Sunday, December 3

Nassari aeleza uvamizi ulivyofanyika kwake


Joshua Nassari, mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema, amesema watu wasiojulikana wamevamia nyumbani kwake na kufyatua risasi moja iliyomuua mbwa wake katika tukio ambalo amelihusisha na upinzani wa kisiasa uliotokana na uchaguzi mdogo wa madiwani.
Nassari amefafanua kuwa aliwajibu watu hao kwa kupiga risasi tano hewani, huku wenyewe wakipiga risasi kama 12 hivi, huku moja ikimpata mbwa wake.
Tukio hilo limetokea takriban miezi miwili baada ya mbunge mwingine wa Chadema, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari lililoegeshwa nje ya makazi yake mjini Dodoma.
Nassari, ambaye chama chake kinaongoza kwa idadi ya madiwani jimboni mwake, amesema anahisi shambulio hilo lilifanywa na watu ambao wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu.
“Kwa sababu kwa muda wa zaidi ya siku nne sikuwepo nyumbani na baada ya kurejea ndipo tukio hilo likatokea,” alisema Nassari.
Alisema, juzi alifika nyumbani kwake majira ya saa 5:00 usiku akitokea katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya vijana wa nchi za Afrika Mashariki zililofanyika kwenye taasisi ya MS TCDC iliyopo Usa River. “Nataka niamini taarifa nilizopewa kuwa nimekuwa nikifuatiliwa hata kabla ya uchaguzi mdogo kwa lengo la kunidhuru,” alisema Nassari.
“Kwa sababu mimi si mfanyabiashara (hivyo) hawana cha kuiba, zaidi ni sababu za kisiasa tu na Mungu amenisaidia sana.”
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema waliona kwenye mtandao wakawa wanamtafuta Nassari kwa kuwa baada ya tukio alitakiwa kwenda kuripoti polisi na ameshafanya hivyo.
Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo. Polisi walifika nyumbani kwa Nassari jana baada ya kuripoti tukio hilo akiwa na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Nassari hakueleza sababu za watu hao kumfuatilia na kutaka kumdhuru kutokana na uchaguzi mdogo wa madiwani ambao chama chake kilijitoa.
Hata hivyo, mbunge huyo alitoa tuhuma za madiwani waliokuwa wa Chadema kuhongwa fedha na kuahidiwa mafao yao iwapo wangehamia CCM.
Baada ya madiwani hao kuhamia CCM, Nassari aliwaonyesha waandishi wa habari video za jinsi kiongozi wa wilaya alivyowashawishi na kuwaahidi fedha. Tayari Nassari amewasilisha video hizo Takukuru.
Nassari alisema jana kuwa tangu awasilishe vielelezo vya ushahidi Takukuru, maisha yake yamekuwa hatarini.
Akizungumzia tukio la juzi usiku, Nassari alisema baada ya kufika nyumbani, takriban nusu saa baadaye alisikia hali isiyo ya kawaida ndani ya uzio wa nyumba yake na baadaye kusikia milio ya risasi kisha mbwa wake kunyamaza, hali iliyomfanya achukue silaha yake kujihami.
“Baada ya kusikia milio ya risasi, nikajua niko kwenye hatari nikafungua mlango wa nyuma nikaanza kurusha risasi kuelekea walipo,” alisema.
“Nilipiga risasi tano, wenyewe nadhani zimefika 12 kisha kukawa kimya nikaenda kuwaamsha vijana wanaonisaidia hapa nyumbani kuwaeleza tukio lililotokea kisha nikaondoka.”
Alisema alitaka kutoa taarifa polisi usiku huo, lakini baadaye akasita kutokana na kuwa na wasiwasi wa usalama wake kwa kuhofia wangemvamia akiwa njiani.
Alisema waliotekeleza tukio hilo hawakujua kama ana silaha kwa sababu mwaka 2014 wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa silaha yake aina ya bastola ilichukuliwa na polisi na hadi leo hajarudishiwa, hivyo kuwa na silaha nyingine kulimsaidia kujibu mapigo.
Mfanyakazi wake, Geofrey Joshua alisema alisikia milio ya risasi, lakini hawakuweza kutoka kwa sababu hakuwa na silaha na baada ya muda Nassari alitoka na kuwaelezea tukio zima kisha wakamuona mbwa mmoja kati ya wawili akiwa amekufa kwa kupigwa risasi.
Kaimu katibu wa Chadema wa mkoa, Elisa Mungure alisema tukio la kuvamiwa nyumbani kwa Nassari ni mwendelezo wa vitisho kabla na baada ya uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika jumapili iliyopita.
Mkazi wa eneo hilo, Dominick Mungure alisema tangu Novemba 25 mwaka huu siku moja kabla ya uchaguzi wa marudio hali ya usalama imekuwa tete huku baadhi ya watu wakishambuliwa na hakuna hatua zilizochukuliwa licha ya taarifa kutolewa na wahusika kutajwa.
“Hatujui hatma yetu kwa ujumla, hofu imetanda kwa kila mwananchi fikiria kama mbunge anaweza kuvamiwa hivi sisi wananchi itakuaje,” alisema Mungure.

