Tuesday, April 10

Mashindano ya kuwabeba wake yafanyika Uingereza

Mshindi wa mchuano wa kubeba mkeHaki miliki ya pichaPA
Image captionMshindi wa mchuano wa kubeba mke
Haya ni mashindano ya 11 ya mbio za kubebana nchini Uingereza.
Chris Hepworth, akiwa amembeba Tanisha Prince kutoka West Drayton, London, alikimbia na kuibuka mshindi wa mbio za umbali wa mita 380.
Waandaaji wa michuano hiyo wanasema zoezi hilo lilianza mwezi June mwaka 793 AD.
Michuano inahusisha umbali wa mita 380 zenye vikwazo kukiwa na miinuko na miteremkoHaki miliki ya pichaPA
Image captionMichuano inahusisha umbali wa mita 380 zenye vikwazo kukiwa na miinuko na miteremko
Washindani walikimbia umbali wa mita 15 kupandisha kwenye mwinuko na kushuka ambapo wameeleza kuwa ni kazi ngumu.
Washindani si lazima wawe na ndoa lakini angalau wawe marafiki.
Chris Hepworth, alimbeba Tanisha Prince, aliibuka mshindiHaki miliki ya pichaPA
Image captionChris Hepworth, alimbeba Tanisha Prince, aliibuka mshindi
Sheria inasema wenza wawe na zaidi ya miaka 18 na uzito wa kilo 50 na kuna adhabu ikiwa utamuangusha mwenza wako, ikiwa uzito ni chini ya kilo 50 aliyembeba analazimika kubeba furushi lenye vikopo ili kuongezea uzito.
Mshindi anasema kupanda mlima ilikuwa rahisi kuliko kuteremka.
Washindi wataenda kwenye michuano ya dunia mwezi Julai nchini Finland
Bwana Hepworth ana matumaini ya kushinda.
Watu takriban 50 walishirikiHaki miliki ya pichaPA
Image captionWatu takriban 50 walishiriki
Waandaaji walitoa tahadhari wakisema kuwa ''kumbeba mke kunaweza kuwa jambo la hatari, kunakoweza kusababisha majeraha kama ya uti wa mgongo, kuvunjika miguu na mikono, majeraha usoni, kwenye fuvu la kichwa na hata kifo."
Ben and Hannah Brackenbury waliingia kwenye michuano hiyo wakiadhimisha mwaka mmoja wa ndoa yaoHaki miliki ya pichaPA
Image captionBen and Hannah Brackenbury waliingia kwenye michuano hiyo wakiadhimisha mwaka mmoja wa ndoa yao
Ben na Hanna Brackenbury waliingia kwenye mashindano hayo kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kumbukumbu ya ndoa yao
Wenza hao wamesema walikuwa wakifanya mazoezi kwenye bustani na kwenye mvua wakijiandaa na michuano.
Mitindo mbalimbali ya kubebana ilishuhudiwaHaki miliki ya pichaPA
Image captionMitindo mbalimbali ya kubebana ilishuhudiwa
Mshindi alipata pipa lenye bia anayeshika nafasi ya mwisho anapatiwa tambi na chakula cha Mbwa.
Washindi watakwenda kushiriki michuano ya dunia nchini FinlandHaki miliki ya pichaPA
Image captionWashindi watakwenda kushiriki michuano ya dunia nchini Finland
Aina hii ya ubebaji imeelezwa iliwafanya wakimbie kwa kasiHaki miliki ya pichaPA
Image captionAina hii ya ubebaji imeelezwa iliwafanya wakimbie kwa kasi
Michuano ya dunia itafanyika mwezi JulaiHaki miliki ya pichaPA
Image captionMichuano ya dunia itafanyika mwezi Julai

