Monday, August 28

Uharibifu wa Kimbunga Harvey Marekani

Brad Matheney akimsaidia mtu mwenye kiti cha magurudumu GalvestonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKimbunga hicho kimesababisha mafuriko katika maeneo mengi
Kimbunga Harvey kilifika maeneo ya Marekani bara Ijumaa jioni na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Upepo wa kasi ya hadi 130mph (215 km/h) ulipiga maeneo ya pwani ya Texas.
Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kuwahi kupiga maeneo ya Marekani bara katika kipindi cha miaka 13 na kimesababisha uharibifu mkubwa maeneo hayo.
Mji wa Rockport ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi. Magari na majumba yaliharibiwa katika uwanja wa ndege wa mji huo...
Destroyed vehicles and buildings at Rockport AirportHaki miliki ya pichaAFP
...sawa na ndege kadha ndogo.
A light plane sits upside down at Rockport AirportHaki miliki ya pichaAFP
Mji wa Rockport ulipigwa na kimbunga hicho usiku kucha.
A Rockport firefighter goes door to door on a search and rescue mission as he looks for people that may need helpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
A woman walks away from a destroyed apartment buildingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Jessica Campbell hugs Jonathan Fitzgerald (L-R) after riding out Hurricane Harvey in an apartment on August 26, 2017 in Rockport, TexasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
A man tries to kick open a door of an apartment to find his friendsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wakazi wa mji wa pwani Corpus Christi pia waliathirika pakubwa. Nguvu za umeme zilikatika na eneo lote likajaa giza.
Stewart Adams, of San Marcos, Texas, battles the winds in Corpus Christi U.S. on 25 August, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Local residents sit at the bar in the dark after a citywide power failure as Hurricane Harvey hit Corpus Christi, Texas, on August 25, 2017Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
A man walks near the bay waters as they churn from approaching Hurricane Harvey on August 25, 2017 in Corpus Christi, TexasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
People walk through high winds in Corpus ChristiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Jumamosi, wengi waliamka kupata barabara hazina watu na majumba yameharibiwa. katika baadhi ya maeneo, moto ulizuka.
Lakini uharibifu katika mji huo haukufikia uharibifu ulioshuhudiwa Rockport.
A burnt out house and cars that caught fire are seen after Hurricane Harvey hit Corpus Christi, Texas on August 26, 2017Haki miliki ya pichaAFP
A white SUV car is seen submergedHaki miliki ya pichaAFP
Ijumaa, kabla ya kimbunga kufika bara, watalii wanaopenda kufuatilia vimbunga walikuwa wamefika kwenye fukwe kujionea mawimbi na kupiga picha. Wengi baadaye walikimbilia maeneo salama.
A resident photographs the beach in Corpus ChristiHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Watu wengi walihama miji na biashara kufungwa kuzuia uharibifu.
Sign on a business reading Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Maafisa wameonya kwamba maeneo mengi yatashuhudia mafuriko mabaya katika kipindi cha siku chache zijazo.
Tayari kumetoka mafuriko Galveston.
People walk dogs through flooded streets as the effects of Hurricane Henry are seen August 26, 2017 in Galveston, TexasHaki miliki ya pichaAFP
Na mjini Port Lavaca.
Floodwaters outside a house in Port LavacaHaki miliki ya pichaREUTERS
Mjini San Antonio, wanyama pia walihamishwa...
Horses are evacuated in San AntonioHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Wakazi wa Houston - mji wa nne kwa wingi wa watu Marekani - wamekuwa wakijiwekea chakula cha akina. Rafu nyingi katika maduka ya jumla hazina bidhaa.
Woman looks over bare refrigerator shelves in a Walmart in HoustonHaki miliki ya pichaREUTERS
Kimbunga Harvey kimeathiri sana uchimbaji wa mafuta Ghuba ya mexico pamoja na uchukuzi wa ndege.
Asilimia 45 ya usafishaji wa mafuta Marekani hufanyika katika ghuba hiyo.
Tangi la mafuta liliharibiwa akribu na mji wa Seadrift, katika wilaya ya Calhoun.
An oil tank damaged by Hurricane Harvey is seen near Seadrift, Texas, August 26, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Picha za Nasa zimeonesha kimbunga hicho kilivyoonekana kutoka anga za juu.
This NASA image from August 25, 2017, taken by NASA astronaut Jack Fischer shows Hurricane Harvey (top) from the cupola module aboard the International Space Station.Haki miliki ya pichaAFP/NASA