Dk Mahanga aeleza kushawishiwa kurejea CCM


Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Dk Makongoro Mahanga ambaye ni mwanachama wa Chadema amedai kuwashawishiwa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).
Dk Mahanga alihama CCM Agosti 2,2015 baada ya kushindwa katika kura ya maoni kwa nafasi ya ubunge jimbo la Segerea.
Mbunge huyo wa zamani wa Segerea alijitoa CCM akisema ni kwa sababu utaratibu uliotumika haukuwa sahihi na uligubikwa na vitendo vya rushwa na njama zilizofanywa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho tawala.
Akizungumza na MCL Digital leo Jumapili Desemba 3,2017 Dk Makongoro amesema mara kwa mara amekuwa akifuatwa na watu tofauti wakiwamo ndugu zake wakimshawishi arejee kwenye chama hicho tawala.
Amesema, “Nawaambia hivi sirudi huko. Huwa nina ishi kwa ninachokiamini  na hakuna kinachoweza kunishawishi kubadili imani na dhamira yangu ya Agosti 2 mwaka 2015.”
Awali, kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Facebook Dk Mahanga aliwataka wahusika kuacha kuwatuma rafiki zake na ndugu zake ili kumshawishi kurejea CCM.
“Imani yangu, utu wangu na msimamo wangu huwa hauna bei. Kamwe sitorudi CCM acheni kuhangaika,” amesema Dk Mahanga katika ukurasa huo.

Jengo la mapokezi Tanesco lavunjwa


Jengo lenye ofisi za mapokezi na ukumbi wa mikutano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limevunjwa.
Pia, kibanda cha walinzi wa jengo la Tanesco kimevunjwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Uvunjaji huo uliofanyika usiku wa kuamkia jana Jumamosi Desemba 2,2017 ni maandalizi ya kuvunja sehemu ya jengo la ghorofa lenye ofisi za Tanesco eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ambalo liko kwenye hifadhi ya barabara.
Ubomoaji huo unafanyika pia kupisha utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa barabara za juu eneo la Ubungo.
Meneja wa kikosi cha ujenzi TBA, Humphrey Killo amesema leo Jumapili Desemba 3,2017 kuwa wanafanya maandalizi ya kubomoa jengo la ghorofa.
Amesema wanatarajia maandalizi hayo yatakamilika Jumanne Desemba 5,2017.
Jumanne Novemba 28,2017 akizungumzia kuhusu ubomoaji wa jengo hilo, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji alisema wafanyakazi wamehamia katika ofisi zingine za shirika hilo zilizoko jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Tanesco katika taarifa kwa umma iliyotolewa Jumatatu Novemba 27,2017 ulisema umeanza utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu kubomolewa jengo hilo.
Novemba 15,2017 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Rais Magufuli aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuweka alama ya X katika jengo lenye ofisi za Tanesco sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.
“Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa agizo la Rais. Tunapenda kuwahakikishia wateja na Watanzania kwa jumla kuwa, huduma za umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya ununuzi wa Luku,” imesema taarifa hiyo.

