Akizungumza kwenye madhimisho ya miaka mitano ya ADC yaliyofanyika kwenye Makao Makuu yake Buguruni, Hamad alisema hatua hiyo inasababishwa na kutanguliza maslahi binafsi.
Hamad alisema kiongozi mzuri ni yule anayeendena na maneno yake kwa wanachama na wananchi, ili kuweza kujenga chama kama taasisi siyo chama cha mtu mmoja.
Hamad badala ya kuzungumzia maadhimisho ya chama chake, alijikita zaidi kwenye mgogoro wa CUF.
Pia, alisema hawataki viongozi wanaokipaka matope chama chake kwa kukiita CCM B. Alisema sera yao ni kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu kwa wanachama wake, ili kupata muda wa kuendeleza demokrasia inayoleta mabadiliko.
“Katika chama chetu hatuna sera ya vurugu wala migogoro binafsi hatukubali hata kidogo, mtu kutuharibia chama chetu. Kiongozi huwezi kufanya kazi kwenye fitina,” alisema.
Alisema kiongozi yeyote hawezi kuongoza chama au wananchi iwapo kuna migogoro inayosababishwa na viongozi wachache.
“Chama chetu hatuwezi kumvumilia kiongozi muongo tunaamini uongozi unaweza kupatikana katika sehemu mbili za mabadiliko na uchanguzi, hatutaki kufanya mabaya yanayofanyika kwenye vyama vingine,” alisema.
Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo alisema ADC siyo chama cha vurungu kutokana na wao kuamini maendeleo hayawezi kupatikana kwa maandamano,
Pia, Doyo alisema kitendo cha viongozi kushindwa kuelewana ndani ya chama, ni jambo ambalo linaleta picha mbaya na kurudisha nyuma maendeleo ya ujenzi wa demokrasia.
“Tuna uwezo wa kusameheana iwapo kumetokea mtafaruku, tunawataka wanachama wote kufanya hivyo katika matawi yao,” alisema Doyo.
No comments:
Post a Comment