Saturday, March 31

Mbwa wa polisi Uhispania kuchezewa muziki kuwaepushia msongo wa mawazo

Polisi wa manispaa wa Madrid wakiwa pamoja na mbwaHaki miliki ya pichaMADRID MUNICIPAL POLICE
Image captionMfumo waliowekewa mbwa wa madrid unatoa muziki wa aina ya classic mara kadhaa kwa siku unaofahamika kama ''Mozart effect.
Mbwa wa polisi wa manispaa ya Madrid wanatarajiwa kupata kiyoyozi kwenye vyumba vyao na pia kuchezewa muziki kama njia ya kuboresha mazingira yao ya kikazi.
Polisi wa manispaa kuu ya Uhispania wamewekeza katika mfumo maalumu unaotoa muziki wa kuwaliwaza mbwa hao wanaotoa huduma ya usalama katika manispaa hiyo.
Manispaa inamatumaini kwamba mfumo huo mpya utapunguza viwango vya msongo wa mawazo ambao unaowapata mbwa.
Mfumo huo unaotoa muziki wa aina ya classic mara kadhaa kwa siku unaofahamika kama ''Mozart effect.''
Mbwa hao 22 wanafanya kazi ya upelelezi katika nyanja tofauti katika kikosi cha polisi wa manipaa hiyo.
Baraza hilo la Madrid, ambalo linaangazia maswala ya walinzi hao, limesema mbwa hao hukumbana na viwango vikubwa vya msongo wa mawazo kutokana na kazi yao.
Vifaa hivyo vimewekwa kama njia ya kuboresha sehemu ambazo mbwa hao wanapoishi.
Mbwa katika kitengo hicho wanautaalam wa kuchunguza vilipuzi au dawa za kulevya na husaidia katika shughuli za uokozi yanapotokea majanga na ajali.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la tabia za wanyama-Veterinary Behavior manamo mwaka 2012 ulibainisha kwamba muziki aina ya classic unauwezo wa kuwasaidia mbwa kupunguza wasiwasi.
Sajenti wa polisi Rafael de la Gándara,anayeongoza kitengo hicho amesema uboreshaji wa makazi ya mbwa utawasaidia kuimarisha hali zao za maisha na kazi wanayoifanya.
Mbwa wa MadridHaki miliki ya pichaMADRID MUNICIPAL POLICE
Image captionMbwa hawa wana uwezo wa kubaini dawa za kulevya na vilipuzi na husaidia katika shughuli za uokozi
Alisema mbwa hao wanahitaji mapumziko na kuchangamshwa ili wawe macho na waweze kufuata maagizo ya kamanda wanapokuwa kazini na kutekeleza wajibu wao wanapohitajiwa kwa kazi ya dharura.
''Mfano, endapo mbwa anatafuta dawa za kulevya , huchimba chini ardhini , kwa kweli si jambo jema iwapo anatafuta vilipuzi,'' alisisitiza Sajenti de la Gándara.
Uboreshaji wa makazi yao pia ulijumuisha kuwekwa kwa viyoyozi kuhakikisha hawaathiriwi na jua linaloambatana na joto wakati wa majira ya joto na kuwalinda na baridi nyakati za majira ya baridi.

No comments:

Post a Comment