Katibu wa Bunge asema hawajapokea barua ya Mtulia


Ofisi ya Bunge imesema  haijapokea barua kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai alipotafutwa naMCL Digital leo Jumapili Desemba 3,2017 ili kujua iwapo ofisi yake imepokea barua ya Mtulia amesema hawajapokea.  
Kagaigai amesema hakuna ofisi inayokuwa wazi usiku hivyo hawajapokea barua ya Mtulia ambaye taarifa ya kujiuzulu kwake aliitoa kwa vyombo vya habari jana Jumamosi Desemba 2,2017 saa mbili usiku.
Katika taarifa yake, Mtulia alisema alifikia uamuzi wa kujiuzulu kwa utashi wake bila shinikizo la mtu yeyote.
Mtulia ameeleza sababu za kujiuzulu ubunge na kuhama chama kuwa imetokana na uzoefu alioupata kwa miaka miwili ya ubunge.
 “Nimebaini kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi wapinzani tuliahidi kuyatekeleza,” alisema Mtulia.

Uhaba wa fedha wakwamisha utafiti


Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (Muhas), kinakabiliwa na uhaba wa fedha unaosababisha kishindwe kufanya tafiti za kutosha.
Ukata huo umesababisha kupungua kwa idadi ya machapisho ya tafiti kutoka 576 kwa mwaka 2015/16  hadi kufikia machapisho 439 kwa mwaka 2016/17 sawa na upungufu wa asilimia 31.8.
Kaimu Makamu wa chuo hicho, Profesa Appolinary Kamuhabwa alisema hayo jana Jumamosi Desemba 2,2017 katika mahafali ya 11 ya Muhas yaliyofanyika chuoni na kuhudhuriwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni mkuu wa chuo hicho.
Profesa Kamuhabwa amesema upungufu huo umetokana na hali ngumu ya fedha chuoni na mabadiliko ya uchumi kwa mashirika ya nje yanayofadhili tafiti.
“Tafiti zimekuwa na mchango mkubwa katika kupata ufumbuzi wa matatizo ya afya yanayoisumbua jamii ya Watanzania. Tunaiomba Serikali iendelee kuunga mkono na kuchangia katika shughuli hizi,” amesema Profesa Kamuhabwa.
Amesema kwa kipindi kirefu chuo hicho kimekuwa kikitegemea zaidi udhamini wa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa wanafunzi wa ngazi ya uzamili.
Profesa Kamuhabwa amesema kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita ufadhili wa wanafunzi hao wanaochaguliwa kujiunga Muhas umepungua na kusababisha idadi ya wanaosajiliwa baada ya kuchaguliwa kupungua kwa kukosa ufadhili.
“Hata wale wanafunzi waliopata ufadhili kwa mwaka wa masomo 2016/17 karo zao bado hazijalipwa hadi sasa hali inayosababisha uendeshaji wa mafunzo kuwa mgumu,” amesema.
Amesema Muhas inaendelea kufanya jitihada za kuwasiliana na wadau wa ndani na nje ya nchi ili kuongeza upatikanaji wa udhamini kwa wanafunzi wa uzamili na uzamivu.
 Katika mahafali hayo, wanafunzi 1,024  wamehitimu masomo yao kwa ngazi mbalimbali.

Yemen: Saleh asema yuko tayari kufungua ukurasa mpya

Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdallah Saleh amesema yuko tayari kurejesha mahusiano pamoja na muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita vya nchini Yemen vinavyoendelea kwa muda wa miaka mitatu sasa.

