Mauzo ya vinywaji kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 yamepigwa marufuku kwenye maduka mengi nchini Uingereza kufuatia hofu ya vinywaji hivyo kuwa na viwango vya juu vya sukari na kafeini
Boots inaungana na maduka kama Asda, Waitrose, Tesco na the Co-op katika kutekeleza sheria hiyo.
- Kijana afariki baada ya kunywa kafeini nyingi kwa haraka
- Uingereza kupambana na unene wa kupindukia kwa Watoto
- Msongo wa mawazo husababisha unene?
Maduka yatapunguza mauzo ya vinywaji vyenye zaidi ya gramu 150 ya kafeini kwa kila lita kwa watu walio chini ya miaka 16.
Co-op ilisema imetambua wasi wasi kuhusu matumizi ya vinywaji vyenye sukari nyingi na kafaeini, miongoni mwa watoto.
The Co-op, Aldi na Lidl zilifanya mabadiliko hayo tarehe mosi mwezi Machi huku Morrisons, Waitrose, Asda na Boots zikitekeleza sheria hiyi tarehe 5 Machi.
Msemaji wa Boots alisema: "Kuwasaidia wateja wetu kuishi maisha yenye afya umekuwa wajibu wetu.
- Mkate 'tosti' unaweza kuchangia saratani
- Faida za kahawa kubwa kuliko athari zake, wasema utafiti
- Nyama zilizopitia viwandani hatari kwa pumu
"Tumeusikiliza umma kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vijana wanaotumia vinywaji hivi vyenye sukari nyinginan kafeini."
Licha ya Tesco kutangaza kufuata mkonndo huo haitatekeleza amri hiyo hadi Machi 26.
No comments:
Post a Comment