Tuesday, March 6

Filamu ya Kenya yakosa kushinda Tuzo ya Oscar 2018

Picha kutoka kwa filamuHaki miliki ya pichaTOBIAS ROSEN
Filamu kuhusu shambulizi la kigaidi la al-Shabab nchini Kenya ambayo ilisifiwa sana baada ya kushinda tuzo ya Oscars kitengo cha wanafunzi mwaka jana, haikufanikiwa kushinda tuzo kuu katika Tuzo za Oscars.
Filamu hiyo kwa jina Watu Wote inahusu shambulio ambapo watu 2 waliuawa ndani ya basi eneo la Mandera mwaka 2015.
Watu Wote ilikuwa imeteuliwa kushindania tuzo ya Oscar katika kitengo cha Filamu Fupi kuhusu Matukio Halisi lakini washindi wa tuzo walipotangazwa, ikabwagwa na filamu ya The Silent Child ambayo waigizaji wake nyota Rachel Shenton na Chris Overton wanatokea Uingereza.
Filamu ya The Silent Child inaangazia maisha ya msichana wa miaka minne asiyeweza kusikia anayeishi maeneo ya mashambani England.
Shenton alitoa hotuba yake ya kupokea tuzo kwa lugha ya ishara ambapo alisema: "Nilitoa ahadi hii kwa mwigizaji wetu nyota ambaye ana miaka sita kwamba ningetoa hotuba hii kwa lugha ya ishara. Mikono yangu inatetemeka, kwa hivyo naomba radhi," alisema.
The Silent Child: Filamu iliyoshinda Watu Wote Oscars 2018
"Filamu yetu inahusu mtoto asiyeweza kusikia ambaye anazaliwa katika ulimwengu wa kimya. Si filamu iliyoongezwa chumvi, haya ni mambo ambayo yanawatendekea mamilioni ya watoto kote duniani ambao huishi katika kimya na kukumbana na matatizo katika kuwasiliana na hasa katika kupata elimu."
"Kutoweza kusikia ni ulemavu wa kimya, ninataka kutoa shukrani zangu kwa watoaji wa tuzo hizi kwa kutuwezesha kueleza hili kwa watu wengi."
Licha ya kukosa kushinda, Wakenya wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta wamekuwa wakiwapongeza walioshiriki katika kuigiza filamu hiyo ya Watu Wote wakiwapa heko kwa kazi nzuri.
Ubalozi wa Ujerumani nchini Kenya pia umewapongeza:
ADMI film school
Image captionWanafunzi Wakenya kutoka taasisi ya filamu ya Africa Digital Media Institute (ADMI) walishiriki katika kuigiza filamu hiyo wakishirikiana na wanafunzi kutoka Ujerumani

Hotuba kwa lugha ya ishara

Overton - ambaye anachumbiana na Shenton - alikuwa mwelekezi wa filamu hiyo. Nafasi ya msichana huyo mlemavu kwa jina Libby iliigizwa na Maisie Sly ambaye pia ana tatizo la kusikia.
Shenton ni mmoja tu miongoni mwa waigizaji wachache wa kike kuwahi kutoa hotuba kwa lugha ya ishara. Jane Fonda alitoa sehemu ya hotuba yake ya ushindi kwa lugha ya ishara kwa filamu yake ya
Coming Home mwaka 1979. Louise Fletcher pia alitoa hotuba kwa lugha ya ishara kwa sababu ya wazazi wake wasioweza kusikia aliposhinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike kwa filamu yake ya One Flew Over The Cuckoo's Nest miaka mitatu awali.
Marlee Matlin, ambaye ana matatizo ya kusikia, pia alitoa hotuba kwa lugha ya ishara baada ya kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike kwa filamu yake ya Children Of A Lesser God mwaka 1987.

