Mkuu wa wilaya hiyo, Chelestino Mofuga ameyasema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi wa maeneo hayo, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo.
Mofuga amesema vituo hivyo vitatu vya afya kwa pamoja vimepewa Sh2.1 bilioni, ambapo kila kimoja kimepewa Sh700 milioni za ujenzi na ununuzi wa vifaa tiba.
Amewahimiza wananchi kuhakikisha wanashirikiana kikamilifu kuchangia nguvu kazi kama ujenzi ili kupunguza gharama na hatimaye kujenga majengo zaidi ya yaliyopangwa.
Mkazi wa kata ya Daudi, Solomon Yaro amesema hivi sasa kituo cha afya cha eneo hilo kimeboreshwa kupitia fedha hizo na sasa hawaendi Mbulu Mjini kufuata huduma ya afya.
No comments:
Post a Comment