Tuesday, March 6

Shepherd Bushiri: Nabii kutoka Malawi anayedai kutenda miujiza na kuwavutia maelfu ya waumini

Bushiri anasema utajiri wake unatokana na Biashara zake binafsiHaki miliki ya pichaECG MINISTRIES
Image captionBushiri anasema utajiri wake unatokana na Biashara zake binafsi
Watu wanapiga makofi, wanacheza, kuimba na kuruka wakati akielekea kwenye ukumbi, akiwa amezungukwa na walinzi. Lakini kwa nini wasifanye hivyo?
Huyu ni mwanaume anayesema kuwa ana dawa ya walioathirika na virusi vya Ukimwi, HIV, anawaponya vipofu, maskini wanakuwa matajiri, na wakati mmoja hivi karibuni anadaiwa kuonekana akitembea hewani
Nabii Mchungaji Bushiri alizaliwa na kulelewa mjini Mzuzu kaskazini mwa Malawi.
Siku hizi, hujaza viwanja vya michezo kwa maelfu ya watu walio wafuasi wake, wafuasi ambao wako tayari kusafiri hadi popote pale duniani kwa ajili ya kumtazama akihubiri yeye mwenyewe.
Amekuwa akitembelewa mara kwa mara na wageni kutoka Marekani, Uingereza hata bara la Asia.
Leo Bendera zao zinapepea kwa mbwembwe ndani ya ukumbi wa kanisa la Enlightened Christian Gathering (ECG). Maana ya jina la kanisa hilo ni Mkusanyiko wa Wakristo Walioongoka
Nakutana na mtu huyu anayefahamika kwa jina ''Mkuu'' ndani ya Kanisa mjini Pretoria Afrika Kusini.
Tulipokewa kuelekea mahala patakatifu, pakiwa pametandikwa kitambaa chekundu na zulia jekundu pembeni wamejipanga walinzi.
Kumponya mlemavu
Mhubiri huyu mwenye miaka kama 30 na zaidi hivi anafahamu fika kuhusu shutuma dhidi yake baadhi ya watu wakimuita msanii na mhubiri bandia, lakini amekua akizipuuzilia mbali haya yote.
''Kanisa langu si kwa ajili ya kila mtu, isipokuwa kwa wale wanaoamini," alinieleza.
''Mimi ni mjumbe wa kazi ya Mungu. Mungu huwaponya watu kwenye kusanyiko letu''.
''Kuna siku nilikuwa na madaktari hapa Pretoria walileta watu wenye virusi vya Ukimwi, waliwapima kabla kuthibitisha kuwa wameathirika. Niliwaombea na sasa hawana virusi tena."
Bidhaa za Nabii Bushiri 'mafuta ya muujiza huuzwa nje ya KanisaHaki miliki ya pichaECG MINISTRIES
Image captionBidhaa za Nabii Bushiri kama vile mafuta ya muujiza huuzwa nje ya Kanisa
Nje ya chumba, wafuasi wanakubaliana.
Wanaamini si tu mchungaji huyu kajazwa na nguvu ya utume, lakini pia ana nguvu ya kuponya wanaougua na kuwaombea watu kuwa na mafanikio.
''Miujiza na mafundisho ambayo baba yetu (Nabii Bushiri) hufundisha kila juma ni ya kustaajabisha,'' anasema Xolani Msibi (24).
Alisema dada yake alikuwa na shida ya kutembea na kuwa aliponywa na nabii ''bila hata kumuwekea mkono''
''Mwenyewe nimekuwa nikihangaika kupata kazi na nilikuja hapa nikapata kazi mbili kwa wakati mmoja ilikuwa suala la kuchagua tu''.
Wahubiri wengine wanaodai kufanya miujiza
Wanawake na wanaume wanaodai kufanya miujiza hawako Afrika Kusini pekee au Afrika pekee-wanapatikana katika maeneo mengi duniani.
Benny Hinn, Kiongozi wa Kanisa la Israel lililo na makazi yake nchini Marekani,Grace Copeland na Rienhard Bonnke wa Ujerumani, hao ni wachache tu.

