Tuesday, August 1

MAONYESHO YA WAZI YA FILAMU FUPI


ALIYEIPAISHA TUSIIME KITAIFA ATAMANI PHD


MWANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya Tusiime, Rashid Abdalah, aliyeshika nafasi ya tatu kitaifa kwa masomo ya biashara amesema nia yake ni kusoma hadi ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD).

Akizungumza leo shuleni hapo Rashid amesema ndoto yake ya miaka mingi ni kuwa mkaguzi wa hesabu hivyo amenuia kusoma kwa bidii hadi afikie ngazi hiyo.

“Naamini nitafikia malengo yangu kwa kuwa najua siri ya kufika huko ni juhudi, kujitambua  na kuwasikiliza walimu, hakuna kingine zaidi ya kuwa makini na masomo na kuwa makini,” alisema Rashid ambaye alianzia kidato cha pili shuleni hapo mwaka 2012.

Amesema juhudi za walimu katika kufuatilia maendeleo ya wanafunzi na mazingira mazuri ya shule, ushirikiano mzuri na wanafunzi wenzake ni baadhi ya mambo ambayo yamekuwa chachu ya mafanikio yake.

Aidha amewaasa wanafunzi waliobaki shuleni hapo kujitambua wamefuata nini shuleni na kufuatilia kila wanachofundishwa na walimu wao ili mwisho wa siku wapate mafanikio kama yake.

“Kufaulu haiwezi kuwa muujiza ni juhudi tu na kusikiliza mafundisho na maelekezo ya walimu, lazima mtambue kuwa walimu wanataka mfaulu hivyo mkiwasikiliza na kuwafuata mtafaulu kwa viwango vya juu sana,” amesema Rashid alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kidato cha tano shuleni hapo.

Mkuu wa shule hiyo, Emil Rugambwa, amesema mafanikio ya shule hiyo kwenye matokeo ya kidato cha sita ni mwendelezo wa mafanikio kwenye matokeo ya kitaifa ambayo shule imekuwa ikiyapata kuanzia yale ya darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili na cha nne.

Kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, Tusiime imefanikiwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) hivi karibuni kwa kufaulisha wanafunzi wote 518.

Mwanafunzi bora nafasi ya tatu kitaifa katika masomo ya biashara wa shule ya Tusiime, Rashid  Abdalah aliyevaa flana, akifurahia na kupongezwa na wanafunzi wa kidato cha tano wa shule hiyo alipokwenda kuwatembelea na kuwadokeza siri ya mafanikio yake.

DKT. ALBINA CHUWA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU UNAOENDELEA MKOANI DODOMA


 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina  Chuwa (wa pili kulia) akizungumza na mmoja wa mafundi wanaojenga Jengo Jipya la Makao Makuu ya ofisi hiyo mkoani Dodoma wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Wa kwanza kushoto ni Mhandisi John Ainainyi Njau kutoka Benki ya Dunia - Tanzania.
 Muonekano wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.
 Baadhi ya mafundi wakiwa wanaendelea na kazi ya ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linalojengwa mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa waandamizi  wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya ofisi hiyo mkoani Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

DKT. HARRISON MWAKYEMBE AWAAHIDI BFT KUWATATULIA KERO YA ENEO LA MAFUNZO


Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaana Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) kuwatatulia kero ya eneo la kufanyia mafunzo pamoja na ofisi ambalo limekuwa likiwakabili kwa muda mrefu zikiwemo na changamoto nyingine za Shirikisho hilo.

Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa shirikisho hilo ikiwa ni sehemu ya kutambua utendaji kazi wao na changamoto zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa.

Dkt. Mwakyembe amesema kwamba, kutokana na tatizo la ukosefu wa eneo rasmi la ofisi na sehemu ya kufanyia mafunzo, yeye atawasiliana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ili kuona namna gani wanaweza kupata eneo kwa ajili ya kulisaidia shirikisho hilo kwa ajili ya kujenga ofisi na eneo la kufanyia mazoezi.

Sambamba na hilo, ameupongeza uongozi wa shirikisho hilo kwa kazi wanazozifanya na kuwataka wazidi kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hususani katika kupeana taarifa zinazohusu maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini.

“BFT jitahidini muwe na ushirikiano wa karibu na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na msifanye mambo yenu kimya kimya, muwasiliane kwa karibu na BMT kwani hii itasaidia Wizara kushughulikia kero zenu mbalimbali kuliko mkichelewa kutoa taarifa mapema”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, amewahakikishia kuwa, yupo tayari kutafuta wafadhili ndani na nje ya nchi ili waweze kulisaidia shirikisho hilo kutatua kero za uhaba wa vifaa, rasilimali fedha pamoja na ukosefu wa mafunzo kwa makocha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo amelitaka shirikisho hilo kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali ikiwemo kujenga tabia ya ulipaji kodi, kuwaelimisha Wanamasumbwi kuachana na tabia chafu wanapokuwa michezoni pamoja na kuachana na kujihusisha na madawa ya kulevya.

Kwa upande wao Viongozi wanaounda shirikisho hilo pamoja na wajumbe kwa pamoja wamemuahidi Waziri Mwakyembe na Wizara kwa ujumla kuzingatia masuala mbalimbali ikiwemo kuboresha suala la mawasiliano kati ya Shirikisho na Wizara, kufuatilia suala la mikataba mbalimbali na uwajibikaji yakinifu.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akionyesha Jarida la Mpango Mkakati la Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) mara baada ya kufanya nao mazungumzo katika Ofisi za Wizara 01 Agosti, 2017 Jijini Dar es Salaam.

