamia aliwasilisha kusudio hilo ofisi za Bunge kwa mujibu wa kanuni ya 81(2) ya kanuni za Bunge toleo la 2016.
Katika barua yake aliyoisaini Septemba 12, mwaka huu na kuwasilishwa ofisi ya Katibu wa Bunge Dodoma, ameeleza kusudio lake la kuwasilisha muswada huo aliouita Muswada Binafsi wa Sheria ya Mabadiliko ya 15 ya Katiba.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, Mhadhiri wa Masuala ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema pamoja na kwamba ni mawazo binafsi, lakini anapaswa kutoa sababu za msingi za marekebisho hayo yatakayokuwa kinyume na Katiba iliyopo.
“Lazima tuangalie mawazo haya kayatoa kwa muktadha gani, huenda ana lengo la kujitafutia umaarufu ili na yeye aonekane kaingiza agenda fulani katika jamii, huyu mtu aliwahi kuwa naibu waziri, isije ikawa anabembeleza nafasi ya uwaziri,” alisema Dk. Bana.
Alisema sababu zinazofanya kuwe na uongozi wa miaka mitano zilizotolewa na Watanzania bado zipo hai, hivyo kama angekuwa muungwana angepeleka hoja ya nafasi ya ubunge kutozidi miaka 10.
Pia alisema Nkamia alipaswa ajitafakari kabla ya kuwasilisha kusudio hilo kwa kuwa hoja ya kuongeza muda wa urais ilishakataliwa na Rais Dk. John Magufuli, hivyo asitafute sababu ya kuibadili.
“Maoni yake hayaakisi uhalisia hata kidogo, Watanzania tuna Katiba na bado haijabadilika, asitake ajiwekee mazingira ya kuonekana anampigia chapuo rais,” alisema Dk. Bana.
Naye mchambuzi wa masuala ya siasa, Profesa Mwesiga Baregu, alisema kauli ya Nkamia inaonyesha nchi ilivyo na wanasiasa waroho wa madaraka.
“Hizi ni kauli za wagonjwa na walevi wa madaraka, hilo suala lipo ndani ya Katiba, sasa labda kama atakuwa na sababu ya msingi ya kuhitaji mabadiliko hayo atuambie, lakini mimi sijaridhika, sioni  kama kuna sababu,” alisema Baregu.
Alisema masuala ya ukomo wa Bunge yalishazungumziwa katika Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba mpya, kwamba ukomo wa rais ulipaswa kuwa vipindi viwili wakati Bunge vipindi vitatu.
Profesa Baregu alisema misingi ya demokrasia ni kuchochea mawazo mapya na maoni tofauti, lakini suala la ukomo wa umri na mihula ni ugonjwa katika nchi za Afrika.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni wakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari, alisema kitendo cha Nkamia kutoa kauli hiyo katika nchi za demokrasia kama Tanzania, kinamfanya kumwona wa ajabu.
“Namwona ni mtu wa ajabu, nchi zote zenye demokrasia kama Uingereza na Marekani, wana awamu nne za urais, lengo ni kumfanya kiongozi asibweteke.
“Mawazo aliyoyatoa ni uhuni wa kutaka kuwa masultani na hii si kauli yake, lazima kuna mtu atakuwa amemtuma,” alisema Profesa Safari.
Alisema Tanzania haiwezi kuiga mfano wa Rwanda kwa kuwa nchi hiyo inaendeshwa kinyume na sheria za kimataifa.
Naye Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Charles Rwechungura, alisema Nkamia anaweza kufanikisha suala hilo endapo atakuwa na sababu za msingi.
“Mimi nadhani tuone kwanza sababu zake za kutaka mabadiliko, labda ana sababu za msingi, lakini pia akiweza kuwashawishi wabunge basi sisi wananchi hatutakuwa na jinsi,” alisema.
Kwa upande wake, Nkamia, alishangazwa na kitendo cha nyaraka hiyo aliyoita ya siri kusambaa katika mitandao ya kijamii na alikiri kuwasilisha kusudio hilo na kusisitiza kuwa ataweka wazi sababu za kufanya hivyo muda utakapofika.
“Ni kweli nimewasilisha kusudio hilo na nitatoa sababu muda utakapofika, lakini mmenishangaza hiyo nyaraka ni ya siri na bado ilikuwa katika ngazi ya kiofisi, sijui imefikaje uko kwenu,” alisema Nkamia.