Pia hata zile ambazo zimeingia ndani ya kituo hicho hazijatoka mpaka muda huu
Baadhi ya madereva wa daladala zinazotumia kituo cha mabasi cha Simu-2000 Mawasiliano kuongezewa ushuru kutoka Sh 500 hadi 1000 wakati wa kutoka ndiyo sababu mojawapo iliyofanya wagome.
Mbali na hilo, wamesema ubovu wa barabara hiyo ya Mawasiliano ni sababu nyingi kwa madai ya kwamba magari yao yanaharibika kila kukicha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili walisema walianza mchakato huo tangu saa 11 alfajiri na kwamba wataendeleza hatua hiyo hadi mamlaka husika itakapotoa mwafaka w sinofahamu.
Mmoja wa madereva hao Abdulsalum Hamad amesema waliingia katika kituo kama kawaida lakini wakati wanataka kutoka wakaamriwa kulipa Sh 1000 jambo ambalo hawalukubaliana nalo.
"Baada ya kuamua kugoma kutolipa kiasi hiki walitushirikilia kwa nusu saa ndipo tukachukua uamuzi wa kugoma kabisa na gari itakayoingia hapa kituo haiwezi kutoka kabisa hadi kieleweke,"amesema Hamad
Kero nyingi ya muda mrefu waliaamua kuiunganisha na katika mgomo huo ni hatua ya wahusika wa kituo hicho cha kuwatoza faini ga Sh 50000 pindi wakatapobainika kunawa nyuso wakiwa msalani kwani hawaruhusiwa kufanya hivyo.
Hamad aliwataka wahusika wa kituo kuliangalia suala kwa jicho la tatu suala la tozo ya Sh 1000 kwani huduma zinatolewa na kituo hicho haziendani na tozo hizo na badala yake waiache ya Sh 500.
Wakati sababu hizo zikitajwa, Tanzania ina wastani wa wanawake 3,000 ambao kila mwaka wanapata tatizo la fistula wakati wa kujifungua, huku 1,600 pekee ndio hujitokeza kutibiwa.
Unafahamu fistula huwapata pia wanaume?
Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya njia ya mkojo wamesema ajali, saratani ya kibofu na magonjwa ya njia ya mkojo yamekuwa sababu za kasi ya kukua kwa ugonjwa huo kwa wanaume nchini kwa sasa.
Wakati sababu hizo zikitajwa, Tanzania ina wastani wa wanawake 3,000 ambao kila mwaka wanapata tatizo la fistula wakati wa kujifungua, huku 1,600 pekee ndio hujitokeza kutibiwa.
Akizungumza na Mwananchi jana, daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya njia ya mkojo kutoka Hospitali ya Tumaini, Profesa Cholonde Yongolo alisema japokuwa fistula imekuwa ikijulikana zaidi kwa wanawake, wapo wanaume wanaougua.
Profesa Yongolo alisema zipo saratani ikiwamo ya kibofu ambazo husababisha ugonjwa huo kwa wanaume na wakati mwingine hutoboa hadi njia ya haja kubwa.
“Tatizo la mwanaume kutokwa mkojo bila kujizuia linatokea zaidi kwa walio na saratani ya kibofu,” alisema.
“Mara nyingi saratani hii husababisha kuzalishwa tundu ambalo hutokea njia ya haja kubwa na wakati mwingine mkojo unaweza kuziba mbele hautoki na ukatafuta kupenya kati ya njia ya mkojo na ngozi chini ya hashuo, hiyo ni fistula.”
Alisema wanaume hupata aina nyingi kadhaa za fistula ambazo wakati mwingine hutokana na magonjwa ya zinaa yanayosababisha njia ya mkojo kuota majipu.
Profesa Yongolo alizitaja aina nyingine kuwa ni fistula ya koo na mfumo wa hewa ambayo ni njia ya kumeza na kukohoa, utumbo, kuumia, kupata ajali.
Alisema tundu lolote likitokea kati ya mifumo hiyo, huitwa pia fistula.
“Ni rahisi sana mwanaume kupata fistula ila hawezi kupata kwa njia ya uzazi kwa sababu saratani ya kizazi ni ya wanawake na yenyewe inaweza ikachimba na kutokezea kwenye njia ya haja kubwa au mkojo, lakini ambayo huwapata wote ni ile ya haja kubwa,” alisema Profesa Yongolo.
Sababu za kutokea kwa wanaume
Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya njia ya mkojo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Obadia Nyongole alisema awali kulikuwa na wagonjwa wachache wa fistula kwa wanaume, lakini sasa wanaongezeka .
