Rais wa Tanzania John Magufuli amemteua aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP - Mstaafu) Ernest Mangu kuwa balozi.
Bw Mangu pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye sasa amefanywa kuwa balozi Dkt. Aziz Mlima watapangiwa vituo vya kazi baada ya taratibu kukamilika.
Dkt Magufuli amefanya uteuzi huo alipokuwa anafanyia mabadiliko makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu katika serikali yake.
Kwenye mabadiliko hayo, amewateua Makatibu Wakuu wapya wane na Naibu Makatibu Wakuu wapya sana.
Magufuli pia amewateua wakuu wapya wa mikoa.
Dkt Magufuli amefanya mabadiliko hayo wiki tatu hivi baada ya kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri.
Orodha ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo;
1.Ofisi ya Rais Ikulu.
•Katibu Mkuu - Bw. Alphayo Kidata
2.Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
•Katibu Mkuu (Utumishi)- Laurian Ndumbaro
•Naibu Katibu Mkuu - Dorothy Mwaluko
3.Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
•Katibu Mkuu - Mhandisi Mussa Iyombe
•Naibu Katibu Mkuu(Afya) - Dkt. Zainabu Chaula
•Naibu Katibu Mkuu(Elimu) - Bw. Tixon Nzunda
4.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
•Katibu Mkuu - Mhandisi Joseph Kizito Malongo
•Naibu Katibu Mkuu - Bi. Butamo Kasuka Phillipo
5.Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
•Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) - Bw. Erick Shitindi
•Katibu Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) - Maimuna Tarishi
•Katibu Mkuu (Sera na Uratibu)- Prof. Faustine Kamuzora
6.Wizara ya Kilimo.
•Katibu Mkuu- Mhandisi Methew Mtigumwe
•Naibu Katibu Mkuu- Dkt. Thomas Didimu Kashililah
7.Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
•Katibu Mkuu (Mifugo)- Dkt. Maria Mashingo
•Katibu Mkuu (Uvuvi)- Dkt. Yohana Budeba
8.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
•Katibu Mkuu (Ujenzi)- Mhandisi Joseph Nyamuhanga
•Katibu Mkuu (Uchukuzi)- Dkt. Leonard Chamriho
•Katibu Mkuu (Mawasiliano) - Dkt. Maria Sassabo
•Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) - Mhandisi Anjelina Madete
9.Wizara ya Fedha na Mipango.
•Katibu Mkuu- Doto James Mgosha
•Naibu Katibu Mkuu (Utawala)- Bi. Suzan Mkapa
•Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) - Bi. Amina Shaaban
•Naibu Katibu Mkuu (Sera)- Khatibu Kazungu
10.Wizara ya Nishati.
•Katibu Mkuu - Dkt. Hamis Mwinyimvua
11.Wizara ya Madini.
•Katibu Mkuu- Prof. Simon S. Msanjila
12.Wizara ya Katiba na Sheria.
•Katibu Mkuu- Prof. Sifuni Mchome
•Naibu Katibu Mkuu- Amon Mpanju
13.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
•Katibu Mkuu - Prof. Adolf F. Mkenda
•Naibu Katibu Mkuu - Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi
14.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
•Katibu Mkuu- Dkt. Florence Turuka
•Naibu Katibu Mkuu- Bi. Immaculate Peter Ngwale
15.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
•Katibu Mkuu- Meja Jen. Projest A. Rwegasira
•Naibu Katibu Mkuu - Balozi Hassan Simba Yahaya
16.Wizara ya Maliasili na Utalii.
•Katibu Mkuu - Meja Jen. Gaudence S. Milanzi
•Naibu Katibu Mkuu- Dkt. Aloyce K. Nzuki
17.Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
•Katibu Mkuu - Dorothy Mwanyika
•Naibu Katibu Mkuu- Dkt. Moses M. Kusiluka
18.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
•Katibu Mkuu- Prof. Elisante Ole Gabriel
•Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) - Ludovick J. Nduhiye
•Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) - Prof. Joseph Buchwaishaija
19.Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
•Katibu Mkuu- Dkt. Leonard Akwilapo
•Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Ave-Maria Semakafu
20.Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
•Katibu Mkuu (Afya)- Dkt. Mpoki Ulisubisya
•Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) - Bi. Sihaba Nkinga.
21.Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
•Katibu Mkuu- Bi. Suzan Paul Mlawi
•Naibu Katibu Mkuu- Nicholaus B. William
22.Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
•Katibu Mkuu - Prof. Kitila Mkumbo
•Naibu Katibu Mkuu- Mhandisi Emmanuel Kalobelo
Rais Magufuli amewapandisha vyeo Wakuu wa Wilaya watatu na kuwateua kuwa Wakuu wa Mikoa kujaza nafasi za Wakuu wa Mikoa waliostaafu.
Wakuu wapya wa mikoa
Bw Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Joel Bendera ambaye amestaafu.
Bw Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa nafasi ya Kamishna wa Polisi Zelote Stephen ambaye amestaafu.
Bw Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita nafasi ya Meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.
Bw Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, nafasi ya Dkt. Charles Mlingwa.
Bi Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, nafasi ya Bw. Jordan Rugimbana.
Bw Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, nafasi ya Bi. Halima Dendego.
No comments:
Post a Comment