Safaricom na Airtel Kenya zaainisha huduma za utumaji wa pesa

Watu milioni 30 Kenya wanatumia simu za rununuHaki miliki ya pichaAFP
Kampuni mbili kubwa zaidi za mawasiliano ya simu za mkononi nchini Kenya Safaricom na Airtel zitaanza kusaidia kurahisisha usambazaji wa pesa chini ya mfumo unaowawezesha wateja kuweza kutuma ama kutoa pesa kupitia mtandao usio wa simu yao.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari makampuni hayo ya mawasiliano yamesema kuwa ushirikiano huu wa kuboresha huduma ya kusambaza pesa kwa njia ya simu miongoni mwa wateja inalenga kurahisisha uhamishaji wa pesa baina ya mitandao kwa kuunganisha mifumo ya usambazaji wa pesa kwa njia ya simu.
Wateja wa mitandao yote ya simu wataanza kwa kujisajili katika huduma ya (USSD) nambari ya ujumbe mfupi badala ya ndani ya programu yenyewe huduma hiyo.
'' Wateja wa mtandao wa Safaricom watahitaji kutumia nambari ya ujumbe mfupi kutuma pesa , tofauti na wanapotuma pesa kwa mtumiaji mwingine wa M-Pesa kwa njia ya Menu ya Safaricom ama programu tumizi'', inasema Safaricom.
Wateja wa mitandao yote ya simu wataanza kwa kujisajili katika huduma ya (USSD)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWateja wa mitandao yote ya simu wataanza kwa kujisajili katika huduma ya (USSD) nambari ya ujumbe mfupi badala ya ndani ya programu yenyewe huduma hiyo.
Mambo unayopaswa kuyafahamu juu ya kuunganishwa kwa huduma za pesa kwa mitandao tofauti ya simu za mkononi:
  • Itapatikana tu kupitia ujumbe mfupi(USSD) si kwa Menu ya safaricom.
  • Wateja wanaweza tu kupokea pesa kwenye wakala wa mitandao walikojisajili.
  • Gharama ya huduma itategemea mtandao.
  • Huduma hii itapatikana tu kwanza kwa wateja wa Safaricom na Airtel, Telecoms ni baadae.
  • Pesa zitakazotumwa zitaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya mpokeaji.
Tayari mtandao wa Safaricom umeanzisha kipengele cha M-Pesa popote kwa ajili ya mfumo huo mpya unaounganisha mitandao ya simu za mkononi kwa ajili ya huduma za usambazaji wa pesa.
Kwa huduma hii makampuni husika yamependekeza kwa pamoja kiwango cha malipo ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mtandao mmoja hadi mwingine yanayotarajiwa kuidhinishwa Benki Kuu ya Kenya (CBK), kulingana na Airtel.
Hata hivyo watumiaji wa huduma ya pesa ya Airtel -Airtel Money hawataweza kupokea pesa zao kutoka kwa wakala wa Safaricom wa M-Pesa ambapo hali itakuwa sawia kwa wateja wa Safaricom.
Airtel inasema kuwa bado inawatarajia wateja wake kupokea pesa kutoka kwa wakala wa mitandao yao kwasababu huduma hakuna wakala wa usambazaji wa pesa chini ya mfumo unaowawezesha wateja kuweza kutuma ama kutoa pesa kupitia mtandao usio wa simu yao.
Simu yenye huduma ya kutuma na kupokea pesa - M-PesaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKampuni ya Simu za mkononi ya Safaricom ndio inayotawala soko la pesa kwa njia ya simu za mkononi ikimiliki asilimia 67 ya wakala wa huduma za pesa kwa njia ya simu.
''Kwa ujumla hii inamaanisha kuwa pale mteja wa Airtel Money anapotuma pesa kwa mteja wa M-Pesa salio la akaunti ya mteja wa M-pesa liaonekana mara moja na mteja wa M-pesa anaweza kweda kwa wakala wa M-pesa kupokea pesa ama kuitumia kwa usambazaji mwingine wa pesa kwa njia ya simu ya mkononi.'' Imesema Airtel.
Kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom ndio inayotawala soko la pesa kwa njia ya simu za mkononi ikimiliki asilimia 67 ya wakala wa huduma za pesa kwa njia ya simu(mobile money) ambapo makampuni na taasisi zipatazo 40,000 zinakubali malipo kwa njia ya M-Pesa.
M-Pesa inadhibiti asilimia 80.8 ya soko la hisa kulingana na tathmini ya robo tatu ya mwaka 2017.
Uunganishaji wa huduma za mitandao ya huduma za usambazaji wa pesa kwa njia ya simu ulitambuliwa na utafiti juu ya ushindani kama moja ya mambo muhimu katika kuhakikisha unakuwepo ushindani unaofaa katika soko la pesa kwa njia ya simu za mkononi. Imesema mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya (CA).

