Mgeni rasmi Bi. Butano Philipo wakiwa na Mwenyekiti wakizindua vitabu mbalimbali ikiwemo kitabu cha Ufugaji wa samaki.
Chama cha wanawake wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo,Uvuvi na Mazingira, Tanzania association of women leaders in agriculture and environment ( TAWLAE) wamefungua rasimi mkutano wa mwaka wa 21 na kuhudhuriwa na Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa raisi bi Butamo Philipo kwa niaba ya waziri wa Mazingira Mhe. January Makamba ambao umefanyika jana katika viwanja vya wizara ya mifugo na uvuvi.
Akizungumza katika mkutano huo wenyekiti wa chama cha wanawake kiongozi katika kilimo na mazingira Dkt. Sofia Mlote amesema Lengo kubwa la mkutano huo ni kuunganisha wakulima na tafiti mbalimbali zilizoandaliwa na wataalamu hao.
Maadhimisho ambayo yamebeba kaulimbiu isemayo uchumi wa viwanda Tanzania wanawake tupo tayari,hapa ni kazi tu.
Aidha, Dkt. Sofia Mlote amesema kazi ya TAWLAE ni kuwaunganisha wakulima wadogo au wakubwa na tafiti mbalimbali ambaozo zimetafitiwa hapa nchini ili kuongeza uwekezaji na ajira kwa watanzania katika kilimo.
Akizungumza Dkt.Mlote amesema kilimo kilikuwa na faida ndogo kwa sababu utalaam,teknolojia na juhudi zilikuwa bado hazijatumika vizuri katika kilimo
kuingia na uchumi wa viwanda ni lazima uzalishaji wa kilimo uwe na tija , kuwepo na uboreshaji wa masoko na teknolojia ambapo wataalamu wanawake ndio wanajukumu kubwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo alisema Dkt.Mlote
Getrude Mongela mlezi wa Tawlea ambaye ana PHD ya Philosophy alisema wanawake Uchumi wa viwanda Tanzania wanawake tupo tayari , Hapa kazi tu.
Vile vile amefarijika kuona amelea wanawake toka wakiwa wadogo na sasa wamesoma na wengine wana PHD lengo kubwa hasa alisistiza mpaka kufikia 2020 wanawake wawe wamekua kiuchumi na kuendelea kutoa wasomi wa kutosha na kufikia malengo.
Kiongozi wa Chama cha Wanawake viongozi katika Kilimo na Mazingira Dkt. Sophia Mlote akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya makamu wa raisi Bi. Butano Philipo katika uzinduzi wa mkutano huo leo.
No comments:
Post a Comment