Wednesday, November 15

Mkufu wa Almasi wauzwa dola milioni 33.7 mjini Geneva

NecklaceHaki miliki ya pichaCHRISTIE'S IMAGES LTD
Image captionMkufu wa Almasi wauzwa dola milioni 33.7 mjini Geneva
Mkufu wa almasi kwa karati 163 ambao ni mkubwa zaidi wa aina yake kuuzwa, sasa umeuzwa kwa dola milioni 33.7 katika mnada huko Geneva.
Mkufuku huo ulichongwa kutoka kwa almasi ya karati 404 iliyopatikana nchini Angola.
Mkufu uliokamilika ulitengenezwa kutoka kwa dhahabu nyeupe, almasi na mawe ya thamani.
Uliuzwa katika hoteli ya Four Seasons mjini Geneva baada kuwekwa kwenye maonyesho huko Hong Kong, London, Dubai na New York.
Bei ya mkufu ilikuwa ya juu kuliko ile iliyotarajiwa ya dola milioni 30.
Aliyeununua mkufu huo hajatajwa.

Watu wengi waunga mkono ndoa za jinsia moja Australia

Two women kiss at a celebration in MelbourneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu wapiga kura kwa wingi kuunga mkono ndoa za jinsia moja Australia
Watu nchini Australia wamepiga kura kwa wingi katika hatua ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja kwenye kura hiyo ya kihistoria.
Kura ilionyesha kuwa asilimia 61.6 ya watu walipiga kura kuruhuru wapenzi wa jinsi moja kufunga ndoa.
Wanaounga mkono ndoa za jinsia moja wamekuwa wakisherehekea maeneo ya umma wakiimba na kucheza,
Waziri mkuu Malcolm Turnbul alisema serikali yake kwa sasa itaruhusu kupitishwa sheria hizo bungeni ifikapo krismasi.
"Watu wa Australia wamezungumza kwa mamilioni na wamepiga kura kwa wingi kura ya ndio kuleta usawa wa ndoa, Bw Turnbull alisema baada ya matoko kutangazwa.
The announcement prominent jubilant scenes across AustraliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu wapiga kura kwa wingi kuunga mkono ndoa za jinsia moja Australia
Matokeo hayo ya Jumatano yanafikisha kikomo iliyokuwa wakati mmoja kampeni kali.
Kura hiyo yenyewe imekosolewa na wale wanaounga mkono ndo za jinsia moja wengine wakisema kuwa haikuhitajika wakati bunge lilikuwa na uwezo wa kuijadili moja kwa moja.
Wati walikuwa wanashiriki kwa hiari kinyume na uchaguzi ambao ni wa lazima nchini Australia.
Zaidi ya watu milioni 12.7 karibu asilimia 79.5 ambai ni wapiga kura walishiriki katika zoezi hilo la majuma 8 ambapo swali moja tu liliulizwa, "sheria ya ndoa inaweza kubadilishwa kuruhusu wapenzi wa jinsia moja kufunga ndo?"
Two men embrace at a celebration in SydneyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu wapiga kura kwa wingi kuunga mkono ndoa za jinsia moja Australia
People listen to No campaigner Lyle Shelton speak after the resultHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu wapiga kura kwa wingi kuunga mkono ndoa za jinsia moja Australia

