Tuesday, March 6

Olympic yafungua mazungumzo kati ya Seoul, Pyongyang



Ujumbe maalum wa Korea Kusini wakati ukiwa uwanja wa ndege tayari kwa safari ya Pyongyang, Korea Kaskazini
Ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Korea Kaskazini Moon Jae-in umeripotiwa kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Jumatatu.
Ripoti za vyombo vya habari zimesema kuwa Kim aliandaa chakula cha usiku kwa heshima ya ugeni huo kutoka Korea Kusini.
Ujumbe huo wa watu 10 ambao umeongozwa na mshauri wa juu wa usalama wa taifa wa Moon, Chung Eui-Yong, uliwasili Pyongyang baada ya usafiri wa nadra wa ndege kufanyika kutoka Seoul.
Mkurugenzi huyo wa usalama wa taifa wa Korea Kusini amesema: ili kuendeleza wimbi la maelewano kupitia mazungumzo ya pamoja na mahusiano yaliopo hivi sasa kufuatia michezo ya kipindi cha baridi ya Olympic iliofanyika Pyeongchang, bila shaka tutafikisha ujumbe kutoka kwa Rais Moon kuwa ana nia ya dhati na utayari wa kuondosha silaha za nyuklia kutoka katika Rasi ya Korea na kufikia amani ya kweli na ya kudumu.
Chung amesema kuwa ataendeleza juhudi za kuwepo mazungumzo “ya kina” ili kutafuta njia ya kufanya matayarisho ya kuanza mazungumzo kati ya Pyongyang na Washington.
Harakati hizo zinaweza kukabiliwa na ugumu wa aina fulani kwa kuwepo mazoezi ya kijeshi yaliokwisha pangwa, lakini, kwa mujibu wa maoni yaliyochapishwa na Shirika la habari la Korea Kaskazini rasmi KCNA limetahadharisha kuwa Pyongyang “itakabiliana na Marekani” iwapo watafanya mazoezi ya kivita na Korea Kusini mwezi wa April.
Baada ya ziara hiyo ya siku mbili nchini Korea Kaskazini, ujumbe maalum kutoka Korea Kusini utasafiri kwenda Marekani ili kuwapa muhtasari maafisa wa serikali ya Marekani juu ya mazungumzo yaliojiri huko Pyongyang.
Hatua hiyo ya kupeleka ujumbe maalum Pyongyang, Moon alikuwa anarejesha ukarimu uliofanywa na Kim Jong Un katika uamuzi wake wa kupeleka ujumbe wa ngazi ya juu, akiwemo dada yake, Kim Yo Jong kuhudhuria michezo ya Olympics huko Pyeongchang.
Maafisa hao wa Korea Kaskazini walimwambia Moon kuwa wako tayari kuanza mazungumzo na Marekani, lakini Rais Donald Trump alijibu wito huo kwa kusema kuwa mazungumzo yatafanyika tu “katika hali inayoridhisha.”

No comments:

Post a Comment