Watu Wote ndiyo filamu ya kwanza kutoka Kenya kushinda tuzo za Oscars kitengo cha wanafunzi.
Picha kutoka kwa filamuHaki miliki ya pichaTOBIAS ROSEN
Filamu hiyo inayoeleza hadithi ya Kenya, kuhusu Wakenya na inashirikisha waigizaji wa Kenya, inasimulia shambulio hilo la mwaka 2014 kaskazini mwa Kenya, ambapo maudhui ya uadui wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu unaangaziwa.
Lupita Nyong'o ndiye Mkenya pekee kuwahi kushinda tuzo ya Oscar kufikia sasa, aliposhinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike msaidizi kwa uigizaji wake katika filamu ya 12 Years a Slave mwaka 2014.
Watu WoteHaki miliki ya pichaHAMBURG MEDIA SCHOOL
Image captionFilamu hiyo inaangazia jinsi Waislamu waliwakinga Wakristo wakati wa shambulio la kigaidi

Watu walio chini ya miaka 16 hawatauziwa vinywaji vyenye sukari Uingereza

Energy drinksHaki miliki ya pichaPA
Image captionMaduka yatapunguza mauzo ya vinywaji vyenye zaidi ya gramu 150 ya kafeini kwa kila lita
Mauzo ya vinywaji kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 yamepigwa marufuku kwenye maduka mengi nchini Uingereza kufuatia hofu ya vinywaji hivyo kuwa na viwango vya juu vya sukari na kafeini
Boots inaungana na maduka kama Asda, Waitrose, Tesco na the Co-op katika kutekeleza sheria hiyo.
Maduka yatapunguza mauzo ya vinywaji vyenye zaidi ya gramu 150 ya kafeini kwa kila lita kwa watu walio chini ya miaka 16.
Co-op ilisema imetambua wasi wasi kuhusu matumizi ya vinywaji vyenye sukari nyingi na kafaeini, miongoni mwa watoto.
Cans of Red BullHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMikebe ya kinywaji cha Red Bull
The Co-op, Aldi na Lidl zilifanya mabadiliko hayo tarehe mosi mwezi Machi huku Morrisons, Waitrose, Asda na Boots zikitekeleza sheria hiyi tarehe 5 Machi.
Msemaji wa Boots alisema: "Kuwasaidia wateja wetu kuishi maisha yenye afya umekuwa wajibu wetu.
"Tumeusikiliza umma kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vijana wanaotumia vinywaji hivi vyenye sukari nyinginan kafeini."
Licha ya Tesco kutangaza kufuata mkonndo huo haitatekeleza amri hiyo hadi Machi 26.

