Mkusanyiko wa picha nzuri zaidi kutoka Afrika na kuhusu Waafrika maeneo mbalimbali duniani wiki hii.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionSkauti wa Kike wa Kenya ni miongoni mwa mamilioni ya watu waliosheherekea siku ya Wanawake duniani siku ya AlhamisiHaki miliki ya pichaEPAImage captionMashabiki wa Gor Mahia ya Kenya wakienda nyumbani kwa mbwembwe kuiona timu ya Tunisia club Esperance katika Michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika walitoka sare ya 0-0Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionHuyu ni shabiki wa Al Ahly ya Misri akiwa amewasha moto kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo timu yake ilishinda 4-0 dhidi ya Mounana Gabon.Haki miliki ya pichaAFPImage captionMechi hii ilichezwa kwenye kituo cha kutunza wahamiaji nchini Libya.Ilikutanisha Timu ya Senegal(Kijani) na Cameroon(rangi ya chungwa).Haki miliki ya pichaAFPImage captionWacheza mieleka wa Dambe wa Kaskazini mwa Nigeria wakipimana nguvu kusini mwa Lagos. Dambe ni aina ya mchezo wa kupigana.Haki miliki ya pichaAFPImage captionMwanakikundi wa sanaa ya sarakasi wa Kibera nchini Kenya, akipumua kwa huku akitoa moto mdomoni wakati wa maonyesho jijini Nairobi Jumatano.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMuigizaji wa Kenya Lupita Nyong'o alitumia uzi wa dhahabu kupamba nywele zake kwa mtindo kutoka Rwanda wakati wa sherehe za Oscar siku ya Jumapili.Haki miliki ya pichaEPAImage captionHali ya hewa ya baridi iliyokumba Ulaya Mashariki wiki hii pia kulikuwa na hali ya kuanguka kwa barafu katika milima ya Atlas nchini MoroccoHaki miliki ya pichaAFPImage captionFamilia hii ni moja kati ya maelfu ya watu waliokimbia machafuko Mashariki mwa Congo.Wametumia boti kuvuka Ziwa Albert kuelekea UgandaHaki miliki ya pichaAFPImage captionSiku ya Jumatatu, wanaume na wanawake walionekana wakitafuta dhahabu mjini Makeni, Sierra LeoneHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionUchaguzi wa siku ya Jumatano ulikuwa wa amani, isipokuwa maandamano yalishuhudiwa nje ya Jengo la Ofisi ya wapinzani la Sierra Leone Peoples Party (SLPP)Haki miliki ya pichaAFPImage captionNchini Ivory Coast, kulikuwa na maandamano yanayodaiwa kupinga vitendo vinavyoelezwa visivyo haki vya watoa huduma za mazishi.Haki miliki ya pichaEPAImage captionKikundi cha wahamiaji wa Eritrea nchini Israel wakiwa wanapata picha ya pamoja kwa kuwa wanaondoka kwenye Kituo cha Holot nchini Israel, Kituo hicho kilicho katikati mwa Jangwa kinatarajiwa kufungwa lakini kwa sasa ni kituo huria ambapo wanaoshikiliwa wanakuwa huru kuondoka saa za mchana na kurejea usiku.Shirika la habari la Ulaya limeripoti.
No comments:
Post a Comment