Saturday, March 10

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa waache kucheza karata


Lindi. Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Lindi mjini, kimewataka vijana kutumia fursa zilizopo ikiwamo ardhi kuendesha uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, badala ya kushinda vijiweni.
Mwenyekiti wa CCM Lindi mjini, Abdallah Madebe alisema hayo wakati wa uzinduzi wa ugawaji miche mipya ya mbegu ya mikorosho kwa wakulima wa kata ya Tandangongoro.
Madebe alisema wakati umefika kwa vijana wa Lindi kuacha kushinda vijiweni wakisubiri kila kitu kufanyiwa na Serikali, badala yake wajitokeze kuchukua maeneo ya kilimo.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Tandangongoro,Ally Hemedi akipokea miche hiyo kwa niaba ya wakulima wake, alipongeza mpango huo wa manispaa wa kubuni mradi huo na kuwapatia miche hiyo bure kwa kuwa utawasaidia kuongeza kipato.
Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Mrisho Satura alisema zaidi ya heka 40,000 na miche milioni moja imeshatengwa kugawiwa (Mwanja Ibadi)

No comments:

Post a Comment