Mabaki ya manowari ya Marekani ambayo ilizamishwa wakati wa vita vya pili vya dunia yamegunduliwa nje ya pwani ya Australia.
Manowari ya USS Lexington iligunduliwa umbali wa kilomita 3 chini ya bahari karibu kilomita 800 kutoka pwani ya Australia.
Manowari hiyo ilikuwa ilitoweka wakati wa vita vya Coral Sea, kati ya tarehe 4-8 Mei mwaka 1942. Zaidi ya wanajeshi 200 waliuawa wakati wa kuzama kwa meli hiyo.
Jeshi la wanamaji la Marekani lilithibitisha kuwa meli hiyo ilikuwa imegunduliwa na kundi la kutafuta, linaloongozwa na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Paul Allen.
Picha zilionyeha mabaki ya meli hiyo yakiwa bado katika hali nzuri.
Tangazo la kugunduliwa meli hiyo na ndege 11 kati ya 35 ilizokuwa imebeba, lilitolewa na kampuni ya Bw Allen ya Vulcan siku ya Jumapili
Adm Harry Harris, mkuu wa kikosi cha jeshi la Marekani huko Pacific alisifu ugunduzi huo.
- Nyambizi ya Ujerumani iliyozama wakati wa vita vya kwanza vya dunia yapatikana
- Bomu kubwa la vita vya pili vya dunia kuharibiwa Ujerumani
Vita vya Coral Sea vinatajwa kama hatua kubwa ya kuizuia Japan kuwa na ushawishi huko Pacific wakati wa vita.
Jeshi la Marekani lilisema kuwa wanajeshi 216 waliuawa wakati meli hiyo ilishambuliwa. Zaidi wa wengine 2,000 waliokolewa.
"Lexington ilikuwa kwenye orodha yetu kwa sababu ilikuwa moja ya meli kuu zilizotoweka wakati wa vita vya pili vya dunia," Msemaji wa Vulcan Robert Kraft alisema.
Picha zinaonyesha majina ya Lexington na bunduki zake. Baadhi ndege za meli hiyo pia nazo zinaonekana zikiwa hali nzuri.
Meli hiyo haitaondolewa baharini kwa sababu jeshi la wanamaji la Marekani linaitaja kuwa kaburi la vita.
Bw Kraft alisema imechukua karibu miezi sita ya kupanga kupata meli hiyo.
Mwaka uliopita Vulcan ilingundua mabaki ya meli ya USS Indianapolis, ambayo ilizama mwezi Julai mwaka 1945.
Imegundua vyombo vingine vikiwemo meli ya vita ya Japan, Musashi na nyingine ya Italia Artigliere zote kutoka eneo hilo.
No comments:
Post a Comment