Mabadiliko ya baraza la mawaziri nchini Zimbabwe siku mbili baada ya Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kufanya uteuzi huo yamepokelewa kwa shangwe kubwa na baadhi ya wafuasi wa upinzani.
Mabadiliko hayo ya baraza la mawaziri yamegusa nafasi nyeti ya wizara ya elimu ambapo aliyekuwa waziri katika wizara hiyo Lazaru Dokora ameondolewa.
Dokora analaumiwa kuwa amechangia kuporomoka kwa kiwango cha elimu miaka michache iliyopita. Baadala yake rais amemchagua aliyekuwa naibu waziri Paul Mavima kuchukua nafasi hiyo.
Jumamosoi serikali ya Zimbabwe ilifanya mabadiliko katika wizara mbili iliziende sambamba na katiba kukidhi masuala ya jinsia, kikanda na mahitaji maalumu.
Duru za siasa nchini Zimbabwe na nje ya nchi zilikuwa zimekosoa safu yake ya mawaziri kuwa muundo wa baraza lake halikuonyesha kuwa ana nia ya kuleta mabadiliko ya kweli.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari Wizara za Elimu na Kazi sasa pia zimefanyiwa mabadiliko ili ziende sambamba na katiba ya nchi hiyo.
Wapinzani wamelaumu kitendo cha kuchaguliwa makamanda wa jeshi kuongoza wizara za mashauri ya nchi za kigeni na ardhi.
Baada ya kurejea kutoka Afrika ya Kusini kufuatia hatua ya jeshi la nchi hiyo kuchukua madaraka kwa muda, Rais Mnangagwa aliahidi kuhudumia taifa kwa uadilifu.
Duru za habari zimeripoti kuwa uteuzi alioufanya hapo awali ulikiuka katiba ambayo imeainisha lazima kuwepo mawaziri wasiokuwa wabunge.
No comments:
Post a Comment