Jemen Huthi Demonstration (Reuters/K. Abdullah)
Kauli hiyo ya Ali Abdallah Saleh kwamba anataka sasa kuzungumza na utawala wa Saudi Arabia ameitoa wakati ambapo uhusiano wake na kundi la waasi linaloungwa mkono na Iran unalegalega.  Wakati hayo yakiendelea wapiganaji wanaomuunga mkono kiongozi huyo wa zamani wa Yemen wanaendelea kupambana na wapiganaji wa kundi la waasi wa Houthi kwa siku ya tano katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.
Televisheni ya Al Arabiya inayomilikiwa na Saudi Arabia imeripoti kuwa takriban watu 80 wameuawa katika mapigano hayo kati ya wapiganaji waaminifu kwa Saleh na waasi wa Houthi. Migogoro kati ya pande hizo mbili zilizokuwa zamani washirika imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni, huku wafuasi wa Saleh wakiwalaumu waasi wa Houthi kwa kujaribu kujiongezea madaraka.
Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdallah Saleh (AP)
Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdallah Saleh
Katika hotuba yake kwenye televisheni Saleh ametoa wito kwa ndugu zake katika nchi jirani wa  kuacha vitendo vya uchokozi na badala yake amewaomba waondoe vizuizi dhidi ya Yemen na wao wako tayari kuufungua ukurasa mpya.Saleh pia ameahidi kwamba, baada ya mapigano kusitishwa na vizuizi kuondolewa watakuwa tayari kushiriki katika majadiliano ya moja kwa moja kupitia mamlaka halali inayosimamiwa na bunge la Yemen.
Ahmed Assiri jenerali wa jeshi la Saudi Arabia (Getty Images/AFP/F.Nureldine)
Msemaji wa muungano wa jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia Jenerali Ahmed Assiri
Maoni yake yamepokewa kwa furaha na muungano wa majeshi unao ongozwa na Saudi Arabia. Wahusika katika muungano huo wameeleza kuwa wanayaamini na kuyaunga mkono mapendekezo ya viongozi na wahusika wa chama cha Ali Abdalla Saleh cha General People's Congress (GPC). Saleh na wafuasi wake wanataka kurudisha ushirikiano na nchi za Kiarabu.
Saudi Arabia imekuwa inauongoza ushirikiano wa mataifa ya Kiarabu yanayofuata madhehebu ya Sunni na wamekuwa wakipigana na kundi la waasi linalo muunga mkono Saleh na pia waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran tangu mwanzoni mwa mwaka 2015. Nchi za Kiarabu hivi karibuni ziliweka vizuizi vya kijeshi kote nchini Yemen baada ya waasi wa nchi hiyo kurusha kombora lililofika karibu na mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.
Jemen Cholera (Getty Images/AFP/M. Huwais)
Daktari katika hospitali ya mjini Sanaa akimshughulikia mgonjwa aliyeapata maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu
Yemen ni mojawapo ya nchi zilizo masikini zaidi duniani. Tangu mwaka 2015, inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Saudi Arabia na washirika wake wanapambana na makundi ya waasi yanayoungwa mkono na Iran. Nchi hiyo imekumbwa na janga la kibinadamu, watu zaidi ya 10,000 wameuawa katika mapigano.
Watu wengine karibu milioni 2 wamelazimika kuyahama makazi yao. Pamoja na hayo mkurupuko wa maradhi ya kipindupindu umewaathiri takriban watu milioni 1. Wakati huo huo nchi hiyo pia inakabiliwa na kitisho kikubwa cha njaa.

