Serikali imekataa wito unaotaka Marekani iingilie kati mgogoro wa sasa wa kisiasa dhidi ya upinzani.
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Macharia Kamau amesema hakuna haja ya mazungumzo kwa kuwa Kenya imefanikiwa kupitia mzunguko wa uchaguzi wa miaka mitano na sasa inazingatia kuwahudumia raia wake.
Kamau alikuwa akijibu makala iliyochapishwa mwishoni mwa mwezi uliopita na mabalozi wa zamani wa Marekani nchini Kenya Johnnie Carson na Mark Bellamy ambao walitaka Marekani iingilie kati hali ya Kenya.
"Jibu letu kwa ombi la kipuuzi la waandishi kutaka uingiliaji wa Marekani nchini Kenya kwa sauti kubwa ni hapana, shukrani," amesema katika taarifa Jumanne.
"Hiki ni kielelezo cha wazi cha jinsi mawazo yaliyotangulia na yaleyale juu ya Afrika kutoka kwa wataalamu hawa wa nchi za Magharibi wanavyoathiri uzoefu wowote na maarifa ambayo wanaweza wawe wameyapata katika bara. Weledi wao wa kukosea juu ya masuala ya Kiafrika na ya Kenya siyo tu unashangaza bali pia unaonyesha kwa nini tafiti zinazofanywa kwenye madawati juu ya Afrika, na chanzo pekee cha habari kikiwa kile kinapendelea vyombo vya habari vya Magharibi, unapaswa kushughulikiwa kikamilifu kwa kukataa," amesema.
Msemaji wa Rais Uhuru Kenyatta Manoah Esipisu alionekana kuthibitisha kuwa, kwa kweli, huo ndio msimamo alionao Mkuu wa Nchi.
"Katibu Mkuu amesema na huo ndiyo msimamo. Je, unataka kuongeza nini?" ameuliza.

No comments:
Post a Comment