Jeshi la Zimbabwe: Tunawalenga wahalifu sio Mugabe

Jeshi la Zimbabwe: Tunawalenga wahalifu
Image captionJeshi la Zimbabwe: Tunawalenga wahalifu
Jeshi la Zimbabwe limesoma taarifa kwenye kituo cha runinga cha serikali ZBC, likisema kuwa linachukua hatua ya kuwalenga wahalifu.
Hata hivyo limesema kuwa hayo sio mapinduzi ya kijeshi na Rais Mugabe yuko salama.
Milio mikubwa ya risasi ilisikika katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu Harare mapema leo.
Taarifa hiyo ya jeshi ilikuja saa kadhaa baada ya jeshi kudhibiti kituo cha ZBC.
Mwanamume mmoja ambaye alikuwa amevaa sare za jeshi alisema kuwa jeshi linataka kukabiliana na watu ambao wanatenda uhalifu unaoleta madhara ya kijamii na kiuchumi nchini Zimbabwe.
"Wakati tutakapomalzia wajibu wetu, tunatarajia kuwa hali itadudi kuwa sawa."
Taarifa hiyo ilisema kuwa Mugabe 93, na familia yake wako salama.
Wanajeshi wakiwa na silaha nzito wameoneakana wakirandaranda mjini Harare
Image captionWanajeshi wakiwa na silaha nzito wameoneakana wakirandaranda mjini Harare
Haijulikani ni nani anaongoza hatua hiyo ya kijeshi.
Magari ya wanajeshi waliojihami kwa silaha yameonekana maeneo ya mjini Harare.
Hali hiyo ya wasi wasi wa lolote kuweza kutokea, imeanza hapo jana jioni, ambapo wanajeshi wakiwa na silaha walionekana wakijipanga katika maeneo kadhaa pamoja na kuzingira ofisi za shirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC.
Hata hivyo taarifa zinasema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo la utangazaji ZBC, waliambiwa na wanajeshi hao kwamba hawapaswi kuwa na wasiwasi na kwamba uwepo wa vikosi hivyo ni kwa lengo la kulinda eneo hilo.
Milipuko mizito imeendelea kusikika pia.
Mkuu wa jeshi la Zimbabwe Constantino Chiwenga alitahadharisha uwezekano wa jeshi kuchukua nchi
Image captionMkuu wa jeshi la Zimbabwe Constantino Chiwenga alitahadharisha uwezekano wa jeshi kuchukua nchi
Chama tawala nchini Zimbabwe kimemtuhumu mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga, kwa hatua yake ya madai kuwa jeshi lipo tayari kuingilia mzozo huo wa kisiasa kwa lengo la kulinda wapigania uhuru wa taifa hilo.
Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Rais Robert Mugabe kutokana na hali ya sasa nchini mwake.
Marekani imesema kuwa inafuatilia kwa karibu hali ya Zimbabwe na kutoa rai pande zote kutatua mzozo huo kwa njia ya amani.
Grace Mugabe anaonekana kukaribia kukirithi kiti cha mumewe
Image captionGrace Mugabe anaonekana kukaribia kukirithi kiti cha mumewe
Naye Balozi wa Marekani nchini Zimbabwe kupitia ukurasa wake wa Tiwtter amesema kuwa leo watasitisha shughuli za kiofisi ubalozini hapo kutokana na halisi ya sasa mjini Harare.
Balozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini Isack Moyo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa serikali ipo imara katika jambo hilo na kuzuia uwezekano wowote wa kufanyika kwa mapinduzi.

