Saturday, November 25

Watu 235 wauawa katika shambulio la msikiti Misri

Wanamgambo waliulenga msikiti mmoja karibu na eneo la al-ArishHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWanamgambo waliulenga msikiti mmoja karibu na eneo la al-Arish
Wanamgambo wametekeleza shambulio la bomu na ufyatuaji wa risasi katika msikiti mmoja uliopo kaskazini mwa eneo la Sinai na kuwaua takriban watu 235 kulingana na chombo cha habari cha taifa.
Walioshuhudia wanasema kuwa msikiti wa al-Rawda katika mji wa Bir al-Abeid , karibu na al-Arish ulilengwa wakati wa ibada ya Ijumaa.
Misri imekuwa ikikabiliana na wanamgambo katika eneo hilo tangu 2013.
Kumekuwa na mshambulio ya mara kwa mara yanayolaumiwa kutekelezwa na wanamgambo katika rasi ya Sinai lakini hilo ni shambulio baya zaidi kuwahi kufanyika.
Picha katika eneo la mkasa huo zinaonyesha damu iliomwagika ndani ya msikiti.
Ramani ya eneo la al-Arish
Image captionRamani ya eneo la al-Arish
Takriba watu 125 walijeruhiwa ripoti zinasema.
Ripoti moja inasema kuwa waliolengwa ni wafuasi wa maafisa wa usalama waliokuwa wakitekeleza ibada katika msikiti huo.
Wakaazi wa eneo hilo wanasema kuwa wafuasi wa madhehebu ya Sufi hukongamana katika msikiti huo.
Makundi ya wanajihad likiwemo lile la Islamic State wanawaona wasufi kama watu wasioamini.
Rais Abdul Fattah al-Sisi anatarajiwa kukutana na maafisa wa usalama kuzungumzia kisa hicho .

No comments:

Post a Comment