Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe hilo jana, alisema kiwanja hicho kinajengwa na mkandarasi Mtanzania kwa kiwango cha kimataifa.
Profesa Mbarawa alisema: “Tunahitaji maendeleo na Serikali hii imefufua shirika la ndege na tayari imenunua ndege sita ambazo zitafanya kazi ndani na nje ya nchi. Kila mkoa utakuwa na kiwanja cha ndege cha kisasa kitakachohudumia wananchi wasiopungua 100.”
Alisema uwapo wa viwanja vya ndege nchini kutakuza na kuchochea uzalishaji kwenye sekta ya viwanda, madini uvuvi na ufugaji.
Waziri Mbarawa alisema katika awamu hii ya tano, wizara imeboresha na kuimarisha ujenzi katika viwanja vya ndege vya Lindi, Iringa, Moshi na Simiyu.
Pia, alisema katika bajeti ya mwaka 2017/18 Serikali imepanga kufanya upembuzi katika viwanja vya Iringa, Musoma na Songea na sasa wanatafuta makandarasi.
Awali, mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale alisema kiwanja hicho kina ukubwa wa kilometa tatu.
Ujenzi huo ulioanza Septemba 2016 umeshajengwa kwa asilimia 52 na unategemewa kuchochea shughuli za maendeleo wilayani Chato na Mkoa wa Geita kwa jumla.
Mbunge wa Geita, Dotto Biteko aliishukuru Serikali kwa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Chato akisema kitachochea maendeleo ya mkoa huku akimwomba Profesa Mbarawa kusaidia ujenzi wa barabara inayounganisha Wilaya ya Bukombe na Geita yenye urefu wa kilometa 60.
No comments:
Post a Comment