Mahakama Uganda yasikiliza kesi dhidi ya ukomo wa umri wa kuwania urais

President Yoweri MuseveniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Yoweri Museveni ameongoza Uganda kwa ziadi ya miaka 30
Mahakama ya Kikatiba inasikiliza kesi iliyoletwa na upande wa upinzani kufuta marekebisho ya katiba ambayo yanatoa ukomo wa miaka ya kuwa rais.
Wabunge waliipigia kura wa kishindo mwaka uliopita kufuta ukomo wa miaka 75.
Ilimaanisha kuwa Rais Yoweri Museveni mwenye miaka 73, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30, anaweza kuwania tena mwaka 2021.
Mawakili wa upinzani walitoa hoja kuwa marekebisho hayo yaliingizwa "kinyemela" hadi kuwa sheria, na bunge halikufuata kanuni zilizopaswa katika kuweka marekebisho hayo.
Ulinzi umeimarishwa katika eneo la mahakama liliopo katika jiji la Mbale, mashariki mwa Uganda, na baadhi ya barabara zimefungwa kuepusha machafuko.
Hii ni mara ya kwanza ombi la haki la kikatiba linasikilizwa , anaripoti mwandishi wa BBC Patience Atuhaire kutoka jiji kuu la Kampala.
Miongoni mwa waomba haki ni wabunge wa upande wa upinzani,chama cha wanasheria Uganda na asasi za kiraia.
Wabunge wapigana makonde Uganda
Wanasema marekebisho hayo hayana msingi kwa sababu yalipitishwa wakati vurugu ilitokea kwenye vipindi ambapo walinzi waliovaa nguo za kawaida waliwatoa wabunge bungeni.
Pia wanatoa hoja kuwa Bw Museveni anataka kuwa rais wa maisha na kuwa mabadiliko hayo yanakiuka misingi ya kidemokrasia, utwala unamlikiwa na watu.
Washirka wa Museveni wanasema marekebisho hayo yanatoa ubaguzi wa kiumri na yalipitishwa baada ya kupata ushauri wa Umma.
Chama tawala cha National Resistance Movement kiliongoza mabadiliko hayo kupitia bunge na Bw Museveni akatia saini na kuifanya sheria.
Bw Museveni alishinda awamu ya tano mwaka 2016 katika uchaguzi uliodaiwa kuwa na dosari.
Ukomo wa awamu mbili ulifutwa mwaka 2005 ili kumwezesha awanie ofisi tena.

Giti: Eneo pekee Rwanda ambalo haikuathirika na mauji ya kimbari

Rwanda, inaadhimisha miaka 24 tangu yafanyike mauaji ya kimbari.Mauaji hayo yalifanyika kote nchini humo isipokuwa wilaya moja tu.
Hiyo ni wilaya ya Giti kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Sababu ya wilaya hiyo kutoshuhudia mauaji ya kimbari ni mshikamano baina ya wananchi na uongozi uliosimama na kupinga kila aina ya uonevu.
Mwandishi wa BBC Yves Bucyana alipatembelea na kuzungumza na wenyeji wa eneo hilo
Mmoja wapo ni Fidele Ntabana anaelezea kuwa aliwekwa kizuizini kwa tuhuma za kuwa jasusi wa RPF lakini wananchi wa eneo hilo walilindana.
Bango hii inasema "Muwe na amani na uvumilivu, umoja na maridhiano, tushirikiane kupiga vita itikadi ya Genocide"
Image captionBango hii inasema "Muwe na amani na uvumilivu, umoja na maridhiano, tushirikiane kupiga vita itikadi ya Genocide"
"Wahutu wa eneo hili walikuwa watu wazuri japo naweza kusema kwamba si wote kwa asilimia 100 lakini wengi hawakuwa na mpango wowote mbaya wa kuuwa watutsi.Familia yangu yote hakuna hata mmoja aliyeguswa.'' anasema
Watutsi kwa wahutu wanamsifu aliyekuwa kiongozi wao nyakati hizo, kunyima fursa propaganda za chuki na mauaji.
Mwenyeji mwingine, Andre Bisamaza anaelezea kuwa watu wabaya walikosa fursa ya kueneza propaganda ya mauaji.
Wenyeji wa wilaya ya Giti
Image captionWenyeji wa wilaya ya Giti
Anasema kuwa "mara kadhaa wanamgambo Interahamwe walitumwa kutekeleza mauaji katika eneo hili lakini yeye na askari jeshi na polisi aliokuwa nao walilazimika kuingilia kati na kuwafukuza wanamgambo hao''
Aliyekuwa kiongozi wa wilaya hii ya zamani ya Giti Sebushumba Edouard sasa ni mzee aliyestaafu.
Bwana Edouard
Image captionBwana Edouard
Mwandishi wa BBC Yves Bucyana alimkuta akisimamia shughuli za ukataji miti katika shamba lake.
Je ni siri gani aliyoitumia kuwaunganisha watu na kuhakikisha hakukuwa na mauaji katika eneo alililokuwa akiliongoza?
Bwana Edouard anasema kuwa ''kilichonisaidia ni desturi yangu kama kiongozi wakati huo ya kupinga uonevu ambayo pia niliijenga miongoni mwa wananchi wangu."
"Pia nilikuwa mtu asiyevumilia machafuko ya aina yoyote na kuadhibu wenye makosa.Kadhalika mimi na wasaidizi wangu tulikuwa tunaelewana kwa kauli moja.Ningelipata shida kubwa tusingekuwa na kauli moja.Ni wazi kwamba wananchi hawangeamua wenyewe kuuwa watutsi bila viongozi kuunga mkono vitendo hivyo'' anasema Edouard
Mwaka 1996 kiongozi huyo mstaafu alikuwa miongoni mwa wengine wengi waliotunukiwa medali za heshima kutokana na juhudi zao za kulinda raia wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Saturday, April 7

