Bodi hiyo imetambulishwa leo jijini Dar es Salaam Machi 15, 2018 itakayohudumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Akitangaza bodi hiyo yenye wajumbe kumi, Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo amewataja kuwa Rais wa MCT, Jaji mstaafu Thomas Mihayo na Makamu wake, Hassan Mitawi.
Wajumbe wengine ni Kajubi Mkajanga,Wakili Anna Henga, Edda Sanga, Barnadina Chahali, Jaji Juxon Mlay, Dk Edmund Mndolwa, Wallace Mauggo na Machumu.
Nsokolo amesema ana imani bodi hiyo italeta mabadiliko katika baraza hilo na ufanisi wa tasnia ya habari nchini kutokana na aina ya wajumbe na umahiri wao katika kada mbalimbali.
Awali, Rais wa MCT, Jaji Mihayo aliitaja bodi inayomaliza muda wake akiwamo yeye mwenyewe na makamu wake, Hassan Mitawi kuwa ni, Wallace Mauggo, Dk Edmund Mndolwa, Jaji Juxon Mlay, Rose Mwalimu,Tuma Abdallah, Badra Masoud, Bernadeta Killian na Ali Mufuruki.
No comments:
Post a Comment