Jeshi la Zimbabwe lakanusha kufanya mapinduzi

Jeshi la Zimbabwe limekanusha madai kwamba mapinduzi ya kijeshi yamefanyika kuiondoa serekali, na kudai kwamba rais Robert Mugabe na familia yake wapo salama.
Katika taarifa iliyotolewa na jeshi kupitia televisheni ya taifa, imeelezwa kwamba jeshi linalenga wahalifu wanaosababisha shida za kijamii na kiuchumi na kuwafikisha mbele ya sheria.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya mashuhuda kusema wamesikia takriban milipuko mitatu pamoja na milio ya risasi katika mji mkuu wa Harare, usiku wa kuamkia Jumatano.
Inaelezwa pia na mashuhuda magari ya jeshi na wanajeshi walikuwa katika mitaa mapema Jumatano hii saa kadhaa baada ya wanajeshi kushikilia chombo cha utangazaji cha serekali cha ZBC.
Wakazi wamesema kwamba tofauti na kuwepo kwa taarifa ya habari ya saa tano usiku, ZBC ilicheza muziki bila taarifa yoyote.
Msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Harare, ameiambia VOA kwamba mitaa ya Harare ilionekana kuwa tulivu usiku wa kuamkia leo, na hakuthibitisha kuona magari ya kijeshi.
Msemaji huyo pia amesema hana taarifa ya milipuko yoyote kutokea kama ilivyoelezwa na baadhi ya wakazi wa Harare.
Hapo jana Jumanne, chama tawala nchini Zimbabwe ZANU-PF kilimshutumu mkuu wa majeshi kwa vitendo vya uhaini baada ya kutishia kuingilia kati mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Taarifa ya ZANU-PF ilitolewa katikati ya wasiwasi uliotanda kwamba jeshi limechukuwa hatua ya kuchukuwa madaraka na kumuondoa rais wa muda mrefu wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Mashuhuda waliripoti kuona vifaru na maafisa wa jeshi wakiwa mitaani na kelekea nje ya mji licha ya Harare kuwa tulivu.
Balozi za nchi mbalimbali nchini humo hazikutoa tahadhari kwa raia wake walioko nchini Zimbabwe kwa sasa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani aliiambia VOA kwamba wanataarifa hizo na wanaendelea kufanya uangalizi.
Hali ya wasiwasi ya sasa ilizuka juma lililopita wakati rais Robert Mugabe alipomfukuza naibu wake Emmerson Mnangagwa na kumshutumu kwa kutomti na kupanga kutwaa madaraka.

PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 15,2017



































VIJANA CCM WAMVAA FREEMAN MBOWE

UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umesema Rais Dk. John Magufuli hajawahi kutamka mahali popote kama Serikali ni ya kwake na si ya CCM, kama ilivyodaiwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Pia umoja huo umesema pamoja na Serikali kuongozwa na Rais Magufuli, bado iko chini ya Chama Cha Mapinduzi na kumtaka Mbowe kuacha maneno ya upotoshaji na uchochezi wa kitoto.
Msimamo huo umetolewa Dar es Salaam jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alipozumgumza na waandishi wa habari kufuatia madai ya Mbowe dhidi ya Rais Magufuli na utawala wake.
Alisema tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita, amekuwa akihimiza shime ya kukuza fikra mpya na kudumisha uzalendo ulioporomoka na kuzaa kundi la mafisadi, wezi wa mali za umma bila kujali itikadi za kisiasa, kwa sababu uzalendo hauna alama ya siasa au chama.
“Mbowe ni mwanasiasa mnafiki na profesa wa kuzua. Amesahau alipowakusanya wananchi pale Mwembeyanga Temeke na kutaja orodha ya viongozi wa Serikali aliodai ni mafisadi likiwemo jina la Edward Lowassa aliyehamia Chadema na kuteuliwa kuwa mgombea urais,” alisema Shaka.
Alisema ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 ni miliki ya CCM na Rais Magufuli hana ilani binafsi ya uchaguzi, hivyo akamtaka Mbowe aache kumlisha maneno  kiongozi huyo wa nchi kwa kusaka kwake umaarufu wa kisiasa.
Akizungumzia madai kuwa utawala wa Rais Magufuli umekuwa ni wa kimabavu, ubaguzi na kujali ukanda na ukabila, Shaka alisema huo ni uzushi mpya kwani sera ya ukanda, ukabila na udini ni ya Chadema kutokana na ushahidi mwingi.
“Mbowe aache kufuatilia mambo ya CCM kwa sababu hayatamsaidia yeye au chama chake. Hana sifa ya kuwa kiongozi mkweli mbele ya Watanzania, kwa sababu ni wakala wa mafisadi na chama chake kimekuwa maficho ya viongozi wasiotamanika katika jamii,” alisema.
Aidha alisema Serikali ya awamu ya tano haijawahi kukataa kupokea ushauri au maoni ndiyo maana Rais Magufuli  amekubali hata kupokea ilani ya uchaguzi ya CCM kama mwongozo wake na hakuna mwenye uwezo wa kumpangia namna ya uteuzi wa wasaidizi wake.
Shaka alisema CCM itaendelea kuamini na kufuata Itikadi ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani ujamaa si utitiri wa vibanda vya nyasi na kadhia ya umasikini bali ni imani na utekelezaji.