DC KIGAMBONI ATOA AMRI KWA WASIMAMIZI WA MRADI WA LAKE OIL KUFANYIWA MAHOJIANO MAALUM NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA


Mkuu wa wilaya ya kigamboni kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama leo wametembelea kata ya Pemba mnazi eneo la Yaleyale panu kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Alhamisi ya wiki iliyopita walipokuwa wakikagua majengo yaliyopo pembezoni mwa fukwe za bahari.
Akiongea na vyombo vya habari katika matembezi hayo Mh.Hashim Mgandilwa amesema kuwa takribani wiki mbili zilizopita walikuwa wanatembelea maeneo ya fukwe za bahari ili kufanya ukaguzi kutokana na wilaya hiyo ya kigamboni kuwa lango la biashara haramu na wahamiaji halamu.


Pia amesema kuwa katika ukaguzi huo waliofanya eneo linalomilikiwa na mwekezaji wa Lake oil lilikutwa na tatizo kwa kuwa na gati linaloweza kutumiwa na chombo chochote cha maji katika kushusha na kupakia mzigo wowote na kuagiza gati hilo kubomolewa ndani ya siku tano lakini maagizo hayo yamekiukwa ambapo utejelezaji umeanza kutekelezwa leo kinyume na barua waliyoituma halimashauri ikionyesha utekelezaji huo kutendeka.
Hata hivyo mkuu wa wilaya akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya usalama ameagiza kukamatwa kwa wahusika hao ili kufanyiwa mhojiano zaidi kwa sababu za kiusalama sambamba na kufika na vibali vinavyowaruhusu kufuga swala pamoja na hati miliki zinazoonyesha umiliki halali wa eneo hilo na kusisitiza kuwa kama hawatafanya hivyo watanyang’anywa eneo hilo na kukabidhiwa kwa mtu mwingine.
Viongozi hao waliokamatwa ni kiongozi mkuu wa miradi kutoka lake oil Fahim Mohammed na Mkurugenzi msaidizi wa lake oil Halid Mohammed, hata hivyo viongozi hao wamekana kukaidi agizo la mkuu wa wilaya na kuomba kupewa angalau muda wa mwezi mmoja kwani shughuli ya ubomoaji waliyoagizwa kufanya ni ngumu na inahitaji vifaa maalumu.
Kwa upande wake mwanasheria kutoka NEMC Manchale Heche amesema kuwa lake oil walipokea barua kutoka ofisi za NEMC ya kuwaruhusu kuendesha mradi pembezoni mwa bahari lakini hawakuruhusiwa kujenga nyumba za kudumu na walipewa masharti ambayo wameyakiuka.Hivyo Kufuatia ukiukwaji wa masharti hayo waliyopewa kutoka NEMC mwanasheria huyo amewafutia kibali cha kuendeleza mradi huo mpaka hapo watakapokutana na kufanya makubaliano ya kupata kibali kingine na kufuata masharti kama sheria inavyosema