Kampuni ya magazeti ya Mwananchi inatowa wito kwa mamlaka ya usalama kuwasiadia kumtafuta au kutoa habari kuhusu kutoweka kwa mwandishi wao Azory Gwanda.
Mkurugenzi mtendaji wa Mwananchi, Francis Nanai akizungumza na Sauti ya Amerika anasema wametoa taarifa Jumatatu baada ya kupokea habari kutoka familia yake kwamba Gwanda ametoweka tangu Novemba 21 huko mjini Kibiti karibu na Dar es Salaam.
Nanai anasema kwa vile ni mwandishi wa kujitegemea hajakua na mawasiliano ya kila siku na kampuni isipokua wakati kuna habari muhimu ya kuripoti na hivyo hakuna mawasiliano ya siku hadi siku na Gwanda.
Anasema mara ya mwisho kuwasilisna na mwandishi huyo wa Mwananchi ilikua Novemba 20 na tangu wakati huo hapatikani kwenye simu zake tatu.
Gwanda mwenye umri wa miaka 42 amekua akiandika mfululizo wa ripoti juu ya kutoweka kwa raia na maafisa wa usalama katika mji wa Kibiti, na haifahamiki ikiwa hiyo ndio sababu ya kutekwa kwake.
No comments:
Post a Comment