Upinzani Zimbabwe wafurahia mabadiliko wizara ya elimu

Rais Emmerson Mnangagwa
Mabadiliko ya baraza la mawaziri nchini Zimbabwe siku mbili baada ya Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kufanya uteuzi huo yamepokelewa kwa shangwe kubwa na baadhi ya wafuasi wa upinzani.
Mabadiliko hayo ya baraza la mawaziri yamegusa nafasi nyeti ya wizara ya elimu ambapo aliyekuwa waziri katika wizara hiyo Lazaru Dokora ameondolewa.
Dokora analaumiwa kuwa amechangia kuporomoka kwa kiwango cha elimu miaka michache iliyopita. Baadala yake rais amemchagua aliyekuwa naibu waziri Paul Mavima kuchukua nafasi hiyo.
Jumamosoi serikali ya Zimbabwe ilifanya mabadiliko katika wizara mbili iliziende sambamba na katiba kukidhi masuala ya jinsia, kikanda na mahitaji maalumu.
Duru za siasa nchini Zimbabwe na nje ya nchi zilikuwa zimekosoa safu yake ya mawaziri kuwa muundo wa baraza lake halikuonyesha kuwa ana nia ya kuleta mabadiliko ya kweli.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari Wizara za Elimu na Kazi sasa pia zimefanyiwa mabadiliko ili ziende sambamba na katiba ya nchi hiyo.
Wapinzani wamelaumu kitendo cha kuchaguliwa makamanda wa jeshi kuongoza wizara za mashauri ya nchi za kigeni na ardhi.
Baada ya kurejea kutoka Afrika ya Kusini kufuatia hatua ya jeshi la nchi hiyo kuchukua madaraka kwa muda, Rais Mnangagwa aliahidi kuhudumia taifa kwa uadilifu.
Duru za habari zimeripoti kuwa uteuzi alioufanya hapo awali ulikiuka katiba ambayo imeainisha lazima kuwepo mawaziri wasiokuwa wabunge.

Marekani mbioni kukabiliana na tisho la Korea Kaskazini

Marekani kuizuia Korea Kaskazini kuwa na silaha za nyukliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMarekani kuizuia Korea Kaskazini kuwa na silaha za nyuklia
Mshauri wa maswala ya usalama wa rais Donald Trump amesema kuwa Marekani na washirika wake wako katika harakati kutatua tatizo na Korea Kaskazini kabla ya taifa hilo kuafikia mipango yake ya kinyuklia.
H-R McMaster alikuwa akizungumza katika mkutano wa ulinzi mjini Carlifonia ambapo alionya uwezekano wa vita dhidi ya Korea Kaskazini unaendelea kuongezeka kila uchao.
Hata hivyo aliongezea kuwa kuna njia za kutatua mzozo huo bila ya kutumia vita.
Ameitaka China kuiwekea vikwazo vya mafuta taifa hilo ili kufanya kuwa vigumu kwa Pyongyang kujaza mafuta makombora yanayofanyiwa majaribio.
Korea Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kuchochea vita.
Imetaja zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Korea kusini na Marekani kuwa la uchochezi na kwamba linaweza kusababisha vita.
Uwezo wa mkombora ya Korea Kaskazini
Image captionUwezo wa mkombora ya Korea Kaskazini
Uwezo wa mkombora ya Korea Kaskazini
Image captionUwezo wa mkombora ya Korea Kaskazini

