Baadhi ya maeneo nchini Kenya yameathirika vibaya baada ya mafuriko ya ghalfa kukata mawasliano ya barabara.
Ripoti kutoka maeneo mbalimbali nchini humo zinaeleza kuwa nguvu ya maji ilikuwa kubwa hivyo baadhi ya watu na magari kusukumwa.
Shirika la Msalaba Mwekundu imeripoti kuwa watu watano waliokuwa kwenye lori walisukumwa na maji eneo la Kitui kilomita 180 Mashariki mwa Nairobi.
Shirika la Msalaba Mwekundu kwenye ukurasa wake wa Twitter imesema baadhi ya barabara nchini humo zimeharibiwa ikiwemo barabara ya Kajiado-Namanga kusini mwa Kenya, na kufanya eneo hilo kushindwa kupitika.
Maelfu ya wakazi wa Nairobi wamekwama na kushindwa kuendelea na shughuli zao kwa sababu ya mvua hizo.
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo miundo mbinu ya barabara za miji ya Nairobi haziwezi kumudu.
Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Nairobi yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.
Kawaida msimu wa mvua nchini Kenya huwa kati ya mwezi Machi na Mei, lakini wadadisi wanasema kuwa safari hii mvua imenyesha kwa wingi zaidi.
Mbinu za kubaki mkavu wakati wa mvua:
Ukimbie au utembee?
Mwanafizikia aliwasilisha mawazo mapya kuhusu ni namna gani ya kuendelea kuwa mkavu wakati wa kutembea kwenye mvua.
Ukikimbia, unaepuka kuloa kwa muda mfupi, hata hivyo utaendelea kuangukiwa na matone zaidi. Je kasi kiasi gani inahitajika?
Franco Bocci, akiongea na jarida la masuala ya Fizikia la Ulaya,anasema kwa pamoja uelekeo wa upepo na kimo cha mtu vinaweza kuwa na majibu.
Mara nyingi, jibu la ujumla ni kukimbia haraka iwezekanavyo: lakini jibu hili linabadilika kutokana na upepo na wembamba.
Mwaka 1987, mtafiti mwingine mwenye asili ya Italia alitetea kwenye jarida kuwa kubadili mbinu hakuthibitishi utofauti huo.
Mwaka 2011, mtaalam wa kutengeneza nguo alitumia jarida hilohilo akisema kuwa kasi inahitajika, kutegemea na uelekeo wa upepo.
Kitu kinachofanya swali hili kuwa gumu ni pamoja na umbo la mwanadamu.
Profesa Bocci alibaini kuwa jibu la suala hili linategemea urefu, upana, uwiano pia uelekeo wa upepo na ukubwa wa matone ya mvua
No comments:
Post a Comment