'Baraka zimewavuta wafuasi wangu'

Kwa siku ya kawaida, Jumapili kanisani kwa Bushiri, watu takriban 40,000 hukusanyika kumsikiliza Nabii akihubiri, kisha hununua bidhaa zinazouzwa kanisani kama vile'' mafuta ya muujiza', kalenda, vibandiko vya mkononi na taulo zeye picha, fulana na kofia, vyote vikiwa na picha ya uso wake.
Wauzaji huwaambia wanunuzi kuwa bidhaa zote hizo zimeombewa na Bushiri mwenyewe na vina nguvu ya uponyaji.
Moja ya Ndege binafsi za Nabii BushiriHaki miliki ya pichaECG MINISTRIES
Image captionMoja ya ndege za kibinafsi za Nabii Bushiri
Kwa miaka mingi Bwana Bushiri amejipatia utajiri mkubwa.
Vipi kuhusu wanaohoji amepata wapi pesa zote hizo?
"Ubaguzi wa rangi huo," anasema.
Presentational grey line
Shepherd Bushiri ni nani?
Prophet Sherpherd BushiriHaki miliki ya pichaECG MINISTRIES
  • Ni "nabii" mzaliwa wa Malawi aliye na makanisa mataifa mengi Afrika, miongoni mwake Ghana na Afrika Kusini
  • Anadaiwa kupigwa marufuku Botswana kutokana na "pesa za mwujiza"
  • Anadai kwamba amewatibu watu wenye Ukimwi
  • Alidaiwa kutembea angani kwenye video iliyosambazwa sana mitandao ya kijamii
  • Ana ndege nne za kibinafsi
Presentational grey line
Hakuna hasa rekodi ya utajiri wake wote lakini inafahamika amekuwa akipata faida kwenye migodi kadhaa na anamiliki ndege binafsi na hoteli kadhaa kwa jina la kampuni yake ya uwekezaji Shepherd Bushiri Investments, makao makuu yake yakiwa Johannesburg.
Suala la yeye kupata utajiri huo kwa madai ya ujasiriamali haliaminiki
Mwenyewe alisema ''Mimi ni mfanyabiashara. Hiyo ni kando na kuwa Nabii. Mafanikio yamekuja kutokana na biashara zangu binafsi.
"Maswali ya namna hiyo hayaulizwi viongozi wa makanisa ya Wazungu, lakini Mwafrika akifanikiwa ni tatizo."
Kisha kidogo anaonyesha kuchukizwa, anaongeza ''inakuwaje kuuza bidhaa kanisani mwangu iwe tofauti na kanisa katoliki kuuza Rozari na makanisa ya Uingereza kuuza Biblia? hii si sawa."
"Kufanikiwa kwangu ni kioo kwa wafuasi wangu. Wanafikiri kama Mungu anaweza kunitendea mimi, anaweza kuwatendea wao pia. Kama waliamini kuwa kuna shida kwenye hilo basi wasingenifuata''.

Kupokea vitisho

Amekuwa akipokea vitisho kwa wale wanaomuona kuwa mshindani wao, wengine wamekuwa na wasiwasi namna ambavyo watu wamekuwa wakitumia pesa kwenye kanisa.
Kumekuwa na sheria nchini Afrika Kusini kuhusu makanisa ya kisasa, nako nchini Botswana Kanisa la Bushiri limefungwa kutokana na kutumia ''pesa za muujiza'' ambako kunakiuka sheria za matumizi ya pesa nchini humo.
Nabii Bushiri ana maelfu ya wafuasi, hapa walikusanyika kwenye uwanja wa watu 95,000Haki miliki ya pichaECG MINISTRIES
Image captionNabii Bushiri ana maelfu ya wafuasi, hapa walikusanyika kwenye uwanja unaotoshea watu 95,000
Thoko Mkhwanazi-Xaluva ni mkuu wa Tume ya kulinda tamaduni, dini na lugha ndani ya jamii. Hivi karibuni alitoa ripoti kuhusu kuchipuka kwa makanisa mengi ambayo yamekuwa maarufu barani Afrika.
"Tumegundua kuwa baadhi ya makanisa yamekuwa yakijipatia faida kutokana na bidhaa za imani zinazonunuliwa na watu maskini wenye shauku ya kubadilisha maisha yao kuwa mazuri," anaeleza
Ripoti hiyo imeeleza zaidi kuwa kuna vitendo vinavyofanywa visivyo salama kwa waumini kama vile kula Panya, Nyoka, Majani na kunywa mafuta ya petroli kuwapima imani yao.
Pia kumekuwa na shutuma za udhalilishaji wa kijinsia kwa baadhi ya makanisa.
Hata hivyo Mkuu huyo anasema suala la dini ni uamuzi wa mtu mwenyewe.

No comments:

Post a Comment