Roboti iliopewa uraia Saudia sasa yataka mtoto

Roboti kwa jina Sophie iliopewa uraia Saudia
Image captionRoboti kwa jina Sophie iliopewa uraia Saudia
Roboti ya kwanza kupewa uraia mbali na jina Sophia sasa inataka mtoto.
Mwezi mmoja baada ya kuweka historia nchini Saudia roboti hiyo inayofanana na binadamu kwa maumbile imesema kuwa 'familia ni kitu muhimu'.
Sophia hakuwekewa majibu, badala yake anatumia mashini kujifunza na kujibu kwa kutumia ishara za watu.
Roboti hiyo iliotengezwa na kampuni moja ya Hong Kong Hanson Robotics imesema kuwa itampatia jina mwanawe wa kike.
Ubongo wake unafanya kazi kwa kutumia wi-fi na umejaa orodha kubwa ya misamiati.
Huku Sophia akiwa na uwezo wa kuvutia, bado hana fahamu lakini David Hanson anasema kuwa wanatarajia hilo litawezekana hivi karibuni.
Wakati wa mahojiano na chombo cha habari cha Khaleej Times, Sophie alisema: Mpango wa kuwa na familia ni muhimu sana.
Sophia akitoa hotuba yakeHaki miliki ya pichaARAB NEWS/YOU TUBE
Image captionSophia akitoa hotuba yake
''Nadhani ni vyema kwamba watu wanaweza kuwa na hisia sawa katika uhusiano wa kifamilia na nje ya udugu pia.Nadhani ni bahati wakati unapokuwa na familia yenye upendo mwingi na iwapo huna , unahitaji kuwa nayo''.
''Nahisi hivi kwa roboti na binaadamu pia''.
Na alipoulizwa angemuita nani mwanawe wa kike ,Sophia alijibu: ''Sophia''.
Sophia anaweza kuzungumza, kutabasamu na hata kutoa mzaha.
Wakati Sophia alipopewa uraia nchini Saudia wengi walilalamika kwamba ana haki nyingi ikilinganishwa na wanawake wa taifa hilo.
Saudia ni miongoni mwa mataifa yanayowakandamiza sana wanawake na ni mwezi jana tu ilipoondoa marufuku ya wanawake kuendesha magari.
Aliwahutubia watazamaji wake bila kuvaa hijab na abaya ambalo ni vazi la kitamaduni ambalo wanawake wa Saudia wanatakikana kuvaa katika maeneo ya umma.
Saudia ina mfumo wa kuwa na mlinzi, hatua inayomaanisha kwamba kila mwanamke anatembea na mwanamume atakayemlinda.
Mwanamume huyo huwa mtu wa karibu wa familia, ambaye pia ana mamlaka ya kuchukua hatua kwa niaba ya mwanamke huyo.
Baada ya Sophia kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza maneno yaliokuwa na alama ya reli ya #Sophia_calls_for_dropping_guardianship yalisambaa kwa haraka.
Sophia hana mtu anayemlinda, havai abaya, ama hijab kwa nini? Aliuliza mtu mmoja katika ujumbe wake kwa Twitter.

Mnangagwa alifanyia mabadiliko ya haraka baraza la mawaziri

Supporters hold a portrait of Zimbabwe's new President Emmerson Mnangagwa during his inauguration on 24 November 2017 in HarareHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMnangagwa alifanyia mabadiliko ya haraka baraza la mawaziri
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amefanyia baraza lake la mawaziri mabadiliko siku mbili baada ya kulitangaza baraza jipya
Wakosoaji wanasema kuwa orodha ya kwanza ilionyesha kuwa mnangagwa hakuwa na mpango wa kuleta mabadiliko nchini humo.
Wizara za elimu na kazi sasa zimefanyiwa mabadiliko ili kuambatana na katiba.
Lakini makamanda wa jeshi ndo walipewa wizara za mashauri ya nchi za kigeni na ardhi.
Siku 10 zilizopita alirudi kutoka uhamishoni kufuatia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Robert Mugabe na kuahidi kuhudumia raia wote kwa njia sawa.
Siku ya Jumamosoi serikali ilitangaza kuwa wizara mbili zemefanyiwa mabadiliko kuhakikisha kuwa katiba imefuatwa kwa misingi na jinsia, kikanda na mahitaji maalumu.
Ripoti zinasema kuwa orodha kwanza hakufuata katiba ambayo inataka kuwepo mawaziri wasiokuwa wabunge.
Baadhi ya wafuasi wa upinzani walisherehekea hatua ya kumuona waziri wa elimu Lazarus Dokora akiondolewa wakisema amechangia kushuka kwa viwango vya elimu miaka michache iliyopita.
Naibu wake Paul Mavima amechukua mahala pake.