Siku ambayo Vladimir Putin alitokwa na machozi hadharani

Vladimir Putin and Lyudmila Narusova at Anatoly Sobchak's funeralHaki miliki ya pichaREUTERS
Raia wa Urusi wanapojiandaa kumchagua Vladimir Putin kuwa kiongozi wao kwa muhula wa nne mnamo 18 Machi, mwandishi wa BBC Gabriel Gatehouse ameangazia tukio la kipekee lililotokea mwanzoni mwa uongozi wa Putin ikulu.
Wakati huo alikuwa kaimu rais na alikuwa anawania urais kwa mara ya kwanza.
Warusi huwa ni nadra sana kumuona rais wao akilia, ingawa kumetokea mikasa mingi sana wakati wa utawala wake wa miaka 18.
Lakini ilitokea wakati mmoja, mwanzoni mwa utawala wake - mnamo 24 Februari 2000, wakati wa mazishi ya Anatoly Sobchak.
Sobchak alikuwa mmoja wa watu ambao, kwa pamoja na Gorbachev na Yeltsin, walisaidia kusambaratika kwa Muungano wa Usovieti.
Ndiye mwanamageuzi ambaye pia alimuinua afisa wa KGB kwa jina la Vladimir Putin ambaye alikuwa afisa wa kiwango cha wastani kutoka kutofahamika hadi kumpa kazi yake ya kwanza katika siasa.
Hakuna ajuaye hasa ni nini kilimhamasisha kuchukua hatua hiyo.
Lakini leo hii, mirengo ya watu wenye msimamo mkali kutoka kwa idara za usalama wakati wa Muungano wa Usovieti imechukua na kudhibiti mamlaka nchini Urusi kwa kiasi ambacho kimetishia demokrasia.
Mayor Anatoly Sobchak opens Austria Square in St Petersburg in September 1992, with Vladimir Putin (left) in attendanceHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionMeya Anatoly Sobchak akifungua rasmi Uwanja wa Austria mjini St Petersburg mnamo Septemba 1992, akiambatana na Vladimir Putin (kushoto)
Kuna wagombea wanane wa wanaowania urais uchaguzi wa sasa, lakini Putin anafahamika kuwa "mgombea mkuu" na hakuna aliye na shaka kuhusu matokeo.
Mmoja wa wagombea wanaoshindana naye ameeleza uchaguzi huo kuwa "uchaguzi bandia".
"Ni kama tu katika chumba cha kuchezea kamari," anasema, "ambapo mwenye chumba ndiye hushinda wakati wote, katika demokrasia ya Urusi, ushindi wakati wote huwa upande wa Putin."
Jina lake mgombea huyu, usishangae, ni Ksenia Sobchak, na ni bintiye Anatoly, rafiki na mlezi wa kisiasa wa zamani wa Putin.


Ksenia, kama anavyofahamika, ana miaka 36 na ni mtangazaji wa zamani wa kipindi cha uhalisia kwenye runinga ambaye amejiingiza kwenye siasa na kuwa mwanasiasa wa upinzani.
Wafuasi wa kiongozi mkuu wa upinzani Alexei Navalny ambaye amezuiwa kuwania wanasema yeye ni kikaragosi wa ikulu ya Kremlin na rafiki wa zamani wa familia ambaye ameingizwa na Putin kwenye kinyang'anyiro cha urais kuupa uchaguzi huo hisia za uhalisia.
Bila shaka, hangeweza kuwania bila idhini ya watawala. Hivyo ndivyo siasa na demokrasia Urusi hufanya kazi.
Ksenia Sobchak election posterHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBango la kampeni: "Kura kwa Sobchak. Kura kwa ukweli. Kura kwa uhuru."
Lakini wanaume wenye kuvalia nadhifu suti za rangi ya kijivu ambao huendesha mambo ikulu Urusi huenda kufikia sasa wanajutia hatua yao.
Ksenia kwa sasa anatembelea studio za runinga mbalimbani na kuwafichua washirika wafisadi wa Bw Putin na pia kueleza hatua ya Urusi ya kutwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine kama iliyo haramu.
Iwapo anawania, kama asemavyo, ndipo ashinde na si asikike tu, basi anavunja miiko fulani.
Nini kinatendeka kweli?
Tumwache binti kwa muda na tumuangazie babake.
Alikuwa meya wa St Petersburg, mji wa pili kwa umuhimu baada ya Moscow. Putin alikuwa naibu wake.
Wawili hao walikuwa na urafiki wa karibu sana kiasi kwamba Sobchak alipotuhumiwa kuhusika katika ulaji rushwa, Putin alimsaidia kuikimbia nchi hiyo akiwa ameabiri ndege maalum ya kukodishwa.
Hayo yalitokea miaka ya 1990.


