Mkufu wa almasi kwa karati 163 ambao ni mkubwa zaidi wa aina yake kuuzwa, sasa umeuzwa kwa dola milioni 33.7 katika mnada huko Geneva.
Mkufuku huo ulichongwa kutoka kwa almasi ya karati 404 iliyopatikana nchini Angola.
Mkufu uliokamilika ulitengenezwa kutoka kwa dhahabu nyeupe, almasi na mawe ya thamani.
- Almasi ya thamani kubwa yapatikana Sierra Leone
- Serikali ya Tanzania yaendelea kuzuia almasi ya kampuni ya Petra
- Almasi iliyopatikana nchini Botswana yauzwa kwa dola milioni 53
Uliuzwa katika hoteli ya Four Seasons mjini Geneva baada kuwekwa kwenye maonyesho huko Hong Kong, London, Dubai na New York.
Bei ya mkufu ilikuwa ya juu kuliko ile iliyotarajiwa ya dola milioni 30.
Aliyeununua mkufu huo hajatajwa.
No comments:
Post a Comment