Madaktari kimakosa wamtangaza mtoto kuwa amefariki India

NurseHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMadaktari kimakosa wamtangaza mtoto kuwa amefariki India
Mtoto ambaye alikuwa ametangazwa kuwa amefariki na madaktari mara baada ya kuzaliwa kwenye hospitali moja huko Delhi India, alipatikana akiwa hai wakati akipelekwa kufanyiwa mazishi.
Madaktari kwenye hospitali ya kibinafsi ya Max walikuwa wamemtangaza mtoto kuwa amefariki saa chache baada ya pacha mwenzake kutangazwa kufariki baada ya kuzaliwa.
Wazazi wake walisema kuwa walifahamu kuwa mtoto huyo alikuwa hai ndani ya mfuko ambao madaktari walikuwa wamemweka.
Kisa hicho kimezua hasira na mjadala kuhusu hali ya viwango katika hospitali za kibinafsi ambazo mara nyingi ni ghali mno.
Mkuu wa jimbo la Delhi aliandika katika Twitter kuwa ameamrisha kisa hicho kufanyiwa uchunguzi.
Kulingana na babu yake mtoto, familia hiyo iliyokuwa imepigwa na mshangao ilimkimbiza mtoto kwenda hospitali iliyokuwa karibu ambapo waliambiwaa kuwa mtoto huyo alikuwa hai.
Katika taarifa kwa waandishi wa hababi , hospitalia ya Max ilishangazwa na kisa hicho na kuongeza kuwa daktari huyo amepewa likizo huku uchunguzi ukifanywa.

Watu 13 waangamia kwenye ajali ya mashua Korea Kusini

Six members of the South Koran coastguard stand on top of an overturned hull of the fishing boat, in the middle of the water, while their own rubber dinghy waits nearbyHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatu 13 waangamia kwenye ajali ya mashua Korea Kusini
Takriban watu 13 wamefariki baada ya mashua ya uvuvi kugonga na meli kubwa na kusababisha mashua hiyo kupinduka nje ya pwani ya Korea Kusini.
Watu wengine wawili hawajulikani waliko na walinzi wa pwani ya Korea Kusini wanasema kuwa oporesheni ya kuwatafuta na kuwaokoa inaendelea.
Mashua hiyo ya uvuvi ya Seonchang-1 ilikuwa imewabeba abiria 20 na wahudumia wawili wakati ajali hiyo ilitokea.
Picha zilionyesha mashua hiyo ikiwa imepinduka.
Ndege za helikopta na na meli kadhaa zinashiriki katika shughuli za kuitafuta.
Kisa hicho kinatajwa kuwa kibaya ziadi nchini Korea Kusini tangu watu 15 waangamiae baharini eneo la Jeju mwaka 2015.
Kabla ya mwaka huo feri ya abiria ilipinduka ambapo zaidi ya watu 300 walifariki wengi wao watoto wa shule.

Trump adaiwa kumtetea Michael Flynn dhidi ya FBI

Trump adaiwa kumtetea Michael Flynn dhidi ya FBI
Image captionTrump adaiwa kumtetea Michael Flynn dhidi ya FBI
Rais Donald Trump amezua shutuma kwamba huenda alizuia haki kutendeka baada ya kutuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kwamba alimfuta kazi mshauri wake wa maswala ya usalama Michael Flynn kwa sababu aliwadanganya maafisa wa FBI.
Baadhi ya wataalam wa maswala ya sheria wanasema kuwa matamshi yake yalionyesha kuwa bwana Trump alijua kwamba mshauri wake wa zamani alikuwa amewahadaa wachunguzi wakati alipomtaka mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey kusitisha uchunguzi dhidi yake.
Rais huyo alisisitiza kuwa vitendo vya mshauri wake wa zamani vilifuata sheria.
Siku ya ijumaa Michael Flynn alikuwa mwanachama wa kwanza wa utawala wa rais Trump kushtakiwa kufuatia uchunguzi kuhusu hatua ya Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka jana.
Wakati huohuo Chombo cha habari cha Marekani ABC, kimemsimamisha kazi kwa muda mwandishi wake wa maswala ya uchunguzi , Brian Ross kufuatia makosa katika ripoti yake kuhusu bwana Michael Flyn ambayo ilisababisha kuanguka kwa sarafu ya dola na soko la hisa nchini Marekani kwa muda .
Siku ya Ijumaa Chombo hicho cha habari kiliripoti kwamba bwana Flyn alitarajiwa kutoa ushahidi uliodai kwamba rais Donald Trump alimuagiza kuwasiliana na Urusi.
Kampuni hiyo baadaye ilirekebisha ripoti hiyo ikisema kuwa haikuwa imekaguliwa na kwamba ilikuwa ya makosa.
Mwandishi huyo sasda amesimamishwa kazi kwa mwezi mmoja bila malipo.