Wazikumbuka siku hizo? Urusi ilikuwa kwenye vurugu.
Rais wake, Boris Yeltsin, alikuwa mlevu mara kwa mara na hakuimudu kazi.
Wanaume wenye suti za majivu Kremlin walifikia wamepata suluhu - mtu mwingine mwenye kuvalia suti za kijivu, asiye na doa, ambaye kutoka kwake wangeunda dawa ya kumkabili Yeltsin.
Walianza kumlea Putin kama mrithi wa Boris.
Kisha, ghafla, Putin alipokuwa anawania urais kwa mara ya kwanza, rafiki yake wa zamani Anatoly Sobchak, akafariki akiwa na umri wa miaka 62, akiwa chumba chake hotelini Kaliningrad.
Uchunguzi wa maiti yake ulisemakwamba alifariki kutokana na mshtuko wa moyo ingawa hakukuonekana dalili zozote za mshtuko wa moyo.
Mjane wa Sobchak alishuku kwamba mumewe alikuwa ameuawa na maafisa walikuwa wanaficha ukweli, na akaagiza uchunguzi huru wa maiti ufanyike.
Jina lake ni Lyudmila Narusova.
Nilikutana naye majuzi na kumwuliza iwapo alifikiri mumewe aliuawa.
Alitulia na kunyamaza kwa muda unaotosha kusema "Ndio" mara kumi, kisha akasema: "Sijui".
Ksenia Sobchak, Vladimir Putin and Lyudmila Narusova at a meeting to commemorate Anatoly Sobchak in February 2001Haki miliki ya pichaALAMY
Image captionKsenia Sobchak, Vladimir Putin na Lyudmila Narusova ibada ya kumkumbuka Anatoly Sobchak
Baadhi wamedokeza kwamba Putin huenda alihusika katika kifo cha Sobchak.
Sobchak alikuwa na siri kumhusu Putin? Narusova alipuuzilia mbali wazo hilo mara moja.
Nilirudi na kuangalia kwa makini video ya mazishi ya mwanasiasa huyo.
Putin anaonekana kuhuzunika sana. Macho yake mekundu, anaonekana kutatizika kumeza kitu kilichokwama kooni, huku akimkumbatia Lyudmila Narusova. Putin si mwigizaji.
Aidha, si mtu ambaye watu wamemzoea kuonesha hisia zake hadharani.
Hivyo, inaeleweka, kuamini kwamba anakabiliana na simanzi na majonzi halisi. Au ni kitu kingine? Dhamira yake inamhukumu?
"Kulikuwa na watu waliokuwa wanamsaidia Putin kuingia madarakani," Nasurova ananiambia.
Yuko sahihi.
Wakati huo, Putin alikuwa chombo cha kufikia madaraka kwa baadhi ya mirengo ya watu ndani ya Kremlin. Na kwa kiasi fulani bado yeye ni chombo.
Iwapo Sobchak aliuawa, aliuawa basi na moja ya mirengo hiyo iliyohofia kwamba mtu aliyemlea angechukua madaraka? Pengine. Na ikiwa ni hivyo, afisa huyo wa KGB aligundua kweli kwamba rafiki yake aliuawa akijaribu kuendeleza Mradi Putin. Ni jambo la kudhania tu, lakini naanza kufikiria hivyo.
Vladimir Putin and Lyudmila Narusova revisit Sobchak's grave in 2007Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVladimir Putin and Lyudmila Narusova revisit Sobchak's grave in 2007
Nilimwuliza Narusova kuhusu uchunguzi wa maiti uliofanywa kwa amri yake.
Anasema hakutoa matokeo hayo hadharani, lakini bado ameweka stakabadhi hizo kwenye sefu katika eneo salama nje ya Urusi.
Nilipomwuliza ni kwa nini, hakusema.
Nilimshinikiza. Nilimwambia, "Inaonekana kana kwamba umejipatia kitu kama mpango wa bima."
"Unaweza kulitazama hivyo," alijibu.
"Una wasiwasi?" nilimwuliza, "kuhusu usalama wako au wa binti yako?"
Anakaa kimya kidogo kisha kusema: "Unajua, kuishi katika nchi hii ni jambo la kuogofya. Hasa kwa wale ambao wana msimamo pinzani na wa serikali. Hivyo ndio, nina wasiwasi, wasiwasi ninao..."