Wednesday, April 4

Spika Ndugai arejea nchini


Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Job Ndugai amerejea leo Aprili 3, 2018 akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya kupata matibabu miezi miwili.
Akizungumza na Mwananchi leo Aprili 3, 2018, Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema, “Mimi sijaonana naye, ila ninazo taarifa za Spika Ndugai amerejea leo na bado yuko Dar es Salaam hajaja Dodoma.”
Katika picha inayosambaa mitandaoni inamwonyesha Spika Ndugai akisalimiana na Mke wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete pamoja na wabunge wengine wakiwa na nyuso za tabasamu.

No comments:

Post a Comment