Mhasiriwa wa ubakaji India, mwenye umri wa miaka 13 aiomba mahakama kuavya mimba

Kina dada wakiashiria wahasiriwa wa visa vya ubakajiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKina dada wakiashiria wahasiriwa wa visa vya ubakaji
Wazazi wa msichana mwenye umri wa miaka 13 mhasiriwa wa matendo ya ubakaji kutoka mji wa Mumbai huko India, wamekwenda katika mahakama kuu ya nchi hiyo, kuomba idhini ya kuavya mimba aliyo nayo binti wao.
Msichana huyo ana mimba ya wiki 30.
Sheria nchini India, inakubalia uavyaji mimba wa wiki 20 ikiwa tu maisha ya mwenye mimba iko hatarini.
Mimba hiyo iligunduliwa baada ya wazazi wake kumchukua kwa daktari kwa matibabu, kutokana na kuongezeka uzito kupita kiasi.
Msichana huyo anasema kuwa alibakwa na rafiki wa babake, ambaye kufikia sasa amekamatwa na kuzuiliwa.
Kesi hiyo inafanyika siku kadhaa baada ya msichana mwengine mhasiriwa wa ubakaji mwenye umri wa miaka 20, alipozaa katika mji ulioko Kaskazini mwa India wa Chandigarh.
Masaibu yake yalisababisha hisia kubwa kote duniani huku vyombo vya habari vikiangazia pakubwa taarifa hiyo, hasa baada ya mahakama kukatilia mbali ombi la kuavya mimba hiyo kwamba mimba hiyo ilikuwa ni kubwa mno kwa kuavya.
Mwezi Mei, kesi kama hiyo iliripotiwa katika mji wa Hyarana kaskazini mwa India, ambapo msichana mwenye umri wa miaka 10 ambaye alidaiwa kubakwa na babake wa kambo, alikubaliwa kuitoa mimba hiyo.
Mwaandishi wa BBC mjini Delhi huyo India, Geeta Pandey, anasema kuwa kesi tatu kama hiyo, imewashangaza wengi, lakini wanaharakati wanaamini kuwa, kuna uwezekana wa visa vingi kama hivyo, ambavyo haviripotiwi na vyombo vya habari, kwa sababu vinagundfuliwa baada ya makataa ya majuma 20 na wazazi wengi waharipoti visa kama hivyo kwa polisi.
Visa vya ubakaji vimeongezeka sana IndiaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionVisa vya ubakaji vimeongezeka sana India

Gurmeet Ram Rahim Singh, amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na mahakama India

Polisi India wanasema kuwa wamepewa idhini ya "kuwapiga risasi na kuuwa" ni amri wakati wa ghasiaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPolisi India wanasema kuwa wamepewa idhini ya "kuwapiga risasi na kuuwa" ni amri wakati wa ghasia
Mahakama moja kaskazini mwa India imemhukumu Guru mmoja wa kidini mwenye utata kifungo cha miaka 10, kwa kosa la kuwabaka wanawake wawili.
Juma lililopita, mahakama hiyo ilimpata na hatia Bw. Gurmeet Ram Rahim Singh, anayejiita mtu mtakatifu na makosa ya kuwabaka wanawake hao wawili, ambao ni waumini wake.
Hukumu yake ilisababisha ghasia na maandamano mabaya katika majimbo ya Haryana na Punjab ambapo watu 38 waliuwawa.
Maelfu ya polisi wa kupambana na fujo, wametumwa karibu kila mahali nchini India ili kuzua vurumai na ghasia ambazo zinaweza kutokea.
Taarifa zaidi zingali zikitokea.
Gurmeet Ram Rahim Singh pia huimba nyimbo za Rock
Image captionGurmeet Ram Rahim Singh pia huimba nyimbo za Rock
Walinda usalama kote nchini India, wamewekwa katika hali ya tahadhari, kabla ya mahakama nchini humo kutoa uamuzi wa mwisho katika hukumu ya ubakaji dhidi ya kiongozi mmoja wa kidini.
Wafuasi wa Gurmeet Ram Rahim Singh, walizua vurumai na ghasia siku ya Ijumaa, baada mahakama moja mjini Panchkula kumshitaki guru huyo.
Watu 38 waliuwawa katika ghasia hizo.
Amri ya kutotoka nje usiku imewekwa katika majimbo mawili ya Haryana na Punjab, ilihali usalama mkubwa ukiimarishwa katika mji mkuu Delhi.
Wanajeshi wa taifa hilo pia wako katika hali ya tahadhari, huku polisi wakisema kuwa wamepewa idhini ya "kuwapiga watu risasi na kuuwa" sheria inayotumika wakati wa matatizo.
Bw. Singh, mwenye umri wa miaka 50, hakupelekwa mahakamani kusomewa mashtaka dhidi yake, badala yake jaji aliyemhukumu, alipelekwa kwa ndege hadi gereza la Rohtak, anakozuiliwa Guru huyo, ili kumhukumu huko.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu mchana, saa za Afrika Mashariki.
Gurmeet Ram Rahim Singh ni nani?
Gurmeet Ram Rahim
Image captionGurmeet Ram Rahim
  • Kiongozi huyo mwenye utata, wa madhehemu ya Dera Sacha Sauda sect, inayodai kuwa na zaidi ya wafuasi milioni 60 kote Duniani.
  • Alianza kuongoza madhehebu hayo- inayodai kuwa "isiyohitaji faida bali inayoshughulikia maslahi ya kijamii na kiroho".
  • Anaigiza katika tasha za muziki aina ya Rock, kuigiza kwenye filamu na pia kuwa na msururu wa bidhaa zake za chakula.
  • Anajulikana kama "rockstar baba" na "guru of bling" kutokana na mavazi yake yanayomeremeta.
  • Ameshutumiwa mara kwa mara kwa kuwakejeli viongozi wa madhehebu ya Sikh na Hindu.
  • Amekuwa akichunguzwa kwa kosa la mauwaji na ubakaji, makosa ambayo ameyakanusha.
  • Ameshutumiwa kwa kuwalazimisha wafuasi wake wa kiume kuhasiwa ili "kukaribia zaidi mungu"
Polisi akimkabili mmojawepo wa wafuasi wea madhehebu ya Dera Sacha Sauda nchini India
Image captionPolisi akimkabili mmojawepo wa wafuasi wea madhehebu ya Dera Sacha Sauda nchini India
Gereza anamozuiliwa Guru huyo imefanywa kuwa ngome, huku waandishi wa habari wakizuiwa kulifikia kwani wanazuiliwa umabli wa kilomita 1.5 au kama (maili moja) mraba.
Mji wa Rohtak ulioko katika Jimbo la Haryana, pia unalindwa na maafisa wa polisi na jeshi, huku barabara zote zikiwekwa sen`genge ya miiba.
Idadi kubwa ya polisi wamezingira boma la Bwana Singh lililoko katika ekari 1,000 huko Sirsa, Haryana.
Shule na vyuo vimefungwa, huduma za simu za mkononi zimekatwa kote Haryana tangu Alhamisi iliyopita, huku marufuku hiyo ikiongezwa kwa masaa 48 yajayo.
Mamia kwa maelfu ya wafuasi wake wanaamini wangali ndani ya makao yake makuu ya madhehebu hayo ya Dera Sacha Sauda, huku baadhi yao wakiamua kuondoka kutokana na taharuki ya uwepo wa polisi.