Alisema hata hivyo, ugonjwa huu huwapata wanawake kwa njia tofauti kwani fistula imegawanyika katika makundi na zipo ambazo mtu huzaliwa nazo.
“Mara nyingi huwepo tundu linalounganisha kiungo kimoja na kingine ambalo kwa kawaida halitakiwi kuwepo, zipo fistula ambazo mtu anazaliwa nazo katika maumbile kunakuwa na viungo ambavyo vimetengeneza muungano usio rasmi na kuna tundu linalounganisha,” alisema Dk Nyongole.
Alifafanua kuwa zipo ambazo hutokana na matibabu ya upasuaji. “Ikiwa likatokea tundu kwenye kiungo kingine na katika kupona likashindwa kupona vizuri au katika kufanya upasuaji kuna kiungo kiliguswa na kifaa kingine bila kugundulika wakati wa upasuaji kikaachwa hivyo hivyo, kinaweza kutengeneza fistula hasa sehemu ya utumbo,” alisema.
Alisema wengi wanaopata fistula ni wale waliofanyiwa upasuaji kwa njia ya mkojo wakawekewa mpira baada ya kutolewa kuna kovu ambalo hutakiwa lipone lenyewe, ikishindikana mkojo huanza kutokea tumboni chini ya kitovu sababu tundu limeshindwa kuziba.
“Wapo wanaopata kovu kwenye njia ya mkojo na litakaposhindwa kutibiwa kwa wakati hivyo patatengeneza jipu na baadaye likipasuka na kutengeneza njia, ni fistula kwa mwanaume,” alisema Dk Nyongole.
Atumia maadhimisho ya chama chake kuzungumzia mgogoro wa CUF
Wakati mgogoro wa uongozi kati ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi ukishika kasi, Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed amesema mgogoro huo unakolezwa na Maalimu Seif kutokana na kung’ang’ania madaraka.
Akizungumza kwenye madhimisho ya miaka mitano ya ADC yaliyofanyika kwenye Makao Makuu yake Buguruni, Hamad alisema hatua hiyo inasababishwa na kutanguliza maslahi binafsi.
Hamad alisema kiongozi mzuri ni yule anayeendena na maneno yake kwa wanachama na wananchi, ili kuweza kujenga chama kama taasisi siyo chama cha mtu mmoja.
Hamad badala ya kuzungumzia maadhimisho ya chama chake, alijikita zaidi kwenye mgogoro wa CUF.
Pia, alisema hawataki viongozi wanaokipaka matope chama chake kwa kukiita CCM B. Alisema sera yao ni kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu kwa wanachama wake, ili kupata muda wa kuendeleza demokrasia inayoleta mabadiliko.
“Katika chama chetu hatuna sera ya vurugu wala migogoro binafsi hatukubali hata kidogo, mtu kutuharibia chama chetu. Kiongozi huwezi kufanya kazi kwenye fitina,” alisema.
Alisema kiongozi yeyote hawezi kuongoza chama au wananchi iwapo kuna migogoro inayosababishwa na viongozi wachache.
“Chama chetu hatuwezi kumvumilia kiongozi muongo tunaamini uongozi unaweza kupatikana katika sehemu mbili za mabadiliko na uchanguzi, hatutaki kufanya mabaya yanayofanyika kwenye vyama vingine,” alisema.
Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo alisema ADC siyo chama cha vurungu kutokana na wao kuamini maendeleo hayawezi kupatikana kwa maandamano,
Pia, Doyo alisema kitendo cha viongozi kushindwa kuelewana ndani ya chama, ni jambo ambalo linaleta picha mbaya na kurudisha nyuma maendeleo ya ujenzi wa demokrasia.
“Tuna uwezo wa kusameheana iwapo kumetokea mtafaruku, tunawataka wanachama wote kufanya hivyo katika matawi yao,” alisema Doyo.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionManowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore
Wanajeshi 10 hawajulikani waliko na wengine watano wamejeruhiwa baada ya manowari ya jeshi la Marekani kugongana na meli ya kubeba mafuta pwani mwa Singapore, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji la Marekani.
Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati iligongana na meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia.
Shughuli kubwa ya kuwatafuta na kuwaokoa wanajeshi inaendelea.
Ndicho kisa cha pili kikubwa kinachoikumba meli ya jeshi la wanamaji wa Marekani miezi ya hivi karibuni.
Ripoti zinasema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu upande wake mmoja, lakini jeshi la Marekani lilsema kwa inaelea peke yake kwenda bandari ya Singapore.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionManowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore
Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singapore pamoja na walinzi wa pwani, wanafanya shughuli za uokoaji. Malaysia nayo imejiunga katika shughuli hiyo.
Kura taarifa kidogo kuhusu hali ya meli ya mafuta ya Alnic MC na wahudumu wake.
Image captionManowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini
Meli hiyo ya mafuta inaripotiwa kuwa na uzito mara tatu wa manowari ya jeshi ya USS John McCain, na taarifa zinasema kuwa haikuwa imebeba mafuta wakati ya ajali hiyo.
Seneta John McCain ambaye jina lake limepewa manowari hiyo, aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa yeye na mke wake wanawaombea mabaharia hao.
Mwezi Juni mabaharia saba wa Marekani waliuawa wakati manowari ya USS Fitzgerald iligongana na meli ya mizigo kwenye bahari ya Japan karibu na bandari ya Yokosuka.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha.
Zaidi ya wataalamu 100 wa teknolojia ya roboti wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ili kuzuia kundwa wa roboti zinazoweza kuua.
Kwenye barua kwa Umoaj wa Mataifa, wataalamu wa masuala ya teknolojia akiwemo tajiri Elon Musk, wameonya kuwa hatua hiyo itasababisha kuwepo kwa vita vitakavyohusisha roboti.
Wataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha.
"Wakati zitaundwa, zitawezesha vita kupiganwa kwa kiwango kingine cha juu na kwa haraka zaidi kuliko vile binadamu hufanya." barua hiyo ilisema.
"Hizi zitakuwa silaha za ugaidi, silaha ambazo magaidi watatumia dhidi wa watu wasio na hatia, na silaha ambazo zitadukuliwa kuhudumu kwa njia ambayo sio nzuri." iliongeza.
Mwaka 2015 zaidi ya wataalamu 1,000 na watafiti waliandika barua wakionya kuhusua kuundwa kwa silaha kama hizo.
Kati ya wale walioweka sahihi barua ya mwaka 2015 ni mwanasayansi Stephen Hawking, na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple Steve Wozniak na bwana Musk.
Roboti za kuua ni zipi?
Roboti za kuua ni silaha ambazo zinaweza kuchagua na kuvamia kitu ambacho zinakilenga bila ya kuelekezwa na binadamu. Tayari kwa sasa zipo lakini kuboreshwa zaidi kwa teknolojia itachangia kuziwezesha kufanya hivyo.
Wale wanaopendelea roboti hizo wanaamini kuwa sheria za sasa za vita zinatosha kutatua shida yoyote ambayo itaibuka ikiwa zitatumiwa.
Lakini wale wanaozipinga wanasema kwa roboti hizo ni tisho kwa binadamu na teknolojia yoyote ya kuziwezesha kuuwa inastahili kupigwa marufuku.
Idhaa mpya ya utangazaji ya BBC, ambayo itakuwa ikipeperusha taarifa kupitia mtandao, imezinduliwa leo ambapo itatumia lugha ya Pidgin kutangazia wakazi wa Afrika Magharibi na Kati.
Pidgin ni moja ya lugha zinazozungumza zaidi katika kanda hiyo, ingawa haijatambuliwa rasmi.
Uzinduzi wa idhaa hiyo ni sehemu ya upanuzi mkubwa wa BBC World Service, kitengo cha shirika la BBC kinachohusika na utangazaji nje ya Uingereza, tangu miaka ya 1940.
Upanuzi huo unatokana na ufadhili wa serikali ya Uingereza ambao ulitangazwa 2016.
Pidgin itafuatwa hivi karibuni na idhaa 10 nyingine mpya katika bara la Afrika na bara Asia.
BBC World Service pia inapanga kuandaa makala zaidi za video na za kusomwa kwa kutumia rununu na pia kuangazia zaidi mitandao ya kijamii.
Kadhalika WS inapanga kuboresha matangazo yake ya runinga kore barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kuanzisha zaidi ya vipindi 30 vipya vya runinga vya kupeperushwa na vituo washirika Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
Matangazo ya Idhaa ya Kiarabu na Idhaa ya Kirusi pia yataboreshwa chini ya mradi wa 2020.
Pidgin ni nini?
· Ni mchanganyiko wa lugha ya Kiingereza na lugha za asili ambao huwezesha watu wasiokuwa na lugha moja kuwasiliana.
· Kiingereza cha Pidgin Afrika Magharibi ilikuwa ndiyo lugha ya biashara iliyozungumzwa katika maeneo ya pwani wakati wa biashara ya utumwa katika bahari ya Atlantiki mwishoni mwa karne ya 17 na karne ya 18.