MANISPAA YA KINONDONI YAKABIDHIWA SHULE YA SEKONDARI MAENDELEO




Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamin Sitta akizungumza na watumishi wa serikali na wanafunzi mapema jana katika hafla ya kupokea msaada wa shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Good Neighbour ambao ndio wadhamini wa shule hiyo,Namun Heo akizungunza na watumishi wa serikali katika hafla ya kukabidhi majengo ya shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors,jijini Dar es Salaam. 
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamin Sitta (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Good Neighbour,Namun Heo (kulia) wakisani hati ya makabidhiano ya shule ya sekondari ya Maendeleo iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors,mapema jana jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamin Sitta (wa kwanza kushoto) akiwa ameambata na watumishi wa serikali wakikagua moja ya majengo ya shule hiyo. 

Muonekano wa shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors jana jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

KESI YA WEMA SEPETU KUSIKILIZWA MCHANA HUU MAHAKAMA YA KISUTU

 Msanii wa filamu nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, akitoka mahakamani baada ya kesi yake kuahirishwa hadi saa Sita na nusu mchana, ambapo mkemia atakuja kutoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili yeye pamoja na wafanyakazi wake wawili.

JAFO APONGEZA MSHIKAMANO WA VIONGOZI NA WATENDAJI RORYA


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Rorya kwa mahusiano mazuri waliyonayo katika kuwaletea wananchi maendeleo. 
Jafo alitoa sifa hizo alipokuwa wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na watumishi .

Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, na vyoo kwa sekondari ya Nyamtinga na Nyamunga ambapo majengo hayo yamebainika kujengwa kwa ubora wa kuridhisha. 

Ujenzi wa miundombinu hiyo imegharimu zaidi ya sh.milioni 500 kutoka serikali kuu kwa lengo la kuboresha elimu hapa nchini
Kwa upande wake,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Agness Marwa amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kufika wilayani Rorya na kwamba amekuwa Waziri pekee aliyefanikiwa kutembelea wilayani humo katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano. 


Mbunge huyo ameishukuru serikali kwa upendo wake wa kuisaidia wilaya hiyo miradi ya maendeleo. Naibu Waziri Jafo leo amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku sita ya kukagua miradi ya maendeleo na kuongea na watumishi kwa mkoa wa Kagera na Mara na anaendelea na ziara yake katika mikoa mingine.

.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikata utepe na kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Nyamtinga wilayani Rorya. 
Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyokaguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Mbunge wa Vitimaalum Agnes Marwa akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Rorya na kuwapongeza kwa ujenzi wa madarasa na mabweni. 

WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAENDELEA NA MAFUNZO KUHUSU UDHIBITI WA VIASHIRIA HATARISHI KATIKA UTENDAJI WA VYUO MKOANI MOROGORO


Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Mwenyekiti wa Mafunzo Bw. Paschal Mahinyila akiwakaribisha washiriki katika mafunzo Wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti mkoani Morogoro leo tarehe 01.08.2017. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike (kushoto) akifafanua umuhimu wa uadilifu kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii(hawapo pichani) katika utendaji kazi wa vyuo wakati wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Uendeshaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani(kulia) akifafanua mambo mbalimbali ya kiutawala kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo.
Mhasibu Mkuu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Fatuma Oloo(kulia) akisisitiza jambo kuhusu udhibiti wa fedha kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi Martha Chuma (katikati) akifafanua mambo mbalimbali yahusuyo ugavi na manunuzi kwa wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bi. Vickness Mayao(kulia) akitoa maelekezo kuhusu mikataba na masuala mbalimbali ya kisheria kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkaguzi wa ndani kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Elightness Mchome(katikati) akifafanua umuhimu wa kuepuka hoja za ukaguzi kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayoendelea katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bw. Salim Mgalla(kulia) akiuliza swali kwa wawezeshaji katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro
Baadhi ya wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii Nchini wakifuatilia wawasilishaji mada(hawapo pichani) katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mratibu wa Usimamizi wa Viashiria Hatarishi Bw. Moris Jackson akifafanua masuala mbalimbali yahusuyo Viashiria Hatarishi kwa wakuu wa vyuo vya maendeleo ya Jamii Nchini katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Kaimu Mkuu wa Chuo (Utawala, Mipango na Fedha) Kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha Bi.Nadhaherieth Mshighath akiuliza swali kwa wawasilishaji mada (hawapo pichani) katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Watendaji kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na washiriki kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 01.08.2017. 

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI PIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI WATANO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Benedict Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba akila kiapo cha uadilifu kwa Viongozi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn mara baada  ya kumaliza mazungumzo pamoja na kupokea Hati za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn katikati akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vatican hapa nchini Mhashamu Askofu Mkuu Marek Solcynski, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akimshukuru Balozi wa Vatican hapa nchini Mhashamu Askofu Mkuu Marek Solcynski mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kukabidhi Hati zake Utambulisho.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter akijitambulisha kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter mara baada ya kupokea hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Tumisiime Kabonero Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipiga ngoma ya Brass Bendi ya Jeshi la Polisi ambayo ilifika Ikulu kwa ajili ya mapokezi ya Mabalozi mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Brass Bendi ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU