Image captionRais Nkurunziza alichukua madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.
Burundi limekuwa taifa la kwanza mwanachama wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa jinai kujiondoa katika mahakama hiyo.
Serikali ya taifa hilo la Afrika ya kati liliuarifu Umoja wa Mataifa UN kuhusu hatua hiyo mwaka mmmoja uliopita , na hii leo kujitoa kwao kunaanza kuidhinishwa rasmi.
Inaonekana kama kipimo cha jamii ya kimataifa kuhusu haki.
Ni hatua sio ya kawaida.
Je kutakuwa na athari zake na ni kwa nini ni muhimu?.
Kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan kujiondoa kwa Burundi ni majuto makubwa.
Mahakama ya ICC imeanza kutathmini iwapo inaweza kuchunguza ghasia za kisiasa zilizoibuka baada ya rais Nkurunziza kuchukuwa madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.
Image captionMakao makuu ya mahakama ya ICC mjini Hague
ICC bado ina uwezo kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo.
Lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote wa siku zijazo.
Hatua hiyo inaweza kuwa mfano na kuonyesha viongozi wengine kwamba kujiondoa katika mahakama hiyo ni njia mojawapo ya kuepuka jicho la kimataifa hadi pale Jamii ya kimataifa itakapochukua hatua na taasisi kama vile Umoja wa Afrika ama baraza la usalama la umoja wa mataifa litakapowafuatilia washukiwa na kuyakumbusha mataifa kwamba kujiondoa katika ICC hakumaanishi moja kwa moja kwamba waathiriwa hawatopata haki.
Image captionPacha walioshikana kichwani Jaga na Kalia
Madaktari wa upasuaiji katika mji mkuu wa India Delhi wamefanikiwa kuwatenganisha wavulana pacha waliokuwa wameshikana katika kichwa.
Wavulana hao wa miaka miwili Jaga na Kalia walifanyiwa upasuaji uliochukua takriban saa 16 na sasa wako katika chumba wagonjwa mahututi ICU, kulingana na madaktari.
Kundi la madaktari 30 walifanya upasuaji huo katika taasisi ya matibabu na sayansi ya All India.
Wavulana hao walizaliwa wakiwa na wanatumia mishipa ya damu ya pamoja mbali na tishu za ubongo, hali isio ya kawaida ambayo hutokea mara moja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa.
Pacha walioshikana watenganishwa hospitali ya Kenyatta
Mkurugenzi wa hospitali hiyo Randeep Guleria aliambia vyombo vya habari vya India kwamba siku 18 zijazo zitakuwa muhimu ili kuthibitisha ufanisi wa uchaguzi huo.
Image captionPacha walioshikana katika kichwa watengenishwa India
Pacha hao wanaotoka katika kijiji cha mashariki cha jimbo la Orissa walikuwa wameshikana katika kichwa, hali inayoitwa 'craniopagus'.
Ni miaka 20 tangu mtu aendeshe gari lenye kasi kubwa duniani katika jangwa la Nevada huko Marekani na kuandisha mwendo wa kilomita 1,227 kwa sasa.
Haki miliki ya pichaBLOODHOUND SSC/STEFAN MARJORAMImage captionBloodhound SSC
Gari hilo jipya limenufaika na teknolojia iliyoboreshwa kwa miongo miwili na litasaidiwa na injini ya ndege ya vita ya Eurofighter-Typhoon ambayo inatumia teknolojia ya roketi.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionHatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mizururu ya mazoiezi ya kijeshi.
Korea Kaskazini inasema kuwa itaiachilia meli ya uvuvi ya Korea Kusini ilioikamata siku sita zilizopita kwa kuingia katika himaya yake kinyume cha sheria, chombo cha habari kimesema.
Meli hiyo na wafanyikazi wake itaachiliwa katika mpaka wa kijeshi katika bahari ya mashariki kulingana na chombo cha habari cha KCNA.
Uamuzi huo ulitolewa baada ya wafanyikazi hao kuomba msamaha kwa kufanya makosa hayo, kiliongezea.
Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mizururu ya mazoiezi ya kijeshi.
Korea Kaskazini imesema kuachiliwa kwa meli hiyo ya uvuvi, baadaye siku ya Ijumaa inafuatia hatua ya kukiri makosa kwa wale waliokuwa wakiabiri chombo hicho ambao walitaka serikali ya Korea Kaskazini kuwavumilia.
Uchunguzi, kulingana na Korea Kaskazini, ulithibitisha kuwa wavuvi hao waliingia maji ya taifa lake siku ya Jumamosi.
Msemaji wa serikali ya Korea Kusini alisema ni afueni kwamba wavuvi hao watarudi kulingana na chombo cha habari cha reuters.
Rais wa Tanzania John Magufuli amemteua aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP - Mstaafu) Ernest Mangu kuwa balozi.
Bw Mangu pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye sasa amefanywa kuwa balozi Dkt. Aziz Mlima watapangiwa vituo vya kazi baada ya taratibu kukamilika.
Dkt Magufuli amefanya uteuzi huo alipokuwa anafanyia mabadiliko makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu katika serikali yake.
Kwenye mabadiliko hayo, amewateua Makatibu Wakuu wapya wane na Naibu Makatibu Wakuu wapya sana.
Magufuli pia amewateua wakuu wapya wa mikoa.
Dkt Magufuli amefanya mabadiliko hayo wiki tatu hivi baada ya kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri.
Orodha ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo;
1.Ofisi ya Rais Ikulu.
•Katibu Mkuu - Bw. Alphayo Kidata
2.Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
•Katibu Mkuu (Utumishi)- Laurian Ndumbaro
•Naibu Katibu Mkuu - Dorothy Mwaluko
3.Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
•Katibu Mkuu - Mhandisi Mussa Iyombe
•Naibu Katibu Mkuu(Afya) - Dkt. Zainabu Chaula
•Naibu Katibu Mkuu(Elimu) - Bw. Tixon Nzunda
4.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
•Katibu Mkuu - Mhandisi Joseph Kizito Malongo
•Naibu Katibu Mkuu - Bi. Butamo Kasuka Phillipo
5.Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
•Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) - Bw. Erick Shitindi
•Katibu Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) - Maimuna Tarishi
•Katibu Mkuu (Sera na Uratibu)- Prof. Faustine Kamuzora
6.Wizara ya Kilimo.
•Katibu Mkuu- Mhandisi Methew Mtigumwe
•Naibu Katibu Mkuu- Dkt. Thomas Didimu Kashililah
7.Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
•Katibu Mkuu (Mifugo)- Dkt. Maria Mashingo
•Katibu Mkuu (Uvuvi)- Dkt. Yohana Budeba
8.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
•Katibu Mkuu (Ujenzi)- Mhandisi Joseph Nyamuhanga
•Katibu Mkuu (Uchukuzi)- Dkt. Leonard Chamriho
•Katibu Mkuu (Mawasiliano) - Dkt. Maria Sassabo
•Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) - Mhandisi Anjelina Madete
9.Wizara ya Fedha na Mipango.
•Katibu Mkuu- Doto James Mgosha
•Naibu Katibu Mkuu (Utawala)- Bi. Suzan Mkapa
•Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) - Bi. Amina Shaaban
•Naibu Katibu Mkuu (Sera)- Khatibu Kazungu
10.Wizara ya Nishati.
•Katibu Mkuu - Dkt. Hamis Mwinyimvua
11.Wizara ya Madini.
•Katibu Mkuu- Prof. Simon S. Msanjila
12.Wizara ya Katiba na Sheria.
•Katibu Mkuu- Prof. Sifuni Mchome
•Naibu Katibu Mkuu- Amon Mpanju
13.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
•Katibu Mkuu - Prof. Adolf F. Mkenda
•Naibu Katibu Mkuu - Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi
14.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
•Katibu Mkuu- Dkt. Florence Turuka
•Naibu Katibu Mkuu- Bi. Immaculate Peter Ngwale
15.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
•Katibu Mkuu- Meja Jen. Projest A. Rwegasira
•Naibu Katibu Mkuu - Balozi Hassan Simba Yahaya
16.Wizara ya Maliasili na Utalii.
•Katibu Mkuu - Meja Jen. Gaudence S. Milanzi
•Naibu Katibu Mkuu- Dkt. Aloyce K. Nzuki
17.Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
•Katibu Mkuu - Dorothy Mwanyika
•Naibu Katibu Mkuu- Dkt. Moses M. Kusiluka
18.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
•Katibu Mkuu- Prof. Elisante Ole Gabriel
•Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) - Ludovick J. Nduhiye
•Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) - Prof. Joseph Buchwaishaija
19.Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
•Katibu Mkuu- Dkt. Leonard Akwilapo
•Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Ave-Maria Semakafu
20.Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
•Katibu Mkuu (Afya)- Dkt. Mpoki Ulisubisya
•Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) - Bi. Sihaba Nkinga.
21.Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
•Katibu Mkuu- Bi. Suzan Paul Mlawi
•Naibu Katibu Mkuu- Nicholaus B. William
22.Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
•Katibu Mkuu - Prof. Kitila Mkumbo
•Naibu Katibu Mkuu- Mhandisi Emmanuel Kalobelo
Rais Magufuli amewapandisha vyeo Wakuu wa Wilaya watatu na kuwateua kuwa Wakuu wa Mikoa kujaza nafasi za Wakuu wa Mikoa waliostaafu.
Wakuu wapya wa mikoa
Bw Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Joel Bendera ambaye amestaafu.
Bw Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa nafasi ya Kamishna wa Polisi Zelote Stephen ambaye amestaafu.
Bw Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita nafasi ya Meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.
Bw Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, nafasi ya Dkt. Charles Mlingwa.
Bi Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, nafasi ya Bw. Jordan Rugimbana.
Bw Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, nafasi ya Bi. Halima Dendego.
Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo.
Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kinga (kondomu) ili kujikinga na magonjwa ya zinaa ambayo yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa. Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa.
Chintinka alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia kondomu.
“Jamani hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi” alisema Chintinka
Chintinka alisema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya kinga
“Naombeni tuwakinge hawa watoto wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto wengine maana bila hivyo tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema Chintinka
Aidha Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za lishe.
“Jamani walimu fungu la lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni walimu mjitokeze ili mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi ndio tunaotenga naombeni fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao hawajafika hapa” alisema Chintinka
Chintinka aliwataka watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha tabia hiyo mara moja ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze kujitokeza na wapate lishe iliyotengwa na wilaya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.
"Kwa kweli mgeni rasmi umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri nje kitu kinachowafanya walimu waathirika kujificha na maradhi yao” alisema Mgongolwa
Naye Katibu wa Chama cha Walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.