Mfanyakazi wa Ndege aliyeanguka kwenye mlango wa dharura wa ndege kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda ameaga dunia, BBC imeelezwa
Mwanamke huyo ambaye uraia wake haujabainishwa, alikimbizwa Hospitali ya Kisubi umbali wa Kilomita 16 lakini alipoteza maisha baadae,Msemaji wa Shirika la Emirates alieleza.
Ripoti zinasema kuwa tukio la kuanguka lilitokea wakati mhudumu huyo alipokuwa akiandaa ndege kwa ajili ya kupandisha abiria.
Mamlaka ya anga nchini Uganda imesema inafanya uchunguzi.
Imesema katika taarifa yake kuwa mhudumu huyo ''alikuwa amefungua mlango wa dharura'' na ''bahati mbaya'' alianguka nje ya ndege hiyo iliyokuwa imepaki baada ya kutua
Msemaji wa hospitali ya Kisubi, Edward Zabonna ameiambia BBC kuwa mfanyakazi huyo alikuwa na majeraha ''usoni mwake na miguuni''
Alisema alikuwa'' amepoteza fahamu lakini alikuwa hai'' alipowasili hospitalini, siku ya Jumatano jioni lakini alifariki muda mfupi baadae.
Shirika la Habari la Ufaransa limenukuu taarifa ya Emirates ikisema ''Mfanyakazi wetu bahati mbaya alianguka kutoka kwenye mlango uliokuwa wazi wakati akiandaa ndege kwa ajili ya abiria kuingia.
Shirika hilo limesema litatoa ushirikiano kwa uchunguzi utakaofanyika.
No comments:
Post a Comment