Katibu wa kamati ya maandalizi Thomas Tlanka alisema baada ya kumalizika mashindano hayo, wanariadha wenye viwango bora wataitwa timu ya Taifa.
Tlanka alisema Mkoa wa Arusha wameandaa mashindano hayo ili kupata wanariadha bora ambao watakuwa hazina kwa Taifa katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Hakuna siri Arusha ikilala ni vigumu kupata timu bora ya riadha, ushahidi upo hata timu iliyokwenda Australia asilimia kubwa wanariadha wake wanatoka Arusha,” alisema Tlanka.
Mratibu huyo alisema wanariadha watachuana katika awamu ya kwanza Aprili 7 na mchujo wa pili utafanyika Aprili 28 kabla ya kuhitimisha Mei 5.
Tlanka mkakati wa mkoa huo timu ya Taifa inaundwa na idadi kubwa ya wanariadha wa Arusha watakaoshiriki mashindano ya mbio fupi na ndefu.
Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha wanariadha wasiozidi umri wa miaka 19 katika mbio za uwanjani mita 100, 200, 400, 800, 1500, 5000 na 10,000.
No comments:
Post a Comment