Upinzani waruhusiwa kukagua mitambo ya tume ya uchaguzi Kenya

Bw Odinga amewasili kesi mahakamani kupinga ushindi wa Bw KenyattaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBw Odinga amewasili kesi mahakamani kupinga ushindi wa Bw Kenyatta
Mahakama ya Juu nchini Kenya imeukubalia muungano wa upinzani nchini humo National Super Alliance (Nasa) kupekua sava zilizotumiwa na tume ya uchaguzi nchini humo wakati wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Mahakama hiyo imesema muungano huo utaweza kusoma data kwenye sava hizo chini ya uangalizi kuhakikisha usalama wa mitambo ya IEBC hauhujumiwi.
Mgombea wa Nasa Raila Odinga amewasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee.
Mawakili wa Bw Odinga wameruhusiwa na mahakama kunakili data kutoka kwenye sava hizo kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu uchaguzi huo.
Miongoni mwa mengine, upinzani utapata utambulisho wa sava zilizotumiwa wakati wa uchaguzi, ukuta wa kinga uliotumiwa kulinda sava hizo pamoja na mitambo ya dijitali ya uchaguzi wa Kenya (KIEMS) dhidi ya wadukuzi na mfumo endeshi wa mitambo hiyo pamoja na nywila zilizotumiwa kuingia katika mitambo hiyo.
Kadhalika, wataweza kupata taarifa kuhusu yaliyojiri katika mitambo hiyo ya uchaguzi kuanzia Agosti tano hadi leo.
Aidha, wataruhusiwa kusoma nakala za Fomu 34A na 34B (fomu za matokeo katika vituo vya kupigia kura na ngazi ya maeneo bunge) ambazo zilitumiwa kutangaza matokeo.
Taarifa kuhusu mchakato wa upinzani kupekua sava na mitambo hiyo ya IEBC itawasilishwa kwa mahakama hiyo kesho jioni.
Majaji saba wa mahakama hiyo ya juu wameanza kusikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa na Bw Odinga leo.
Kwa mujibu wa matokeo ya IEBC, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.

Matokeo na mshindi kila kaunti uchaguzi wa urais 2017

Bofya kwa maelezo zaidi
Chanzo: IEBC

Tarehe muhimu kesi ya kupinga uchaguzi wa rais

  • Agosti 18: Siku ya mwisho ya kuwasilisha kesi
  • Agosti 20: Siku ya mwisho ya kuwasilisha nyaraka za kesi kwa wanaofaa kujibu kesi
  • Agosti 24: Siku ya mwisho kwa wanaofaa kujibu kesi kuwasilisha majibu
  • Septemba 1: Siku ya mwisho kwa Mahakama ya Juu kutoa uamuzi.
Uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kesi hiyo ni wa mwisho. Kwa mujibu wa Katiba ya kenya, iwapo mahakama hiyo itaidhinisha ushindi wa Bw Kenyatta kiongozi huyo ataapishwa kuongoza kwa muhula mwingine tarehe 12 Septemba, siku saba baada ya kutolewa kwa uamuzi.
Iwapo mahakama hiyo itakubali malalamiko ya upinzani na kubatilisha ushindi wa Bw Kenyatta, basi uchaguzi mpya utafanyika katika kipindi cha siku 60 baada ya uamuzi kutolewa, kufikia tarehe 31 Oktoba.