
Kimbunga Harvey kilifika maeneo ya Marekani bara Ijumaa jioni na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Upepo wa kasi ya hadi 130mph (215 km/h) ulipiga maeneo ya pwani ya Texas.
Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kuwahi kupiga maeneo ya Marekani bara katika kipindi cha miaka 13 na kimesababisha uharibifu mkubwa maeneo hayo.
Mji wa Rockport ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi. Magari na majumba yaliharibiwa katika uwanja wa ndege wa mji huo...

...sawa na ndege kadha ndogo.

Mji wa Rockport ulipigwa na kimbunga hicho usiku kucha.




Wakazi wa mji wa pwani Corpus Christi pia waliathirika pakubwa. Nguvu za umeme zilikatika na eneo lote likajaa giza.




Jumamosi, wengi waliamka kupata barabara hazina watu na majumba yameharibiwa. katika baadhi ya maeneo, moto ulizuka.
Lakini uharibifu katika mji huo haukufikia uharibifu ulioshuhudiwa Rockport.


Ijumaa, kabla ya kimbunga kufika bara, watalii wanaopenda kufuatilia vimbunga walikuwa wamefika kwenye fukwe kujionea mawimbi na kupiga picha. Wengi baadaye walikimbilia maeneo salama.

Watu wengi walihama miji na biashara kufungwa kuzuia uharibifu.

Maafisa wameonya kwamba maeneo mengi yatashuhudia mafuriko mabaya katika kipindi cha siku chache zijazo.
Tayari kumetoka mafuriko Galveston.

Na mjini Port Lavaca.

Mjini San Antonio, wanyama pia walihamishwa...

Wakazi wa Houston - mji wa nne kwa wingi wa watu Marekani - wamekuwa wakijiwekea chakula cha akina. Rafu nyingi katika maduka ya jumla hazina bidhaa.

Kimbunga Harvey kimeathiri sana uchimbaji wa mafuta Ghuba ya mexico pamoja na uchukuzi wa ndege.
Asilimia 45 ya usafishaji wa mafuta Marekani hufanyika katika ghuba hiyo.
Tangi la mafuta liliharibiwa akribu na mji wa Seadrift, katika wilaya ya Calhoun.

Picha za Nasa zimeonesha kimbunga hicho kilivyoonekana kutoka anga za juu.

No comments:
Post a Comment