· Lugha hii hutumiwa sana Nigeria, Ghana, Cameroon na Equatorial Guinea
· Kimsingi ni lugha ya kutamkwa na kuzungumzwa, lakini hakuna aina ya kuandikwa ya lugha hii ambayo imeafikiwa.
'Kuvuka mipaka'
Ni vigumu kufahamu idadi hasa ya watu wanaozungumza lugha ya Pidgin, kwani huwa haifundishwi rasmi shuleni na pia wazungumzaji huifahamu kwa viwango tofauti.
Lakini nchini Nigeria, inakadiriwa kwamba watu kuanzia milioni tatu hadi milioni tano huitumia kama lugha yao ya kwanza katika shughuli zao za kila siku.
Inadaiwa kuwa lugha ya pili kwa watu karibu 75 milioni nchini Nigeria pekee, nusu ya raia wote.
Na pia huzungumzwa sana katika nchi nyingine katika kanda hiyo.
"Ni lugha ya biashara na mawasiliano isiyo rasmi. Ni lugha ambayo huwaunganisha watu na huvuka mipaka na vizuizi vyote - kikabila, kikanda na kijamii na kiuchumi," anasema
Bilkisu Labaran, mhariri anayeongoza idhaa hiyo mpya.
Ingawa kuna kituo cha redio kinachotumia Pidgin pekee, kituo cha Wazobia FM ambacho kilianzishwa miaka 10 iliyopita, BBC itakua ya kwanza kuanzisha tovuti na kuwa na mitandao ya kijamii.
Hili sana hutokana na kwamba si lugha iliyo rasmi, na hadi sasa hakuna aina iliyoafikiwa ya kuandika lugha hiyo.
" BBC itakuwa mwasisi katika hili," anasema Bi Labaran, mzungumzaji mzuri wa Pidgin.
Anatarajia changamoto - lakini pia kuna fursa kutokana na mjadala unaotarajiwa kuhusu kulainisha lugha hiyo, kuandikwa na kuzungumzwa kwake.
Kutakuwepo na nini?
BBC Pidgin itakuwa na mseto wa habari na makala za uchanganuzi wa kina zitakazoangazia matukio katika nchi ambazo lugha hiyo huzungumzwa na pia kimataifa - italeta ulimwengu kwa kanda hiyo, na kuiwasilisha kanda hiyo kwa ulimwengu.
Shirika hilo la utangazaji linasema idhaa hiyo ya dijitali pia itaangazia kuwavutia wasikilizaji na wasomaji wa umri mdogo pamoja na wanawake, ambapo mitandao ya kijamii itakuwa na mchango muhimu.
Kwa hivyo, hali kadhalika, kutakuwa na "Makala kuhusu utamaduni, burudani, ujasiriamali, sayansi na teknolojia, afya na michezo - ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu ya England".
Kitovu cha idhaa hii kitakuwa Lagos, mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria, lakini kutakuwepo na waandishi nchini Ghana na Cameroon pamoja na Nigeria kwenyewe, ambao watakuwa mashinani wakitafuta habari na makala.
Aidha, pamoja na Pidgin, raia wa Nigeria hivi karibuni watapokea idhaa nyingine mpya za Yoruba na Igbo , ambazo zitasaidia kuwafikia watu zaidi ya wanaofikiwa na Idhaa ya Kihausa na Kiingereza.
Idhaa hii mpya ya Pidgin itaanza kupeperusa rasmi taarifa na Makala kuanzia saa 0001GMT (saa kumi alfajiri Afrika Mashariki) siku ya Jumatatu 21 Agosti.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionWashambuliaji wa Barcelona walikuwa na mitungi 120 kufanyia mashambulizi
Washukiwa wa ugaidi ambao waliendesha mashambulilizi nchini Uhispania walikuwa wamekusanya mitungi 120 na walikuwa wakipanga kuitumia kwenye mashambulizi ya magari, kwa mujibu wa polisi nchini Uhispania.
Mitungi hiyo ilipatikana ndani ya nyumba ambayo inadaiwa kutumiwa na magaidi hao katika mji wa Alcanar siku ya Jumatano usiku.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWashambuliaji wa Barcelona walikuwa na mitungi 120 kufanyia mashambulizi
Polisi bado wanamtafuta dereva wa gari ambalo liligonga watu kadha katika eneo la Las Ramblas mjini Barcelona na kuwaua 13.
Leo Jumapili misa ilifanyika mjini Barcelona kuwaomboleza waathiriwa.
Kando na watu 13 waliouawa siku ya Alhamisi huko Las Ramblas, mwanamke mwingine aliuawa wakati wa shambulizi la pili la gari mapema Ijumaa katika mji wa Cambrils.
Image captionWashambuliaji wa Barcelona walikuwa na mitungi 120 kufanyia mashambulizi
Washukiwa watano magaidi waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye shambuliza hilo la pili.
Polisi wamethibitisha kuwa bado wanamsaka Younes Abouyaaqoub, mzaliwa wa Morocco, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania.
Haki miliki ya pichaAFPImage caption(kutoka kushoto) Moussa Oukabir, Said Aallaa, Mohamed Hychami na Younes Abouyaaqoub
Haki miliki ya pichaAFPImage captionUSS Indianapolis - picha ya mwaka 1937
Manowari ya jeshi la Marekani ya USS Indianapolis ambayo ilizama wakati wa vita vya pili vya dunia, imepatikana kwenye bahari ya Pacific, Miaka 72 baada ya kuzamishwa na nyambizi wa Japan.
USS Indianapolis ilikuwa ikirejea kutoka oparesheni ya siri ya kupeleka sehemu za kunda bomu la atomic ambalo baadaye lilitumiwa huko Hiroshima.
Manowari hiyo ilipatikana kilomita 5.5 chini ya bahari.
Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Paul Allen, ambaye aliongoza kikosi cha kutafuta manowari hiyo alisema ugunduzi huo ni wa kutia moyo.
USS Indianapolis iliharibiwa tarehe 30 Julai mwaka 1945 katika habari ya Ufilipino kati ya Guam na Leyte baada ya kugongwa na kombora kutoka kwa nyambizi ya Japan.
Image captionPicha ya Indianapolis baharini
Kilikuwa kisa kibaya zaidi cha kupotea kwa maisha kulikumba jeshi la wanamaji wa Marekani.
Kulikuwa na wanajeshi 1,196 ndani ya manowari hiyo na ni kati ya wanajeshi 800 na 900 walinusurika kuzama.
Lakini manowari hiyo haikutuma ishara na hadi wakati masura walipatikana siku nne baadaye ni watu 316 tu waliopatikana wakiwa hai katika eneo hilo lenye papa wengi.
Meli hiyo ni maarufu kwa kufanya safari ya siri ya kusafiirjha sehemu za kuunda bomu la atomic lilifahamika kama "Little Boy" .
Image captionSehemu za USS Indianapolis
Bidhaa hizo zilipelekwa katika kisiwa cha Tinian kwenye kambi ya jeshi la Marekani ambayo ilifanya shambulizi la kwanza na bomu la nyuklia.
Siku nne baadaye Indianapolis ilizama chini ya wiki moja kabla ya bomu hilo la nyuklia ililosaidia kuunda kuharibu mji wa Hiroshima.
Sawa na bomu lenye jina "Fat Man" lililoangushwa mji wa Nagasaki, ambalo liliilazimisha Japan kuachana na vita na kumalizika kwa vita vya pili vya Dunia.
Image captionIdadi ya watu waliouawa kwenye maporomo ya ardhi DRC kuongezeka hadi 200
Idadi ya watu ambao wameuawa kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, huenda ikapanda hadi kufikia watu 200, maafisa wamesema.
Watu ambao walikufa ni kutoka jamii ya wafugaji katika ziwa Albert.
Maafisa wanasema kuwa idadi hiyo ni kutokana na idadi ya familia zilizofukiwa baada ya mvua kubwa kusababisha sehemu za mlima ulio karibu kuporomoka.
Matumaini ya kuwapata manusura yamedidimia wakati waokoaji wakiwa hawana njia za kuondoa mawe makubwa.
"Kuna watu wengine zaidi waliofukiwa ambao hatuna uwezo wa kuwakoa," naibu gavana wa mkoa wa Ituri aliliambia shirika la Reuters.
Milima nayo inasababisha eneo hilo kutofikika kwa urahisi.
Sehemu nyingi za magharibi na kati kati mwa Afrika zinakubwa na maporomoko ya ardhi kwa sababu miti imekatwa sana na jamii zimesongamana kwenye maeneo yaliyo chini ya milima.
Mashariki mwa Congo ni eneo ambalo pia hukumbwa na mitetemeko ya ardhi.
Zaidi ya watu 400 wameuawa huku 600 wakiwa hawajulikani waliko baada ya janga kama hilo kuikumba Sierra Leone.